ChescoMatunda
JF-Expert Member
- Jan 7, 2009
- 1,232
- 442
Nadhani mahubiri Haya angehubiri akiwa Zanzibar Kule ndiko fujo itaanzia huku tanganyika hakuna shaka hiyo anapoteza muda bure...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
How? Why and when maana inaonekana ccm mlisha tengeneza kalenda na kuweka utaratibu kuwa muungano usivunjwe na ukivunjwa tu nchi inaingia katika machafuko.SERIKALI TATU=kusambaratika kwa Muungano?
Wewe na nani mnataka Tanganyika, si mlisema Kskazini mnataka kujitenga? Nendeni huko kaskazini.
Kwani hata muungano ukivunjika hayo machafuko yatatokana na nini tena wakati kila upande utakuwa umepata kile walichokitaka kwa hiari yao?Hivi wewe hujui kuwa wanaotaka serikali tatu wanalenga kuvunja Muungano, swali ni je kuvunjika kwa muungano kunaweza kuhatarisha amani kutoweka? Nadhani KINANA ana point
thatha Hebu fafanua serikali tatu zinavyoleta fujo na uvunjifu wa amani, na serikali mbili zinavyodumisha amani, na utuambie AMANI ni nini?
Katibu mkuu wa CCM taifa Kinana akihutubia wananchi wa shinyanga vijijini amesema CCM inaendelea na msimamo wake wa serikali mbili na kupinga muundo wa serikali tatu kuingizwa kwenye katiba mpya kwa kuwa, serikali tatu ni hatari, itasababisha machafuko na vile vile eti itashangaza dunia.
Source gazeti Mtanzania la leo.
Je kuna ukweli gani katika kauli hii ya Kinana ambayo pia ndio msimamo wa CCM?
Kinana unaongea wewe?Tunaitaka Tanganyika yetu usituletee habari za machafuko hapa kama huitaki Tanganyika wewe na wenzako hamieni Nchi nyingine!
Mara nyingi wanasiasa hushangaza sana! huyu Kinana anatetea muungano wa serikali mbili ambao umejaa migogoro na kuonekana kutotakiwa na kutoaminiwa na pande zote mbili, haya ni maajabu ya wanasiasa!! CCM katika hili wanasumbuliwa na matatizo yao ya kutopenda mabadiliko kwa kujifanya wao ni wafalme njozi wenye kuona yatakayotokea mbeleni ili hali ni usultani wao tu unawasumbua!. Nani kamwambia kinana kuwa serikali tatu ni machafuko!!!!! Watanzania kwa wingi wamependekeza serikali tatu, CCM wanawanachama si zaidi ya milioni 5 nchini kwanini wadhani kwamba wanahati miliki ya Tanzania na watanzania?
Mkuu hilo swali ni la msingi sana kwa wote wanaopinga muundo wa serikali tatu kwa kisingizio cha machafuko bila kuelezea yatatokea kwa namna gani.
Hapana Sio sahihi: Kinana nilishuhudia hotuba yake na hakuna mahali aliposema hivi (sina sababu ya kumtetea maana bado iko shida huko juu). Aliyeropoka kaya ni Nape huku povu likimtoka, vyombo vya habari vimemnukuu vibaya. na nakumbuka karibu sehemu zote walizoonyesha hata radio waliotoa hotuba yake, alikuwa makini sana na hata kusema kuwa Serikali ya CCM itafuatilia kwa umakini hoja za wananchi na itawasikiliza, wakiamua serikali tatu sawa wakiamua mbili sawa, jambo ambali Nape hakulisoma akaingia jukwani na kuanza kutokwa na Povu la serikali mbili na vijembe kedekede huku akiweweseka na mzimu wa CHADEMA ambao nahisi umemkalia kooni, na sijui kwanini.* Asema Tanzania itashangaza dunia
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeendeleza msimamo wake wa kupinga muundo wa Serikali tatu kuingizwa katika Katiba mpya, kikisema kuwa muundo huo ni hatari kwa umoja na mshikamano wa taifa.
Chama hicho kimeonya kuhusu muundo huo na kusema kuwa Serikali zaidi ya mbili zinaweza kuvuruga ustawi wa taifa, kwani ni rahisi zaidi nchi kuingia katika machafuko.
Tamko hilo lilitolewa jana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi katika Wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Kinana alisema muundo wa Serikali tatu ni mzigo kwa taifa na kwamba Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kuwa na marais watatu, jambo ambalo halipo duniani kote.
Katiba ni jambo muhimu kwa ustawi wa nchi yetu, lakini katika hili la kuwa na Serikali tatu ni hatari, kwani kwa mujibu wa rasimu yetu ya sasa, inaonyesha kuwa kila Serikali itakuwa na mamlaka kamili.
Ikiwa kutatokea serikali moja kati ya hizo tatu na moja ikasema sasa inanunua vifaa vya kujilinda, basi ile ya Zanzibar nayo itafanya hivyo na ile ya Muungano pia itafanya hivyo.
Hata kama kuna vita serikali moja ikasema hatutaki nyingine itasema tunataka, mwishowe mtaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe, alisema Kinana na kuendelea:
Kwa hali hiyo, ninachotaka kuwaambia ni kuwa Katiba Mpya itaandikwa na maisha yale yale yataendelea. Afrika Kusini, India na Kenya wamebadili katiba zao, lakini hali ya maisha ya wananchi wao iko vilevile, alisema.
Katika mkutano huo, Kinana alisema msimamo wa chama chake kuhusu muundo ni Serikali mbili na kueleza kuwa chama chake kitaheshimu maoni ya Watanzania kuhusu muundo wowote bila shinikizo la kisiasa.
Alisema hatua ya kuwa na wingi wa Serikali kuna hatari ya nchi kuwa na Bunge la Mabwenyenye na Bunge la Makabwela, ambapo alisema kuna hatari ya fedha za walipa kodi kutumika vibaya.
Kinana alionya hatua ya kuwa na ukubwa wa Serikali ambayo itakuwa mzigo kwa Watanzania, ambao wamekuwa wakiendesha kwa kulipa kodi zao.
Hivi sasa nchi ipo katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya, ninapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa CCM itakuwa tayari kupokea maamuzi yoyote yatakayoamuliwa na wananchi.
. Na ikiwa mtaamua kuwa ya Serikali mbili, tatu hata tano sawa, lakini kubwa katika hili CCM hatuhitaji mchakato huu ufanyike kwa kuingiliwa kwa shinikizo kutoka kwa vyama vya upinzani au hata taasisi ambazo zimejificha kwa mlango wa nyuma.
Sisi tulisema wazi tunapenda tuendelee na Serikali mbili, lakini katika hili tambueni kuwa na Serikali nyingi zaidi kuna hatari ya kuingia katika mifarakano na hata vita, alisema Kinana.
Katibu Mkuu huyo alisema kuwa hatua ya baadhi ya watu kupita na kupandikiza chuki kuhusu Katiba Mpya, mawazo yao yanatakiwa kupimwa, kwani watu hao wana lengo la kuvunja badala ya kuimarisha umoja.
Ni muhimu kuandika Katiba mpya ambayo itasaidia kuweka misingi bora na imara ya uongozi, lakini si kuwa na Katiba yenye utitiri wa kila aina ya Serikali, hili hapana, ila ikiwa mtaamua nyie wananchi wenyewe sisi hatuna pingamizi, alisema.
Mapema Agosti mwaka huu, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, aliwataka wanachama wa CCM kujiandaa kisaikolojia na muundo wa Serikali tatu, ikiwa Watanzania wataamua hivyo.
Rais Kikwete alinukuliwa na vyombo vya habari kupitia vikao vya NEC mjini Dodoma, ambapo alisema mwaka 1992, kundi kubwa la wananchi lilipinga kuingia katika mfumo wa vyama vingi, lakini lilisikilizwa na nchi ikaingia kwenye mfumo huo.
Source: Gazeti Mtanzania la leo.
Je kuna ukweli gani katika kauli hii ya Kinana ambayo pia ndio msimamo wa CCM?
* Asema Tanzania itashangaza dunia
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeendeleza msimamo wake wa kupinga muundo wa Serikali tatu kuingizwa katika Katiba mpya, kikisema kuwa muundo huo ni hatari kwa umoja na mshikamano wa taifa.
Chama hicho kimeonya kuhusu muundo huo na kusema kuwa Serikali zaidi ya mbili zinaweza kuvuruga ustawi wa taifa, kwani ni rahisi zaidi nchi kuingia katika machafuko.
Tamko hilo lilitolewa jana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi katika Wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Kinana alisema muundo wa Serikali tatu ni mzigo kwa taifa na kwamba Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kuwa na marais watatu, jambo ambalo halipo duniani kote.
"Katiba ni jambo muhimu kwa ustawi wa nchi yetu, lakini katika hili la kuwa na Serikali tatu ni hatari, kwani kwa mujibu wa rasimu yetu ya sasa, inaonyesha kuwa kila Serikali itakuwa na mamlaka kamili.
"Ikiwa kutatokea serikali moja kati ya hizo tatu na moja ikasema sasa inanunua vifaa vya kujilinda, basi ile ya Zanzibar nayo itafanya hivyo na ile ya Muungano pia itafanya hivyo.
"Hata kama kuna vita serikali moja ikasema hatutaki nyingine itasema tunataka, mwishowe mtaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe," alisema Kinana na kuendelea:
"Kwa hali hiyo, ninachotaka kuwaambia ni kuwa Katiba Mpya itaandikwa na maisha yale yale yataendelea. Afrika Kusini, India na Kenya wamebadili katiba zao, lakini hali ya maisha ya wananchi wao iko vilevile," alisema.
Katika mkutano huo, Kinana alisema msimamo wa chama chake kuhusu muundo ni Serikali mbili na kueleza kuwa chama chake kitaheshimu maoni ya Watanzania kuhusu muundo wowote bila shinikizo la kisiasa.
Alisema hatua ya kuwa na wingi wa Serikali kuna hatari ya nchi kuwa na Bunge la Mabwenyenye na Bunge la Makabwela, ambapo alisema kuna hatari ya fedha za walipa kodi kutumika vibaya.
Kinana alionya hatua ya kuwa na ukubwa wa Serikali ambayo itakuwa mzigo kwa Watanzania, ambao wamekuwa wakiendesha kwa kulipa kodi zao.
"Hivi sasa nchi ipo katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya, ninapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa CCM itakuwa tayari kupokea maamuzi yoyote yatakayoamuliwa na wananchi.
"…. Na ikiwa mtaamua kuwa ya Serikali mbili, tatu hata tano sawa, lakini kubwa katika hili CCM hatuhitaji mchakato huu ufanyike kwa kuingiliwa kwa shinikizo kutoka kwa vyama vya upinzani au hata taasisi ambazo zimejificha kwa mlango wa nyuma.
"Sisi tulisema wazi tunapenda tuendelee na Serikali mbili, lakini katika hili tambueni kuwa na Serikali nyingi zaidi kuna hatari ya kuingia katika mifarakano na hata vita," alisema Kinana.
Katibu Mkuu huyo alisema kuwa hatua ya baadhi ya watu kupita na kupandikiza chuki kuhusu Katiba Mpya, mawazo yao yanatakiwa kupimwa, kwani watu hao wana lengo la kuvunja badala ya kuimarisha umoja.
"Ni muhimu kuandika Katiba mpya ambayo itasaidia kuweka misingi bora na imara ya uongozi, lakini si kuwa na Katiba yenye utitiri wa kila aina ya Serikali, hili hapana, ila ikiwa mtaamua nyie wananchi wenyewe sisi hatuna pingamizi," alisema.
Mapema Agosti mwaka huu, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, aliwataka wanachama wa CCM kujiandaa kisaikolojia na muundo wa Serikali tatu, ikiwa Watanzania wataamua hivyo.
Rais Kikwete alinukuliwa na vyombo vya habari kupitia vikao vya NEC mjini Dodoma, ambapo alisema mwaka 1992, kundi kubwa la wananchi lilipinga kuingia katika mfumo wa vyama vingi, lakini lilisikilizwa na nchi ikaingia kwenye mfumo huo.
Source: Gazeti Mtanzania la leo.
Je kuna ukweli gani katika kauli hii ya Kinana ambayo pia ndio msimamo wa CCM?
Kama ni dunia mbona tumeishangaza kwa mengi tu! Kwa mfano; wanafunzi kufaulu mitihani bila kujua kusoma na vituko vingine kibao tu.bora kushangaza dunia kuliko kuwa na muungano huu tulio nao ambao ni kituko---muungano wa maneno usio documented.