Uchaguzi 2020 Kinana na Membe 2020 wanaitosha CHADEMA

Uchaguzi 2020 Kinana na Membe 2020 wanaitosha CHADEMA

Chama changu kisirudie makosa ya kumkaribisha fisadi lowassa 2015 kisha kumteua kama mgombea wa Urais. Kama Membe na Kinana wanataka kuhamia Chadema na uongozi wa Chadema unaridhia basi waruhusiwe lakini HAWASTAHILI kuteuliwa kugombea nafasi yoyote ile katika Uchaguzi wa 2020.

Fool me once shame on you, fool me twice shame on me.
Sahihi
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mi nimeona kama msigwa anamsafisha kinana huku akilaumu aliyemwamini kuwa anampa habari yakweli. Na yeye kwavile ndo in charge ikamfanya atende.

Japo siasa ni kama ajira zingine ..maslahi mbele
 
Upinzani mkubwa ulikuepo wakati vyama vilipokua na kina Dr slaa, Mrema, Lipumba, Seif na Hamad. Sioni chama kinachoweza kuinyima usingizi CCM kwa sasa. Zama hizi siasa za kupingana sio kazi tenatena tutafute kazi nyingine za kufanya
 
Tetesi kitaa zinasema, wale maswahiba wakubwa wa JK enzi zake, Abdulrahman Kinana a.k.a. Mzee wa Tembo, na Bernard Membe a.k.a Jasusi, wanaungana nguvu kuchapisha tiketi yao ya kupeperusha bendera ya CHADEMA 2020.
Duuuh . . . . another mistake in the making. Sasa hivi hatutaki kuchezewa. Tumechoka siasa zenu za kijinga na zisizo na msimamo. Leo wapinzani wakubwa kesho mnakaribisha maccm wagombee upuuzi tu.
 
Upinzani mkubwa ulikuepo wakati vyama vilipokua na kina Dr slaa, Mrema, Lipumba, Seif na Hamad. Sioni chama kinachoweza kuinyima usingizi CCM kwa sasa. Zama hizi siasa za kupingana sio kazi tenatena tutafute kazi nyingine za kufanya
Ila ile CHADEMA ya Dr Slaa na Zitto ilikuwa vizuri kwa kweli
 
Tetesi kitaa zinasema, wale maswahiba wakubwa wa JK enzi zake, Abdulrahman Kinana a.k.a. Mzee wa Tembo, na Bernard Membe a.k.a Jasusi, wanaungana nguvu kuchapisha tiketi yao ya kupeperusha bendera ya CHADEMA 2020.

Msidhani msigwa kakurupuka kuanza kumsafisha Kinana. Chadema wamejifunza toka 2015 ilipowalazimu kutumia kila jukwaa kumsafisha Lowassa badala ya kuuza sera na kumchafua Magu. Mwaka huu, wanajipanga usafi uishe kabla ya kampeni kuanza ili kampeni zikianza, Nyumbu wawe wamemsahau Kinana kama mbaya wa Tembo.

2020 Kutanoga tuu.

NCCR kazi kwenu.
Achilia mbali kufungamana na chama chochote membe simwelewi kwakweli
 
Tetesi kitaa zinasema, wale maswahiba wakubwa wa JK enzi zake, Abdulrahman Kinana a.k.a. Mzee wa Tembo, na Bernard Membe a.k.a Jasusi, wanaungana nguvu kuchapisha tiketi yao ya kupeperusha bendera ya CHADEMA 2020.

Msidhani msigwa kakurupuka kuanza kumsafisha Kinana. Chadema wamejifunza toka 2015 ilipowalazimu kutumia kila jukwaa kumsafisha Lowassa badala ya kuuza sera na kumchafua Magu. Mwaka huu, wanajipanga usafi uishe kabla ya kampeni kuanza ili kampeni zikianza, Nyumbu wawe wamemsahau Kinana kama mbaya wa Tembo.

2020 Kutanoga tuu.

NCCR kazi kwenu.
Chadema imeshajifunza kupitia upuuzi uliofanywa na Mbowe mwaka 2015 wa kumkumbatia na kumsafisha mtu waliyemuita fisadi.

Itakuwa ni ushamba wa karne kufanya usajili wa kilofa kama ule wa 2015
 
Hapo inategemea kama watafanikiwa kutoboa 2020 au itakuwaje. Wasipotoboa, na NCCR ikawa kubwa kuliko Chadema bungeni, 2022 watarudi tu bila shida. Lakini wakipeta, CCM wajiandae kuhama nchi [emoji16][emoji16][emoji16]
Ccm haiwezi kushindwa uchaguzi, labda ikose support ya vyombo vya ulinzi.
Maana kwa kutegemea sanduku la kura hawawezi kupata kura
 
CCM form za urais mnatoa lini tukachukue?
 
Tetesi kitaa zinasema, wale maswahiba wakubwa wa JK enzi zake, Abdulrahman Kinana a.k.a. Mzee wa Tembo, na Bernard Membe a.k.a Jasusi, wanaungana nguvu kuchapisha tiketi yao ya kupeperusha bendera ya CHADEMA 2020.

Msidhani msigwa kakurupuka kuanza kumsafisha Kinana. Chadema wamejifunza toka 2015 ilipowalazimu kutumia kila jukwaa kumsafisha Lowassa badala ya kuuza sera na kumchafua Magu. Mwaka huu, wanajipanga usafi uishe kabla ya kampeni kuanza ili kampeni zikianza, Nyumbu wawe wamemsahau Kinana kama mbaya wa Tembo.

2020 Kutanoga tuu.

NCCR kazi kwenu.
Wewe umeleta jambo jema lakini ukashindwa kulieleza vizuri, au ulilielewa kivingine kabisa.

Sasa ngoja nikupashe:

Sio Kinana tu na Membe, CHADEMA inawapasa wawatafute viongozi wengi waliopo huko CCM ambao wamechukizwa sana na mambo yanayoendelea ndani ya serikali yao.
Viongozi hawa wapo wengi, kati yao wakiwepo waliokwishastaafu, na baadhi ambao bado wamo kwenye chama wakiumia ndani kwa ndani.

Mtu kama Kinana hana shida tena ya kushika cheo ndani ya serikali yoyote hata kama akiifanyia kazi CHADEMA.

Mtu kama huyu akikubali kupiga kazi, hata kimya kimya tu akitumia mtandao wake aliokuwa akiutumia akiwa Katibu Mkuu atasababisha uharibifu mkubwa sana kwa hawa waliolewa madaraka.

Wapo viongozi wengi sana wenye ushawishi mkubwa kama yeye. CHADEMA na wapinzani wenzao wanachotakiwa kukifanya ni kuwaendea hawa viongozi wawape ushirikiano.

Wakifanya hivi kazi yao itarahisishwa ya kutosha ili kuiangusha CCM.

Wasilotakiwa kulifanya ni kuwaingiza ndani ya chama na kugombea vyeo kabla ya uchaguzi.
 
Napenda jinsi unpredictability ya CHADEMA inavonyima watu usingizi!

Sent using Jamii Forums mobile app
Safari hii, kama sio mazingaombwe yanayofanyika, huenda wakatia maajabu maanake inaonekana hawatabiriki- na hili ni jambo jema kwao; kwa sababu hasimu yao mkuu naye amejawa wasiwasi tupu. Angalia tu hata humu JF wanavyohangaika!
 
Back
Top Bottom