Kinana: Serikali tatu ni hatari, itasababisha machafuko

Nadhani mahubiri Haya angehubiri akiwa Zanzibar Kule ndiko fujo itaanzia huku tanganyika hakuna shaka hiyo anapoteza muda bure...
 
SERIKALI TATU=kusambaratika kwa Muungano?
How? Why and when maana inaonekana ccm mlisha tengeneza kalenda na kuweka utaratibu kuwa muungano usivunjwe na ukivunjwa tu nchi inaingia katika machafuko.
Twambieni nani ataleta vurugu na machafuko ili tumjue na tumdhibiti, maana kumjua adui ni ushindi tayari.
Kabla ya vyama vingi na vilipoanza mlisema kutakuwa na machafuko. Vyama vingi vikaja na hapo mkasema tukivichagua nchi itaingia katika mapigano. Wakati ule watu waliwaelewa lakini sasa wamejua ni hila za ccm. Sasa hivi tunahitaji kupata majibu ya maswali yetu ya msingi, why how?? Sio porojo.
 
Wewe na nani mnataka Tanganyika, si mlisema Kskazini mnataka kujitenga? Nendeni huko kaskazini.

Acha kuongea kama umebanwa na tumbo la kuhara wewe!!...Kama mnaichukia Tanganyika kiasi hiki huku Rasilimali zake mnaendelea kuzifilisi nendeni kwa Mfadhili wenu China hakika kuna maeneo ya kutosha ya kuishi kule kwaajili ya MaCCM yote yanayoichukia Tanganyika.Mtake msitake Tanganyika yetu lazima irudi la sivyo Nchi mtaiona chungu hii.CCM hamjazoea kutikiswa hata kidogo basi sasa mjiandae kwa hilo na kitakachofuatia ni kwa MaCCM kuhudhuria kesi The Hague!!!??
 
huo ni msimamo wa chama chake. tatizo liko wapi? anaetaka serikali moja sawa, anaetaka 2 sawa na anaetaka 3 sawa. kila mmoja ajenge hoja kwa nini anaunga mkono muundo anaoutaka. mambo ya Somalia yametoka wapi?
 
Sasa hvi ndio kuna machafuko bwana kinana.au machafuko ya huyaoni ya wazanzibari na tanganyika.usionge vitu ambavyo kama vile haunavo akilini.suluhisho la kuendelea machafuko ni serekali tatu tu.hakuna zaidi ya hapo.kama walimwengu watashangaa basi waache washangae tu ila sisi wananchi tunatazama kwa maslahi ya nchi yetu sio ya wengine
 
Hivi wewe hujui kuwa wanaotaka serikali tatu wanalenga kuvunja Muungano, swali ni je kuvunjika kwa muungano kunaweza kuhatarisha amani kutoweka? Nadhani KINANA ana point
Kwani hata muungano ukivunjika hayo machafuko yatatokana na nini tena wakati kila upande utakuwa umepata kile walichokitaka kwa hiari yao?
 
thatha Hebu fafanua serikali tatu zinavyoleta fujo na uvunjifu wa amani, na serikali mbili zinavyodumisha amani, na utuambie AMANI ni nini?
 
Hata muungano ukivunjika kwani kiuna hasara gani zaidi ya faida.huoni wazanzibari wanalia kila siku kwa hio muungano sasa kuna faida gani huo?si bota tu uvunjike ndio bora zaidi.tanganyika watakuwa free na wazanzibar watakuwa free pia.kila nchi itakuwa na mamlaka yake kamili.wananvhi wa zanzibar asilimia 95% hawataki serekali mbili cause itakuja kuelekea moja hapo baadae.na nchi ya znz itakuwa mkoa sio nchi tena.hilo ndilo hawalitaki
 
Mara nyingi wanasiasa hushangaza sana! huyu Kinana anatetea muungano wa serikali mbili ambao umejaa migogoro na kuonekana kutotakiwa na kutoaminiwa na pande zote mbili, haya ni maajabu ya wanasiasa!! CCM katika hili wanasumbuliwa na matatizo yao ya kutopenda mabadiliko kwa kujifanya wao ni wafalme njozi wenye kuona yatakayotokea mbeleni ili hali ni usultani wao tu unawasumbua!. Nani kamwambia kinana kuwa serikali tatu ni machafuko!!!!! Watanzania kwa wingi wamependekeza serikali tatu, CCM wanawanachama si zaidi ya milioni 5 nchini kwanini wadhani kwamba wanahati miliki ya Tanzania na watanzania?
 
thatha Hebu fafanua serikali tatu zinavyoleta fujo na uvunjifu wa amani, na serikali mbili zinavyodumisha amani, na utuambie AMANI ni nini?

Mkuu hilo swali ni la msingi sana kwa wote wanaopinga muundo wa serikali tatu kwa kisingizio cha machafuko bila kuelezea yatatokea kwa namna gani.
 

bora kushangaza dunia kuliko kuwa na muungano huu tulio nao ambao ni kituko---muungano wa maneno usio documented.
 

Utamtambuaje kama ni Msoooomali, matendo jamani matendo.. x4 Aaaaehhhh!
Utamtambua eeeeee..
 
Mkuu hilo swali ni la msingi sana kwa wote wanaopinga muundo wa serikali tatu kwa kisingizio cha machafuko bila kuelezea yatatokea kwa namna gani.

Nadhani ni wakati wa kujua amani ni kitu gani, na pia kuelewa kuwa muundo hauna tatizo, ni kama ramani inayoelekeza namna ya utendaji wa shughuli za serikali zitakavyokuwa, lakini wenyewe ni "abstract". Fujo na AMANI vitatokea kutokana na watu/ watendaji katika muundo huo, kitu ambacho pia kinaweza ama kinatokea katika muundo wa serikali 2 kama wanavyojipambanua. TATIZO SIO MUUNDO BALI WATU/WATENDAJI ndani ya huo muundo!!
 
Hapana Sio sahihi: Kinana nilishuhudia hotuba yake na hakuna mahali aliposema hivi (sina sababu ya kumtetea maana bado iko shida huko juu). Aliyeropoka kaya ni Nape huku povu likimtoka, vyombo vya habari vimemnukuu vibaya. na nakumbuka karibu sehemu zote walizoonyesha hata radio waliotoa hotuba yake, alikuwa makini sana na hata kusema kuwa Serikali ya CCM itafuatilia kwa umakini hoja za wananchi na itawasikiliza, wakiamua serikali tatu sawa wakiamua mbili sawa, jambo ambali Nape hakulisoma akaingia jukwani na kuanza kutokwa na Povu la serikali mbili na vijembe kedekede huku akiweweseka na mzimu wa CHADEMA ambao nahisi umemkalia kooni, na sijui kwanini.

cc: TECH WIZ, wema_1, babalao 2, MAPUMA MIYOGA, Kongolo
 

Sababu alizotoa Kinana za kupinga Serikali tatu ndizo hizo hizo zinahusika pia kupinga Serikali mbili! Sijui kwa nini anaunga Serikali mbili wakaati akijua Zanzibar huru inaweza kuagiza vifaru vyake, submarine zake na ikatangaza vita bila kuhusisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano! Kwa nini hasa asiseme Serikali moja ni bora kuliko mbili au tatu? Duniani tayari wanatushangaa kuwa na Serikali mbili ndani ya 'nchi moja' na kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungaano anaweza kuwa chini ya Raisi wa Zanzibar katika matukio ya kitaifa! Wanaounga serikali mbili haya hawayasemi kwa sababu wameyatengeneza wao waliporuhusu Zanzibar kuwa huru! lakini kubwa ni kuwa mapendekezo yao waliyotoa ya serikali mbili hayatatui tatizo bali yanaliongezea na yanatugawa zaidi kama taifa - kwa kuruhusu Zanzibar kuwa mwanachama wa UN!
 
bora kushangaza dunia kuliko kuwa na muungano huu tulio nao ambao ni kituko---muungano wa maneno usio documented.
Kama ni dunia mbona tumeishangaza kwa mengi tu! Kwa mfano; wanafunzi kufaulu mitihani bila kujua kusoma na vituko vingine kibao tu.
 

Blue: CCM ndo inashangaza dunia, mfano Ujerumani Mashariki na Magharibi zilipoungana ziliamua kuwa na serikali moja, Federal Republic of Germany, lakini Taganyika/Zanzibar = Tanzania na serikali 2, ajabu hilo, error of incosistency 1+1=2!
Maroon/Pink: reference yake ni nini? Tukichukulia modal states kama USA ina Federal States 51 na kila 1 ina internal gornance systems na sheria zake ambazo unakuta haziingiliani/hazitumiki na state nyingine, lakini maendeleo yapo juu! Hata Uchina province governments ziko OK (Hong Kong, Macau, ...), labda kama anarejea mfumo wa failed former USSR!
Red: Kwani CCM ni nani haswa na upinzani ni nani? Wanachama wa CCM na upinzani si ni raia wanaotaka katiba mpya? Kwanini CCM iseme ...hawahitaji shinikizo.... wakati wao wanashinikiza... mf. serikali mbili? Hii si double standards with hidden and vested interests from a certain hidden group of greed individuals within rulinng elite like Kinana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…