kukomya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2011
- 344
- 144
Ni Waswaziland wale si watanzania. Tuna tamaduni tofauti na hii si ajabu maana kila taifa na kabila lina utamaduni unaolitambulisha dhidi ya mataifa/makabila mengine. Inawezekana baadhi ya mambo katika tamaduni fulani yakawa kero kwenu kama mambo ya kwenu yalivyo kero kwao maana sumu inayoweza kukuua wewe inaweza kuwa dawa muhimu kwa mwingine. Si vema kuukosoa utamaduni wa wengine usiotuhusu ili mradi wao pia hawaukosoi wenu.KUmbe binti yake kweli!!!! Do lakini kifua wazi mbele ya baba! Wakaka wa JF mpa hapo?
Yaelekea wachangiaji wengi humu wana inda na jinsi Mfalme "anavyofaidi" totos, nasema ni wivu tu maana pengine nafasi hiyo wangeipata wao ingekuwa kiama! Anyway, zile zilikuwa sherehe za kifalme zinazomjumuisha Binti yake; kwa waswazi hazina ubaya wowote na ukipenda na wewe nenda kaigize kwenu uwe kioja na ukamalizie maisha yako na Baba Seya. Maana wabongo kwa kuiga bwana... wee acha tu.