Obamaeli Rutajecha
JF-Expert Member
- Jan 7, 2016
- 230
- 274
Habari za kunyapianyapia kutoka katika viunga vya mitaa ya kariakoo zinasema msanii huyo anayeamini kuwa yeye ndio bora yupo mbioni kuachia collabo lake na msanii huyo wa kutoka huko duniani.
Mfalme huyo wa wauza mbogamboga na mitumba wa K/koo inadaiwa kwamba ameshtushwa sana na tukio alilolifanya Mnyama mmoja asiye na chembe ya huruma kutoka huko Madale lililomnyong'onyeza na kumfanya kufura mithili ya Nyumbu aliyempoteza mwanae.
Hadi muda huu inasemekana kwamba, mfalme huyo wa makuli wa K/koo aliyejawa na nyodo na majigambo amemtishia Rihanna akidai kutaka kutoa part aliyoimba msanii huyo kutoka huko ughaibuni.
Nitaendelea kuwajuza kinachoendelea hapa ufalmeni K/koo