Kinana: Serikali tatu ni hatari, itasababisha machafuko

Kinana: Serikali tatu ni hatari, itasababisha machafuko

Mi nashangaa Kikwete kwa unafiki kawatoa 'warwanda' kawaacha wasomali! Aziz Ally wana mtaa wao, hadi mkaa wanauza!
 
unaweza ku prove mkuu au ndio viroba asubuhi

Fuatilia vizuri thread hii toka mwanzo pamoja na michango ya wengine utajikuta peke yako ndo upo tofauti. Inawezekana hujaelewa au unataka malumbano tu. Unataka kuprove nini? Kwamba kinana na CCM wana msimamo waserikali mbili au?
 
CCM na Amani:

Tukiruhusu vyama vingi itatokea fujo.
Mkichagua upinzani itatokea machafuko.
Na Sasa Serikali tatu italeta machafuko.

Hivi CCM wamekosa kabisa Sera zaidi ya hiii ya Amani na Mshikamano ambao tayari haupo?
 
Mods kwa nini mmetoa uzi huu wakati umzingatia itifaki zote za jf? Halafu haieleweki mmeunganisha na uzi gani! Naomba mrudishe tafadhali, tunajadili mustakabali wa taifa letu.
 
Mh Kinana hajui hata maana ya Muungano unaotakiwa na watanzania wa leo. Yeye anafikiri ni wa mke na mume kama ule wa awali? Maana katika muungano mwaka 1964, Tanganyika ilipoteza uasili wake. Ni kama iliolewa na Zanzibar, maana Zanzibar ilibaki na serikali yake. Kama tunafikiria Muungano wa "Federation" hakuna nchi inayopaswa kupoteza uasili wake. Wakati Tanganyika inaungana na Zanzibar maono ya watu wake yalikuwa duni ukilinganisha na watanzania wa wakati huu. Sasa hii hofu ya CCM na viongozi wake inatoka wapi wakati wananchi wana upeo mkubwa wa kuelewa ukilinganisha na mwaka 1964? Hata jina la serikali ya Muungano liliyotajwa kwenye "Articles of Union"ya wakati ule ilitaja kabisa jina litakuwa "The united Republic of Tanganyika and Zanzibar." Jina laTANZANIA liliasisiwa baadaye kuondoa mlolongo wa kutamka majina ya nchi mbili. Kwa sababu za uandishi wa historia kupotoshwa makusudi na watawala wetu, ni watu wachache sana wanaofahamu, au kukumbuka mambo yalivyokuwa. Hawa viongozi wote wa CCM walio madarakani ni wale waliolishwa historia iliyopotoshwa, ndio maana wanahubiri hofu walizonazo. MH. KINANA NA VIONGOZI WA CCM WAACHIE WATANZANIA WAPATE FURSA YA KUTENGENEZA NCHI WANAYOTAKA BILA YA KUTIWA HOFU. Hata hivyo katiba sii BIBLIA wala QURAN ambazo yaliyoandikwa yalishaandikwa!! Ni kitu kinachojadilika na kurekebishwa muda wowote inapohitajika. Wamarekani pamoja na kuwa makini na katiba yao, wameshaifanyia marekebisho mara 27!! SISI NI KWA NINI TUIONE KATIBA KAMA KITU KITEULE KISICHOWEZA KUBADILISHWA HAJA INAPOKUWEPO? WANANCHI TUAMKE TUSILEMAZWE NA HAWA WANAOTAKA KUTUTAWALA KIFIKRA.
 
Kinana hana hoja.

ccm ndio inayoingilia mchakato wa katiba mpya.
Na ndio itakayoleta vurugu nchini.maana ni mambo mazuri yaliyoandikwa kwenye rasmu ya awali ndio maoni ya watanzania na yeyote anayeyapinga huyo sio mtanzania bali ni msaliti na mroho wa madaraka.

cha msingi ni kuiboresha hiyo rasimu na ccm kujiandaa kisaikolojia kuongozwa na serikali ya cdm bara na zanzibar cuf.

hofu ya ccm sio serikali 3 wala gharama za uedeshaji maana kama ni gharama wasingeongeza mikoa ,wilaya n.k bali hofu yao ni zanzibar kuongozwa na cuf.

tayari tuna marais kibao,kuna rais wa TFF,n.k
Hoja rais wa nchi atakuwa mmoja wengine watakuwa mawaziri wakuu.
 
* Asema Tanzania itashangaza dunia

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeendeleza msimamo wake wa kupinga muundo wa Serikali tatu kuingizwa katika Katiba mpya, kikisema kuwa muundo huo ni hatari kwa umoja na mshikamano wa taifa.

Chama hicho kimeonya kuhusu muundo huo na kusema kuwa Serikali zaidi ya mbili zinaweza kuvuruga ustawi wa taifa, kwani ni rahisi zaidi nchi kuingia katika machafuko.

Tamko hilo lilitolewa jana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi katika Wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Kinana alisema muundo wa Serikali tatu ni mzigo kwa taifa na kwamba Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kuwa na marais watatu, jambo ambalo halipo duniani kote.

“Katiba ni jambo muhimu kwa ustawi wa nchi yetu, lakini katika hili la kuwa na Serikali tatu ni hatari, kwani kwa mujibu wa rasimu yetu ya sasa, inaonyesha kuwa kila Serikali itakuwa na mamlaka kamili.

“Ikiwa kutatokea serikali moja kati ya hizo tatu na moja ikasema sasa inanunua vifaa vya kujilinda, basi ile ya Zanzibar nayo itafanya hivyo na ile ya Muungano pia itafanya hivyo.

“Hata kama kuna vita serikali moja ikasema hatutaki nyingine itasema tunataka, mwishowe mtaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe,” alisema Kinana na kuendelea:

“Kwa hali hiyo, ninachotaka kuwaambia ni kuwa Katiba Mpya itaandikwa na maisha yale yale yataendelea. Afrika Kusini, India na Kenya wamebadili katiba zao, lakini hali ya maisha ya wananchi wao iko vilevile,” alisema.

Katika mkutano huo, Kinana alisema msimamo wa chama chake kuhusu muundo ni Serikali mbili na kueleza kuwa chama chake kitaheshimu maoni ya Watanzania kuhusu muundo wowote bila shinikizo la kisiasa.

Alisema hatua ya kuwa na wingi wa Serikali kuna hatari ya nchi kuwa na Bunge la Mabwenyenye na Bunge la Makabwela, ambapo alisema kuna hatari ya fedha za walipa kodi kutumika vibaya.

Kinana alionya hatua ya kuwa na ukubwa wa Serikali ambayo itakuwa mzigo kwa Watanzania, ambao wamekuwa wakiendesha kwa kulipa kodi zao.

“Hivi sasa nchi ipo katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya, ninapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa CCM itakuwa tayari kupokea maamuzi yoyote yatakayoamuliwa na wananchi.

“…. Na ikiwa mtaamua kuwa ya Serikali mbili, tatu hata tano sawa, lakini kubwa katika hili CCM hatuhitaji mchakato huu ufanyike kwa kuingiliwa kwa shinikizo kutoka kwa vyama vya upinzani au hata taasisi ambazo zimejificha kwa mlango wa nyuma.

“Sisi tulisema wazi tunapenda tuendelee na Serikali mbili, lakini katika hili tambueni kuwa na Serikali nyingi zaidi kuna hatari ya kuingia katika mifarakano na hata vita,” alisema Kinana.

Katibu Mkuu huyo alisema kuwa hatua ya baadhi ya watu kupita na kupandikiza chuki kuhusu Katiba Mpya, mawazo yao yanatakiwa kupimwa, kwani watu hao wana lengo la kuvunja badala ya kuimarisha umoja.

“Ni muhimu kuandika Katiba mpya ambayo itasaidia kuweka misingi bora na imara ya uongozi, lakini si kuwa na Katiba yenye utitiri wa kila aina ya Serikali, hili hapana, ila ikiwa mtaamua nyie wananchi wenyewe sisi hatuna pingamizi,” alisema.

Mapema Agosti mwaka huu, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, aliwataka wanachama wa CCM kujiandaa kisaikolojia na muundo wa Serikali tatu, ikiwa Watanzania wataamua hivyo.

Rais Kikwete alinukuliwa na vyombo vya habari kupitia vikao vya NEC mjini Dodoma, ambapo alisema mwaka 1992, kundi kubwa la wananchi lilipinga kuingia katika mfumo wa vyama vingi, lakini lilisikilizwa na nchi ikaingia kwenye mfumo huo.


Source: Gazeti Mtanzania la leo.

Je kuna ukweli gani katika kauli hii ya Kinana ambayo pia ndio msimamo wa CCM?
.ENYI WANACCM Mnaoamini kuwa serikali tatu ni kuvunja muungano ningewaelewa sana mngekuja na wazo la kuwa na serikali moja ya Tanzania, kama Tanganika ilipoungana na Zanzibar ikazaliwa Tanzania ,why Zanzibar ilibaki mpaka leo?...Wakti mwingine nafikiri ILIKUWA NI KUBADILI JINA LA NCHI NA KUISAIDIA zanziba kiuchumi.
 
Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya filauni.Muungano wa nchi mbili umetusumbua kwa muda mrefu na tumekaa vikao vingi sana tukisema tunatatua kero ndogondogo za Muungano ambazo mpaka leo zimeshindwa kutatulika.Kwa akili ya kawaida isiyohitaji elimu ya juu embu tujiulize mambo yafuatayo: 1) Ikiwa leo hii katika hali ya muungano tulionao tukasambaratika na kugawanyika,mustakabali wa nchi yetu upo vipi?.2)Vijana wengi walio na umri chini ya miaka 35 wengi hawahitaji aina hii ya muungano,si kwa Zanzibar wala Tanzania bara,je tunatengeneza mazingira yapi ya baadae kwa kizazi hicho.Tuache ushabiki wa kisiasa na tuangalie mustakabali wa nchi yetu.Gharama za Serikali ya tatu zitachangiwa na nchi zote mbili na kila nchi itatambua rasilimali ilizo nazo na namna ya kendesha nchi bila ya kuingiliwa na upande mwingine.Wakati umefika wa kufikiria nje ya box.
 
Propaganda ndivyo ilivyo. Zua jambo, lipambe lipambike, watu watakuamini tu. Kinana anasema Serekali 3 zitauvunja muungano, ati serekali moja ikiamua kwenda vitani nyingine inaweza kukataa. Saa hii tunavyo danganywa na Kinana, kule Zenji, wao wana bunge lao, bajeti yao, Rais wao, Bendera yao, wimbo wao wa Taifa. Hao Kinana anadhani akitaka kwenda vitani tayari watafuatana naye. Pole Kinana, yeye mwenyewe akitaka kwenda Zenji lazima aonyeshe pass ya kuingia Zenji, sasa huo ndo Muungano??? Ama kweli, Zidumu fikra sahihi za M/Kiti wa CCM.
Kuwe na serekali 10 au ishirini, Muungano wako Kinana upo kwenye mushkeli mpaka sasa. Tupe serekali 3, tujadili aina ya muungano. Nasema; "TUUJADILI" Yaani "Shirikisho". BAAAAAASI. Vingine, muungano utakufia mkononi Kinana.
Tanganyika ni lazima. Kama unautaka muungano uwepo siku mbili tatu hivi.
Ati serekali 3 zitaleta machafuko; kakuambia nani? Kwani hizo serekali 3 zitaundwa na watu kutoka sayari nyingine au ni sisi! Kama umekosa cha kupingia kubali yaishe. Ukikubali haitakuwa aibu ati kwa sababu Dr. Slaa amekubali. CCM kazi yao ni kupinga kila kitu ambacho upinzani umekisema.
 
Kinana sisi hatuna tabu na ww sisi shida yetu ni Tanganyika yetu sasa kama mtaifuta zanzibar then Tanganyika ndo ibaki nchi xawa 2.
 
Mbona hawaongelei Serikali moja, endapo tatu ni mzigo?
 
Serikali tatu si kwa ajili ya Chadema au CUF au NCCR. Si kwa ajili ya Wahaya, wanyakyusa , wachaga,wasukumuma,wazaramo, wasambau n.k . Ni kwa ajili ya Watanzania wote na ni maoni kutoka kwa Watanzania walio wengi sasa huyu katibu asituleetee maoni yake! Tanganyika kwanza Vyama vyetu baadaye.
 
Maccm yanajua yakiruhusu Tanganyika itakuwa ngumu kuiba kura kwenye sanduku la rais wa muungano, Tanganyika na Zanzibar wakati uchaguzi,
 
Back
Top Bottom