Kwa nini viongozi wa dini wasiwakutanishe Ruto na Odinga kwa ajili ya mazungumzo? Inaonekana wote, Ruto na Odinga, wanawaheshimu sana viongozi wa dini. Wangewakutanisha ili wamalize tofauti zao. Kutokuelewana kwao kunawaumiza wasio na hatia.
Maisha ni malezi.Kenya asili yao ni UJIVUNI.Hivyo kufananisha maisha ya Kenya na Tanzania ni vitu viwili tofauti.Sisi Tanzania tuna Baba,Baba mkubwa,Baba mdogo,Mama,Mama mkubwa,Mama mdogo,Shangazi wa kweli na Wajomba wa kweli lakini Kenya hawana Baba mkubwa au Baba mdogo,pia hawana Mama mkubwa au Mama mdogo ni kila mtu na baba yake na mama yake.Kama baba na mama wakishindwa kudhibiti nidhamu ya watoto inakuwa imekula kwao na jamii inayowazunguka kwa sababu ya upunguani wa fikra kusahau asili ya Mwafrika na kuiga mila desturi za Wazungu.
Unapoona Watanzania wengi wanapinga Mkataba wa DP World siyo kwamba hawana akili bali wanalinda kizazi chao walichobarikiwa na Mungu.Pamoja kwamba ni uwekezaji wenye manufaa makubwa kwa Taifa hili lakini bado kutakuwa na hasara ya milele kama ilivyo Kenya.Hakuna Mtanzania aliyezoea fujo za mara kwa mara,hakuna Mtanzania anapenda kuwa mtumwa kwa sababu ya mali,hakuna Mtanzania anapenda kuwa mtumwa kwa sababu ya Uwekezaji.Kila kitu Mungu ametupa kama vile Ardhi,Watu,Milima,Bahari,Maziwa,Mito,Mabonde,Misitu,Wanyama,Akili,Elimu,Vyuo mbalimbali,Vyama vya siasa kwa nini tushindwe kujiongoza mpaka tumtegemee tajiri DP World kuja kuinua maisha yetu?