Elections 2015 King of De Docta Ignorantia: Hatuwezi kumpa FISI ulinzi wa BUCHA

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
2,009
Reaction score
1,607
Zipo juhudi kubwa za kuwapumbaza watanzania kwa kile kinachoitwa kuwaelewesha ili kufanya Informed Decision kwa kumchagua LOWASSA wa Ukawa dhidi ya MAGUFULI wa CCM..juhudi hizi zilizoimarika hivi karibuni zinatumia waandishi wa habari wa vyombo maalum na wale wa kujitegemea, lakini nguvu hiyo imesambaa zaidi mpaka kwenye mitandao ya kijamii..nguvu ya wanamabadiliko waliobadilika.

Juzi niliandika nikimjibu PASCO wa JF kuhusu kile alichokiita Ujinga wa watanzania kwa kuichagua CCM, akiwa anawaelekeza watanzania kuamini na kumchagua EDWARD LOWASSA eti kwa madai yake HUYU NDIO MUSSA ATAKAYETUVUSHA BAHARI YA SHAMU..lakini hakuishia hapo amejitokeza tena kuendelea na msimamo wake ila kwa bahati mbaya ameacha maswali na hoja muhimu katika majibu yangu na kuhamia katika hoja zingine ambazo majibu yake ni Rahisi...maana amehamia kwenye hoja ya RUSHWA ambae huyo anayemnadi kuitokomeza RUSHWA hawezi hata kuizungumza kwenye majukwa yake ya kisiasa na anaamrisha wengine pia wasiizungumze..AJABU SANA.

I don't believe on mistakes, hivyo siamini kuwa makosa katika nukuu ya PASCO yalikuwa ni BAHATI MBAYA...binafsi najua ni muendelezo wa De Docta Ignorantia, on learned ignorance ambayo PASCO ni mfalme akitaka tumchagua FISI akatulindie BUCHA kwa kigezo kuwa MLINZI wetu wa sasa anasinzia sinzia....Noooooo NEVER..!!

Nitajinukuu;

Nimesoma andiko la PASCO wa JF kuhusu kile anachodai ni UJINGA wa watanzania, kwa kuendelea kuichagua CCM ambayo kwa mawazo ya PASCO ni chama kibaya.

1. Naomba kumthibitishia kuwa MIMI na watanzania sio wajinga, tunatambua jema na ovu, tunatambua nani ni mbaya na nani ni mwema..yawezekana yeye ameshindwa kutambua, hivyo siwezi kuzungumzia ujinga wake ila nitazungumzia juu yangu na Watanzania wenzangu ambao kwa Miaka zaidi ya 50 sasa tumeendelea kuiamini CCM.

Tanzania is exceptional country with extra ordinary countrymen..TUNGEKUWA wajinga tungekubali nchi yetu KUTOTAWALIKA..nchi hii ni ya mfano katika nchi za Afrika, mfano kwa UONGOZI imara, mfano kwa AMANI na UTULIVU, mfano kwa UMOJA wa KITAIFA, mfano kwa kujitoa katika kusaidia nchi nyingine za Afrika kwa hali na mali, hakuna Nchi yeyote katika Afrika kusini mwa jangwa la sahara ambayo imepiga hatua na kufikia ilipofikia leo ikawa HAIJAPATA msaada wa TANZANIA,
kama ipo naomba niambiwe.

Hivyo mimi binafsi napingana kabisa na WAZO kuwa CCM haijafanya chochote katika ujenzi wa ustawi wa jamii ya Watanzania na Afrika kwa ujumla..Marais wa Tanzania kutoka BABA wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mpaka Jakaya Mrisho Kikwete wameendelea kuwa ICON sio tu kwa Tanzania bali kwa DUNIA nzima katika suala zima la Utawala na uongozi uliotukuka,
hata leo tuzo mbalimbali za Kimataifa zimeendelea kuelekezwa Tanzania kwa heshima ya utendaji wa kazi zao...ni UJINGA na MJINGA tu ambae anaweza kupaza sauti bila aibu kusema kuwa WATANZANIA ni wajinga...na inatia shaka zaidi pale inapotokea mtu huyo akiwa MTANZANIA.

Na kama ni kile ninachokiona ni MAHABA kwa Upinzani wa nchi hii, niseme tena mimi nimewahi kuwa Mpinzani wa CCM kwa muda mrefu, its no better kwenye upinzani kuliko hata kwa CCM..
Hauwezi kulizungumza suala la UONGOZI BORA kwa upinzani..hauwezi kuzungumzia Suala la kukuza ELIMU kwa wapinzani, hauwezi kuliongelea suala la kukomesha Rushwa kwa Wapinzani wa nchi hii...hauwezi kuwaamini kwa lolote wapinzani wa nchi hii..Ni watu wasiojitambua, wasiojielewa, wasio na misimamo, wanaoyumba na baya zaidi WASIOFIKIRI.

CCM imeendelea kuwa CHAMA kinachojitathimini na kinachojiimarisha siku hadi siku, sipingi wala sisemi kuwa CCM haijawahi kukosea, haina makosa na haijaaribu katika utawala wake..hapana na nikisema hivyo nitakuwa mnafiki, lakini tunaiona CCM ikijivua gamba katika new style, ikikataa kuwakumbatia mafisadi na kwa mara ya nyingine tena ikipata mgombea BILA RUSHWA, BILA HILA na BILA MTANDAO...hivyo kama PASCO unaamini kuwa CCM ni ile ile, yenye watu wale wale na sera zile zile basi PASCO wewe sio PASCO yule ninayemjua ambae huwa anaandika baada ya kufikiria, it seems contrary to my experience., perhaps U have personally and intentionally decides to do wrong and u seemed to know full well of ur decision.

Najua unataka tuamini katika UPINZANI basi tusaidie watanzania sisi ambao wewe (mwerevu) unadhani tu wajinga kupindukia, sababu 3 tu za kuamini katika Upinzani..jaribu kutushawishi, kutuita wajinga pekee hakusaidii..tupe HOJA kuwa CCM imechoka na hivyo UPO UPINZANI MBADALA wa kutuvusha baada ya kuiweka CCM pembeni...Mind U nilikuwa MPINZANI, yawezekana kabisa najua hata yale USIYOYAJUA.

Ndio tarehe 25th October 2015, tutaichagua tena CCM, tena kwa kishindo KIKUU, lakini kamwe hatuchagui kwa UJINGA..,tunazo akili, tunajua BAYA na ZURI kwetu, na hivyo..TUMEKUSIKIA, TUMETAFAKARI na TUMESHAAMUA kuwa MAGUFULI ndio Rais wetu wa AWAMU ya TANO..

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI CCM.

Kwenye RED ni maeneo ambayo nimeonyesha strength ya CCM ambayo PASCO kakimbia kuyajadili kwa hoja, kuwa CCM imeamua kujijenga UPYA na kufukuza manyang'au wote waliokuwa wanaharibu IMAGE ya Chama, manyang'au hayo yamenunua chaka jipya na wanalipa watu wawasafishe kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii...na bahati mbaya wamejitokeza watu waliojitoa ufahamu na kukubali kutumika..na hakika HAKUNA DENI BAYA KAMA DENI LA TUMBO linawatesa wengi katika watu hata wale wenye elimu zao.

Kwenye KIJANI ni maswali ambayo PASCO kwa maksudi ameyakimbia, HASEMI lolote kuhusu UPINZANI, hasemi kuhusu THE DON na makando kando yake...anasema tu kuwa anachukia RUSHWA lakini hasemi DON LOWASSA amejiandaaje kupambana na Rushwa hata awe bora kuliko MAGUFULI wa CCM..

1. LOWASSA wa CHADEMA na UKAWA ni kielelezo cha ubovu, uchafu na uovu uliokuwa unasababisha harufu mbaya ndani ya CCM kwa zaidi ya miaka 30 aliyokuwa anatumikia Serikali kupitia chama hicho. He re

2. LOWASSA hawezi kuwa Kiongozi wa Mabadiliko (hayo ambayo PASCO) anawaaminisha Watanzania, kwani alikuwa katika mfumo huo kwa zaidi ya miaka 30 na hakubadilisha chochote, leo LOWASSA amebadilika nini..?

3. LOWASSA ni MWIZI, NI MLA RUSHWA MKUBWA na nimeandika haya nikitumia ID yangu kamili, na nitasema haya popote pale..na kwa fedha zake za wizi amekuwa akinunua watu wa kumsafisha kila uchao, nina mashaka ndugu yangu PASCO is on the list.

4. LOWASSA anasimama na mwenzie SUMAYE kukosoa Serikali ambayo maamuzi makubwa yaliyoangamiza TAIFA walishirikia kuyapitisha kama sio KUYASIMAMIA ili yapitishwe na Serikali..leo wamekuwa wasafi ghafla kwa kuwa wamehamia UPINZANI..kama sio UJUHA ni nini..?

5. LOWASSA ameishi, ametenda na ameendelea kutetea IMANI kuwa pesa ndio kila kitu, imani ambayo PASCO and the TEAM MABADILIKO imeendelea kuamini, hawezi kuishi nje ya IMANI hiyo ambayo inapingana na IMANI ya UADILIFU...na tunachotaka watanzania ni MTU MUADILIFU ili akanyooshe mambo yaliyopinda ndani ya Serikali..

5. HAKUNA ushahidi ama rekodi yeyote ambayo inaonyesha LOWASSA amebadilika, bali upo USHAHIDI na REKODI ambazo zinathibitisha kuwa LOWASSA ni MWIZI, MLA RUSHWA, MUONGO na FISADI PAPA..hana moral authority ya kukemea Rushwa.

PASCO..,narudia tena kuwa WATANZANIA sio WAJINGA: tumekusikia, tumetafakari na tumeamua MAGUFULI ndio ajaye. Hatuko tayari kumpa FISI ulinzi wa BUCHA.

VIDEO: KINANA na CCM MPYA

https://youtu.be/bSG2TBeCS_A

Hakunawa mwanasiasa ambaye si mwizi. CCM miaka Yao ya kutawala inatosha. Hawana jipya isipokuwa hadaa na uongo. Ni aibu kuzungumza Maji Leo na Umeme. Inatosha
 
Nani kauza nyumba za serikali kwa wake zake?

Hasara kubwa fidia samaki wa magufuli?

Mafisadi Chenge,Ngeleja,Tibaijuka ni vyoo vya ccm vyenye harufu kali waliopitishwa kuwania ubunge.

Ccm imehusika na ESCROW.

Lowassa taka usitake ndio chaguo letu walala hoi.

Ikulu siyo ya mzee wako utunyime.
 
juliana shonza acha ubinafsi ccm ikiingiamadarakani mtanufaika kikundi cha watu wachache na matajiri voda fasta watazaliwa acha zamu hii tuchague mabadiliko dhidi ya ukale chama chenu kitaendelea kua cha upinzani vilevile huku safari hii kikitumika na chadema dhidi ya ccm
 
Tumesoma na tumeelewa
Ila Mzee kaishatuingia kwenye mioyo yan katikati ya moyo hakuna namna tutampa Nchi tu
 
CCM ndio MAFISI na wezi wakubwa... tena wakubwa sana,

Ona hapa chini hadi wako na FISI na huyo Kinana, kamaliza tembo wetu...!!!
 
Zipo juhudi kubwa za kuwapumbaza watanzania kwa kile kinachoitwa kuwaelewesha ili kufanya Informed Decision kwa kumchagua LOWASSA wa Ukawa dhidi ya MAGUFULI wa CCM..juhudi hizi zilizoimarika hivi karibuni zinatumia waandishi wa habari wa vyombo maalum na wale wa kujitegemea, lakini nguvu hiyo imesambaa zaidi mpaka kwenye mitandao ya kijamii..nguvu ya wanamabadiliko waliobadilika.

Juzi niliandika nikimjibu PASCO wa JF kuhusu kile alichokiita Ujinga wa watanzania kwa kuichagua CCM, akiwa anawaelekeza watanzania kuamini na kumchagua EDWARD LOWASSA eti kwa madai yake HUYU NDIO MUSSA ATAKAYETUVUSHA BAHARI YA SHAMU..lakini hakuishia hapo amejitokeza tena kuendelea na msimamo wake ila kwa bahati mbaya ameacha maswali na hoja muhimu katika majibu yangu na kuhamia katika hoja zingine ambazo majibu yake ni Rahisi...maana amehamia kwenye hoja ya RUSHWA ambae huyo anayemnadi kuitokomeza RUSHWA hawezi hata kuizungumza kwenye majukwa yake ya kisiasa na anaamrisha wengine pia wasiizungumze..AJABU SANA.

I don't believe on mistakes, hivyo siamini kuwa makosa katika nukuu ya PASCO yalikuwa ni BAHATI MBAYA...binafsi najua ni muendelezo wa De Docta Ignorantia, on learned ignorance ambayo PASCO ni mfalme akitaka tumchagua FISI akatulindie BUCHA kwa kigezo kuwa MLINZI wetu wa sasa anasinzia sinzia....Noooooo NEVER..!!

Nitajinukuu;

Kwenye RED ni maeneo ambayo nimeonyesha strength ya CCM ambayo PASCO kakimbia kuyajadili kwa hoja, kuwa CCM imeamua kujijenga UPYA na kufukuza manyang'au wote waliokuwa wanaharibu IMAGE ya Chama, manyang'au hayo yamenunua chaka jipya na wanalipa watu wawasafishe kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii...na bahati mbaya wamejitokeza watu waliojitoa ufahamu na kukubali kutumika..na hakika HAKUNA DENI BAYA KAMA DENI LA TUMBO linawatesa wengi katika watu hata wale wenye elimu zao.

Kwenye KIJANI ni maswali ambayo PASCO kwa maksudi ameyakimbia, HASEMI lolote kuhusu UPINZANI, hasemi kuhusu THE DON na makando kando yake...anasema tu kuwa anachukia RUSHWA lakini hasemi DON LOWASSA amejiandaaje kupambana na Rushwa hata awe bora kuliko MAGUFULI wa CCM..

1. LOWASSA wa CHADEMA na UKAWA ni kielelezo cha ubovu, uchafu na uovu uliokuwa unasababisha harufu mbaya ndani ya CCM kwa zaidi ya miaka 30 aliyokuwa anatumikia Serikali kupitia chama hicho. He re

2. LOWASSA hawezi kuwa Kiongozi wa Mabadiliko (hayo ambayo PASCO) anawaaminisha Watanzania, kwani alikuwa katika mfumo huo kwa zaidi ya miaka 30 na hakubadilisha chochote, leo LOWASSA amebadilika nini..?

3. LOWASSA ni MWIZI, NI MLA RUSHWA MKUBWA na nimeandika haya nikitumia ID yangu kamili, na nitasema haya popote pale..na kwa fedha zake za wizi amekuwa akinunua watu wa kumsafisha kila uchao, nina mashaka ndugu yangu PASCO is on the list.

4. LOWASSA anasimama na mwenzie SUMAYE kukosoa Serikali ambayo maamuzi makubwa yaliyoangamiza TAIFA walishirikia kuyapitisha kama sio KUYASIMAMIA ili yapitishwe na Serikali..leo wamekuwa wasafi ghafla kwa kuwa wamehamia UPINZANI..kama sio UJUHA ni nini..?

5. LOWASSA ameishi, ametenda na ameendelea kutetea IMANI kuwa pesa ndio kila kitu, imani ambayo PASCO and the TEAM MABADILIKO imeendelea kuamini, hawezi kuishi nje ya IMANI hiyo ambayo inapingana na IMANI ya UADILIFU...na tunachotaka watanzania ni MTU MUADILIFU ili akanyooshe mambo yaliyopinda ndani ya Serikali..

5. HAKUNA ushahidi ama rekodi yeyote ambayo inaonyesha LOWASSA amebadilika, bali upo USHAHIDI na REKODI ambazo zinathibitisha kuwa LOWASSA ni MWIZI, MLA RUSHWA, MUONGO na FISADI PAPA..hana moral authority ya kukemea Rushwa.

PASCO..,narudia tena kuwa WATANZANIA sio WAJINGA: tumekusikia, tumetafakari na tumeamua MAGUFULI ndio ajaye. Hatuko tayari kumpa FISI ulinzi wa BUCHA.

VIDEO: KINANA na CCM MPYA

https://youtu.be/bSG2TBeCS_A

Jully Ndoa lin? Tuliona Pete tu na mida inakwenda. Angalia dada usisindikize siasa kutafuta shibe ya watoto wa vigogo ukaikosa ndoa yako takatifu
 
Juliana Shonza

Haupo tayari kumwachia fisi ulinzi wa bucha, lakini upo tayari kumfanya fisi kuwa mchungaji wa huo mfugo unaliochinjwa na kuletwa buchani, upo tayari kumafanya fisi kuwa mchinjaji wa huo huo mfugo na vile vile upo tayari kumpa fisi kuwa muuza bucha.... Hatariii ya ndorobo....

Do you see chances mnazompa huyo mchungaji-fisi, mchinjaji-fisi na muuzaji-fisi..?? Kumbuka mlinzi-fisi, bucha linakuwa limefungwa na chances za kuibwa ni ndogo sana.

Juliana Shonza

Ahadi anazotoa Magufuli ni kwa namna nyingine kumpiga vijembe JK. Haiwezekani eti nimpe kura Magufuli, simply kashangaa hakuna kiwanza cha samaki Tanga hadi Mtwara, ANAMSHANGAA NANI..?? CCM, WANANCHI AU JK..?? Anashangaa habari ya dawa kukosekana hospitali, anashangaa watoto kukaa chini... HIVI ANAMSHANGAA NANI..??? Swezi ishi kwa ahadi.. Tena nyingine zimeshindikana kuzitekeleza miaka michache iliyopita..
1. Ahadi ya GRIDI ya TAIFA Songea, Kigoma na Kagera... Hakuna hata anayechakata
2. Meli ziwa victoria hakuna...
3. Ahadi ya viwanja vya ndege hakuna...

Siwezi kumchagua kwa ahadi anazotoa, ambazo nyingine mlitakiwa muwe mmeshazitekeleza ndani ya miaka 50 iliyopita....
 
Hoja zako ni nzito kichwani kwako mwenyewe,ila kwenye mizani ni nyepesi mno,na upande mwingine zinakuacha uchi kabisa!! Kwanza naomba nikutambue kama mpizani muasi uliyejiunga na ccm chafu huku ikiwa bado ni chafu!! Ningekuelewa walau kama ungerudi ccm kipindi hiki ambapo wale tuliowaita wachafu wameondoka huko(si kuondolewa)sasa leo unasimama kumtukana lowassa ambaye ulimfuata ccm na akakukimbia na kukuacha huko??absurd!! Pili nikuulize tu je chadema unayoichukia ni hii yenye lowassa na sumaye au ni ile ya slaa na zitto?maana uliikimbia ya slaa na unaitukana ya lowassa,unafiki ni kuichukia ukawa ya lowassa na kuipenda ccm ya chenge,
 
Juliana Shonza

Haupo tayari kumwachia fisi ulinzi wa bucha, lakini upo tayari kumfanya fisi kuwa mchungaji wa huo mfugo unaliochinjwa na kuletwa buchani, upo tayari kumafanya fisi kuwa mchinjaji wa huo huo mfugo na vile vile upo tayari kumpa fisi kuwa muuza bucha.... Hatariii ya ndorobo....

Do you see chances mnazompa huyo mchungaji-fisi, mchinjaji-fisi na muuzaji-fisi..?? Kumbuka mlinzi-fisi, bucha linakuwa limefungwa na chances za kuibwa ni ndogo sana.

Juliana Shonza

Ahadi anazotoa Magufuli ni kwa namna nyingine kumpiga vijembe JK. Haiwezekani eti nimpe kura Magufuli, simply kashangaa hakuna kiwanza cha samaki Tanga hadi Mtwara, ANAMSHANGAA NANI..?? CCM, WANANCHI AU JK..?? Anashangaa habari ya dawa kukosekana hospitali, anashangaa watoto kukaa chini... HIVI ANAMSHANGAA NANI..??? Swezi ishi kwa ahadi.. Tena nyingine zimeshindikana kuzitekeleza miaka michache iliyopita..
1. Ahadi ya GRIDI ya TAIFA Songea, Kigoma na Kagera... Hakuna hata anayechakata
2. Meli ziwa victoria hakuna...
3. Ahadi ya viwanja vya ndege hakuna...

Siwezi kumchagua kwa ahadi anazotoa, ambazo nyingine mlitakiwa muwe mmeshazitekeleza ndani ya miaka 50 iliyopita....

anashangaa utadhani alikua haiishi tanzania.
 
Kura yangu nitampa Magufuli. Lakini sioni vibaya UKAWA wakishinda kwa Urais,huku tukigawana viti vya ubunge na udiwani. Sifa kuu ya kuwa mgombea ni kuwa MTANZANIA. Tanzania ni yetu wote.
 
Maneno mengi...!!!! ?CCM Wananchi wameshaochoka?....Ahadi za uongo kila leo....Its over kwa CCM....
 
Mafisi yashatulindia sana bucha letu....heri kumkabidhi bucha fisi mmoja kuliko kukabidhi kwa mamia ya mafisi......KURA YANGU KWA FISI MMOJA...........
 
Moyoni mwako ni dhahiri unajua unachotetea si sawa.... Mabadiliko ni lazima mwaka huu tumeamua kuchagua fisi mmoja tutajua jinsi ya kumtazama asile nyama buchani kuliko kuchagua mchungaji wa mafisi 300 atulindie bucha letu..... Mafisi yakipata njaa yatamla kuanzia mchungaji mpaka bucha zima....
MABADILIKO NJE YA CCM NI LAZIMA....
 
attachment.php

647800644.JPG

attachment.php

attachment.php
 
Attachments

  • Raia Mwema - Ni Wizara ya Mifugo na Uvuvi au Uvivu-.jpg
    Raia Mwema - Ni Wizara ya Mifugo na Uvuvi au Uvivu-.jpg
    59.2 KB · Views: 276
  • Raia Mwema - Ni Wizara ya Mifugo na Uvuvi au Uvivu- (1).jpg
    Raia Mwema - Ni Wizara ya Mifugo na Uvuvi au Uvivu- (1).jpg
    68.5 KB · Views: 280
  • Raia Mwema - Ni Wizara ya Mifugo na Uvuvi au Uvivu- (2).jpg
    Raia Mwema - Ni Wizara ya Mifugo na Uvuvi au Uvivu- (2).jpg
    77.9 KB · Views: 274
Ivi shonza ufisadi wa nchi hi ni richmond tu?vp kuhusu ripot ya prof asad ya uuzaji wa nyumba za serikali.funga mdomo.
 
Zipo juhudi kubwa za kuwapumbaza watanzania kwa kile kinachoitwa kuwaelewesha ili kufanya Informed Decision kwa kumchagua LOWASSA wa Ukawa dhidi ya MAGUFULI wa CCM..juhudi hizi zilizoimarika hivi karibuni zinatumia waandishi wa habari wa vyombo maalum na wale wa kujitegemea, lakini nguvu hiyo imesambaa zaidi mpaka kwenye mitandao ya kijamii..nguvu ya wanamabadiliko waliobadilika.

Juzi niliandika nikimjibu PASCO wa JF kuhusu kile alichokiita Ujinga wa watanzania kwa kuichagua CCM, akiwa anawaelekeza watanzania kuamini na kumchagua EDWARD LOWASSA eti kwa madai yake HUYU NDIO MUSSA ATAKAYETUVUSHA BAHARI YA SHAMU..lakini hakuishia hapo amejitokeza tena kuendelea na msimamo wake ila kwa bahati mbaya ameacha maswali na hoja muhimu katika majibu yangu na kuhamia katika hoja zingine ambazo majibu yake ni Rahisi...maana amehamia kwenye hoja ya RUSHWA ambae huyo anayemnadi kuitokomeza RUSHWA hawezi hata kuizungumza kwenye majukwa yake ya kisiasa na anaamrisha wengine pia wasiizungumze..AJABU SANA.

Juliana were you prematurely:

ignorance.jpg
Meanwhile you have got to understand that:
143210_600.jpg
 
Mifisi inaendelea kula bucha hadi leo. Tusiichague tena Lowassa atosha
 
Hakunawa mwanasiasa ambaye si mwizi. CCM miaka Yao ya kutawala inatosha. Hawana jipya isipokuwa hadaa na uongo. Ni aibu kuzungumza Maji Leo na Umeme. Inatosha

Nkulikwa,
Nimepata fadhaa na andiko lako.
Hakika umepotoka na umepotoka haswaa.

Katika kumtetea Lowassa/Ukawa na tuhuma za rushwa/ufisadi unasema kirahisi tu kuwa hakuna mwanasiasa asiye kuwa mwizi kwa hiyo miaka ya ccm imekwisha. Waondoke.

Kwa hoja yako hii, kwa kuwa hakuna wanasiasa ambao sio wezi basi ni wakati wa sisi kuchagua wezi wengine wachukue nchi ili nao wapate zamu yao ya kutuibia.

Mawazo duni na potofu.
Kwa hiyo mabadiliko unayoyataka wewe ni ya kutoa mwizi mmoja na kuleta mwingine kwa sababu tu yule aliyekuwepo keshatuibia kwa miaka mingi.

Ni aibu sana.
 
Back
Top Bottom