Kinana na CCM tunaomba majibu ya kero hizi za Muungano

Kinana na CCM tunaomba majibu ya kero hizi za Muungano

jiwe angavu

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2015
Posts
20,419
Reaction score
39,217
Kuna ukweli tunatotakiwa kuufafanua na kama ni kero irekebishwe kama kweli tunafikiri muungano huu ni wa muhimu.

1. Wazanzibar wengi sana wanamiliki ardhi na majengo bara, kama raia. ila Wabara wanachukiwa wakienda kule, wanaitwa chogo, na katiba yao inazuia watu wa bara kumiliki ardhi. Juzi nilikuwa Dodoma, kwenda benjamin Mkapa kwenye kona ya Udom, kuna migorofa fulani hivi imejengwa, wanasema karibu na vile vijengo vya majaji, wengine wanamtaja mzanzibari fulani anamiliki hiyo migorofa. tukisema wazanzibar leo hii muungano umevunjika waondoke, wengi wataanza kuuza nyumba nyingi na ardhi kubwa wanayoimiliki. KWANINI BARA HATURUHUSIWI KUMILIKI KULE? faida yao ni nini?

2. Kwenye ajira, hii ni kero, wazanzibar maelfu na maelfu wameajiriwa bara, hata kwenye mambo yasiyo ya muungano, wameajiriwa bara ambayo kiukweli ipo bara kwasababu zanzibar kuna utawala wao, lakini wabara hawaruhusiwi kabisa kuajiriwa zanzibaar, hii ni kero, inatakiwa iondolewe, ama la kila mtu abaki kwake.

3. Wazanzibar wanakuwa wabunge kule kwao, na huku. akiwa mbunge kule kwao, atakula masurufu ya kule na atakuja kula masurufu ya bara kwa kodi za watu wa bara. tuambieni, yale mipesa wanaku wabunge 50 wa zanzibar wanakiula, zanzibar huwa imechangia bei gani? ni pesa za walipa kodi wa bara. na hao hao wakifika huku wakishiba, wanasenma twende kule kwa passport, kwa msiojua, kile ameongea yule mbunge wa zanzibar kwamba wabara twende kwa passport kwao ndicho kilichopo kwenye mioyo ya wazanzibari wote hata wenye mamlaka huku na hata walioajiriwa huku na hata wanaomiliki ardhi huku, amesema kilichopo kwenye mioyo ya wengi. wala hatakiwi kulaumiwa. kwa waliofika zanzibar wanajua kuwa hicho ndio huwa matamanio yao.

4. Mzanzibar anaweza kuwa Mkuu wa wilaya, mkoa, na waziri bara, ila sisi kule marufuku. kwanini?

Nimeongea hayo kwa uchache tu, lakini ukweli mwingi hata wanaopinga wanaujua, kama tunataka muungano uwepo, ondoeni kero hizi kwa watu wa bara, ama la, kila mtu achukue hamsini zake kwasababu hakuna kitu wabara wanafaidika nacho as of now. na hawajawahi kufaidika. watu wasioelewa watasema huu ni uchochezi, ila jibuni kwa hoja kama mnazo.

Credit Yesu Anakuja

PIA SOMA
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?
 
Haya

Jibu rahisi sana

Kila Mzanzibar ni Mtanzania kwa mujibu wa Katiba ya JMT 1977 lakini siyo kila Mtanzania ni Mzanzibar kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya 1984
Kwa hiyo unakili kuwa Muungano unalalia upande mmoja??

Kwa hali hii wakiondoka hawa wazee, vijana hawa wa leo watapasua hii meli lizame!

It's just a matter of time.
 
Kinana ni spent force hawezi tena kujibu sense
 
wengine wanamtaja mzanzibari fulani anamiliki hiyo migorofa. tukisema wazanzibar leo hii muungano umevunjika waondoke, wengi wataanza kuuza nyumba nyingi na ardhi kubwa wanayoimiliki. KWANINI BARA HATURUHUSIWI KUMILIKI KULE? faida yao ni
Kula nao usiwaguse mikono waache kunuke ndipo watajua
 
Kinana ni spent force hawezi tena kujibu sense
Kinana kasema ukweli Mbunge anawakilisha Hoja na Ndio sababu kuna Wakati Tundu Antipas Lisu, Zitto Kabwe na JJ Mnyika wakiwa wabunge walikuwa wanabeba Hoja za Tanganyika nziima
 
Maoni, ushauri, maswali, na mitazamo kuhusu muungano imara sana waJMT, yawasilishwe kwa maandishi katika wizara na taasisi mahususi zinazohusika kwa maelezo zaidi :whatBlink:
 
Kinana badala ya kumjibu Tundu Lissu angeenda kufanya vikao na wenzake wa ccm kurekebisha madudu waliyoyatengeneza.
CCM ndiyo iliyoharibu huu Muungano hivyo wachague moja ama wawajibishe au tubadilishe muundo wa muungano uliopo.
 
Haya

Jibu rahisi sana

Kila Mzanzibar ni Mtanzania kwa mujibu wa Katiba ya JMT 1977 lakini siyo kila Mtanzania ni Mzanzibar kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya 1984
Hilo ndilo hatutaki, wataondoka tu as long as majority ya Tanganyikans linawakera, kuna siku wewe na mimi hatupo duniani wataondoka na kuacha kila kitu
 
Back
Top Bottom