Elections 2015 King of De Docta Ignorantia: Hatuwezi kumpa FISI ulinzi wa BUCHA

Elections 2015 King of De Docta Ignorantia: Hatuwezi kumpa FISI ulinzi wa BUCHA

Nani kauza nyumba za serikali kwa wake zake?

Hasara kubwa fidia samaki wa magufuli?

Mafisadi Chenge,Ngeleja,Tibaijuka ni vyoo vya ccm vyenye harufu kali waliopitishwa kuwania ubunge.

Ccm imehusika na ESCROW.

Lowassa taka usitake ndio chaguo letu walala hoi.

Ikulu siyo ya mzee wako utunyime.
Bavicha mna hoja nyepesi sana, hamnazo kabisa! Kila la kheri tarehe 25.10.2015, ila JPM ndo Rais wa JMT.
 
Hoja zako ni nzito kichwani kwako mwenyewe,ila kwenye mizani ni nyepesi mno,na upande mwingine zinakuacha uchi kabisa!! Kwanza naomba nikutambue kama mpizani muasi uliyejiunga na ccm chafu huku ikiwa bado ni chafu!! Ningekuelewa walau kama ungerudi ccm kipindi hiki ambapo wale tuliowaita wachafu wameondoka huko(si kuondolewa)sasa leo unasimama kumtukana lowassa ambaye ulimfuata ccm na akakukimbia na kukuacha huko??absurd!! Pili nikuulize tu je chadema unayoichukia ni hii yenye lowassa na sumaye au ni ile ya slaa na zitto?maana uliikimbia ya slaa na unaitukana ya lowassa,unafiki ni kuichukia ukawa ya lowassa na kuipenda ccm ya chenge,
Ngoja nikusaidie maana naona unahangaika na kutokwa povu katika jambo usilolijua...sikua na tatizo na Slaa wala Zitto, bali nilikuwa na tatizo na aina ya uongozi dhaifu ndani ya CHADEMA, nikaliweka bayana kwenye vikao kuwa umefika wakati Mwenyekiti atupishe, maana CHADEMA ilipofikia ilihitaji renewed vision na mission...na yeye aliendelea kuwa Muhafidhina akiifanya CHADEMA ni yake na familia yake..nililipinga hilo na sio jingine.

Ila kwenye kuzungumzia unafiki ukawalinganisha CHENGE na LOWASSA kisha ukasema CCM na UKAWA ni sawa kwa kuwa sehemu zote mbili kuna WEZI...ni irrelevant comparison..Who is CHENGE kwenye CCM...zaidi ya kuwa mgombea UBUNGE ana lipi jingine ambalo amefungamana na CCM kwalo, hana effect and easy to deal with..ila LOWASSA ndio kila kitu UKAWA, ndio Kauli mbiu, ndio Kiongozi Mkuu, ndio Mgombea Urais., ndio anayedictate nini kisemwe na nini kisisemwe (refer to list of shame)

Lowassa ndio kila kitu kwenye UKAWA...hana mfano wake.
 
Ule msemo wa chukua chako mapema unaanza kuwa kweli sasa. Wajiandae kukaa pembeni hawa ccm, siku zao zinahesabika. Hatuhitaji uongo mwingine toka kwao.
 
hahahaaaaaa... Kumbe copy paste ni syndrome

Nilijua ni ya John Pombe Ngoyai pekee yake mzee wa kuiga kila kitu

mabadilikooooo.... magufuli
Magufuliiiii.... mabadiliko!!

Teh Teh Teh Teh Teh

#hapaahaditu
UFISADI ni ajenda endelevu haiwezi kuondoshwa kwa kufuta list of shame..LOWASSA ni MWIZI na hakuna mabadiliko ndani ya LOWASSA bali kuna Ufisadi uliotopea..

#HapaKaziTu.
 
UFISADI ni ajenda endelevu haiwezi kuondoshwa kwa kufuta list of shame..LOWASSA ni MWIZI na hakuna mabadiliko ndani ya LOWASSA bali kuna Ufisadi uliotopea..

#HapaKaziTu.

Unaandika lakini?? Haya

Nyumba za serikali ziliuzwa shilingi ngapi??
Na ile hasara ya kituo cha mafuta mwanza je??
Vepee kuhusu ile meli feki ya kwenda bagamoyo ukilinganisha na Kilimanjaro 5 ya Azam??
Umecheki average cost ya kujenga one kilometer ya barabara na kujua tunapigwa kifisadi matrilioni mangapi??

Bado unaandika lakini??
Hebu andika na hii... Vipi ESCROW, Meremeta, DOWANS, Meno ya Tembo, Twiga na Safari za nje zisizo na kichwa wala miguu??

Haya naomba jumla sasa

#HapaAhadiTu
 
mimi nikiri kuwa siyo mwanasiasa. Nawaombeni msaada kwa nia njema. Hivi uzuri waccm ulianzia wapi na liisha lini? Ni watu gani waliohusika kuifanya nzuri na ni nani aliyeiharibu? Watanzania au mtanzania anataka mabadiliko ya namna gani na ni nini wajibu wa kila mtanzania kwenye haya mabadiliko.
 
unatetea maslai tuu ...mengine yote ni mbembwe tuu kujionyesha nawe umesoma.(wasomi wetu wa copy and paste)
 
Juliana Shonza huna jipya a chanana na upinzani ulikushinda pandikizi wewe. Lowassa tutamchagua kwa kishindo. Mtaomba pooo.
 
Last edited by a moderator:
Peleka katika magazeti yanayopokea makala,maana hii ni story ndefu kusoma
 
Zipo juhudi kubwa za kuwapumbaza watanzania kwa kile kinachoitwa kuwaelewesha ili kufanya Informed Decision kwa kumchagua LOWASSA wa Ukawa dhidi ya MAGUFULI wa CCM..juhudi hizi zilizoimarika hivi karibuni zinatumia waandishi wa habari wa vyombo maalum na wale wa kujitegemea, lakini nguvu hiyo imesambaa zaidi mpaka kwenye mitandao ya kijamii..nguvu ya wanamabadiliko waliobadilika.

Juzi niliandika nikimjibu PASCO wa JF kuhusu kile alichokiita Ujinga wa watanzania kwa kuichagua CCM, akiwa anawaelekeza watanzania kuamini na kumchagua EDWARD LOWASSA eti kwa madai yake HUYU NDIO MUSSA ATAKAYETUVUSHA BAHARI YA SHAMU..lakini hakuishia hapo amejitokeza tena kuendelea na msimamo wake ila kwa bahati mbaya ameacha maswali na hoja muhimu katika majibu yangu na kuhamia katika hoja zingine ambazo majibu yake ni Rahisi...maana amehamia kwenye hoja ya RUSHWA ambae huyo anayemnadi kuitokomeza RUSHWA hawezi hata kuizungumza kwenye majukwa yake ya kisiasa na anaamrisha wengine pia wasiizungumze..AJABU SANA.

I don't believe on mistakes, hivyo siamini kuwa makosa katika nukuu ya PASCO yalikuwa ni BAHATI MBAYA...binafsi najua ni muendelezo wa De Docta Ignorantia, on learned ignorance ambayo PASCO ni mfalme akitaka tumchagua FISI akatulindie BUCHA kwa kigezo kuwa MLINZI wetu wa sasa anasinzia sinzia....Noooooo NEVER..!!

Nitajinukuu;


Kwenye RED ni maeneo ambayo nimeonyesha strength ya CCM ambayo PASCO kakimbia kuyajadili kwa hoja, kuwa CCM imeamua kujijenga UPYA na kufukuza manyang'au wote waliokuwa wanaharibu IMAGE ya Chama, manyang'au hayo yamenunua chaka jipya na wanalipa watu wawasafishe kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii...na bahati mbaya wamejitokeza watu waliojitoa ufahamu na kukubali kutumika..na hakika HAKUNA DENI BAYA KAMA DENI LA TUMBO linawatesa wengi katika watu hata wale wenye elimu zao.

Kwenye KIJANI ni maswali ambayo PASCO kwa maksudi ameyakimbia, HASEMI lolote kuhusu UPINZANI, hasemi kuhusu THE DON na makando kando yake...anasema tu kuwa anachukia RUSHWA lakini hasemi DON LOWASSA amejiandaaje kupambana na Rushwa hata awe bora kuliko MAGUFULI wa CCM..

1. LOWASSA wa CHADEMA na UKAWA ni kielelezo cha ubovu, uchafu na uovu uliokuwa unasababisha harufu mbaya ndani ya CCM kwa zaidi ya miaka 30 aliyokuwa anatumikia Serikali kupitia chama hicho. He re

2. LOWASSA hawezi kuwa Kiongozi wa Mabadiliko (hayo ambayo PASCO) anawaaminisha Watanzania, kwani alikuwa katika mfumo huo kwa zaidi ya miaka 30 na hakubadilisha chochote, leo LOWASSA amebadilika nini..?

3. LOWASSA ni MWIZI, NI MLA RUSHWA MKUBWA na nimeandika haya nikitumia ID yangu kamili, na nitasema haya popote pale..na kwa fedha zake za wizi amekuwa akinunua watu wa kumsafisha kila uchao, nina mashaka ndugu yangu PASCO is on the list.

4. LOWASSA anasimama na mwenzie SUMAYE kukosoa Serikali ambayo maamuzi makubwa yaliyoangamiza TAIFA walishirikia kuyapitisha kama sio KUYASIMAMIA ili yapitishwe na Serikali..leo wamekuwa wasafi ghafla kwa kuwa wamehamia UPINZANI..kama sio UJUHA ni nini..?

5. LOWASSA ameishi, ametenda na ameendelea kutetea IMANI kuwa pesa ndio kila kitu, imani ambayo PASCO and the TEAM MABADILIKO imeendelea kuamini, hawezi kuishi nje ya IMANI hiyo ambayo inapingana na IMANI ya UADILIFU...na tunachotaka watanzania ni MTU MUADILIFU ili akanyooshe mambo yaliyopinda ndani ya Serikali..

5. HAKUNA ushahidi ama rekodi yeyote ambayo inaonyesha LOWASSA amebadilika, bali upo USHAHIDI na REKODI ambazo zinathibitisha kuwa LOWASSA ni MWIZI, MLA RUSHWA, MUONGO na FISADI PAPA..hana moral authority ya kukemea Rushwa.

PASCO..,narudia tena kuwa WATANZANIA sio WAJINGA: tumekusikia, tumetafakari na tumeamua MAGUFULI ndio ajaye. Hatuko tayari kumpa FISI ulinzi wa BUCHA.

VIDEO: KINANA na CCM MPYA

https://youtu.be/bSG2TBeCS_A




Juliana Shonza kama nimekuelewa vizuri, kwa kuangalia picha kubwa una maana kuwa CCM ni Fisi ambaye hawezi kulinda bucha, kwa kuwa tayari tuna ushahidi mwingi wa nyama aliyokula. Sidhani kama kuna anayeweza kubisha hilo. Na tukiangalia picha ndogo unasema Lowassa naye ni fisi ambaye hastahili kupewa ulinzi wa bucha.

Kwa maana hiyo unataka kutuambia tufuate chama cha Zitto Kabwe. Maana ACT si wezi, na mgombea wake si mwizi.

Lakini ni kweli electorate iko tayari kwa ACT na mgombea wake?
 
Chama kinaweza kuwa na sera nzuri sana lakini kama hakina mshika bendera ambaye nyota yake ingang'aa , yaani kipenzi cha watu wengi, hakiwezi kupata ushindi. Ni watu wachache sana watakaotambua kwamba kipo. Hivyo ACT mwaka huu hawapati.
Ccm walidhani wameteua kipenzi cha watu lakini bahati mbaya nyota yake imekuja kufunikwa na ya lowassa. Hapo hamna jinsi tena mshindi ni lowassa tu, hata kama hawataki.

Kila wanavyomchafua lowassa wanamuongezea wanaompenda na wanajichafua wenyewe. Wanataka lowassa aonekane mchafu ili wao waonekane wasafi. Haiingii akilini kwamba wanamshtaki mwizi kwenye kampeni wakati dola wanalo. Watu wamestuka, wagundua mabaya wanayomsemea lowassa ndio mabaya wayafanyayo .

Tatito la nchi hii ccm, hiyo habari ya wizi na ufisadi chanzo ni nini kama siyo ccm?. Wezi ni ccm na mafisadi ni ccm, adui wa maendeleo ni ccm.

Ccm ijiandae kukaa pembeni, kwenye mioyo ya watz mgombea wao amefunikwa vibaya, kununua wasanii haitawasaidia bora wagawe dawa bure mahospitalini.
Na wale wezi na mafisadi wa ccm wajiandae kukamatwa maana nina hakika serikali ya ukawa haitakuwa legelege kama serikali ya ccm.
 
Siku ile nimekufuma umepanda bajaj mnazi mmoja ulikuwa unatoka kuchukuwa buku 7 lumumba? Muambie kinana akununulie japo starlet maana kujibaraguza kote anashindwa kukuona?
 
Wanawafuata watu vijijini kwa malori kuwapeleka kwenye mikutano yao, mtu akipanda kwenye lori anapewa buku tano. Nani abaki? Lakini wakirudi nyumbani jioni wanasema kura ukawa.
 
Juliana Shonza
Ahadi za JK baadhi zinarudiwa kuahidiwa na Magufuli....

Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora .... MAGUFULI KAAHIDI TENA, KWA NINI JK HAKUTEKELEZA HATUJUI NA HAISEMWI....


Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera.... KIMYAAAAA .... KWA NINI JK HAKUTEKELEZA HATUJUI NA HAISEMWI....
Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini ..... KIMYAAAAA....... KWA NINI JK HAKUTEKELEZA HATUJUI NA HAISEMWI....

Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini..... KIMYAA........ KWA NINI JK HAKUTEKELEZA HATUJUI NA HAISEMWI....

Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera...... KIMYAAAA......... KWA NINI JK HAKUTEKELEZA HATUJUI NA HAISEMWI....

Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera............ MAGUFULI KAAHIDI TENA, KWA NINI JK HAKUTEKELEZA HATUJUI NA HAISEMWI....


"The trust of the innocent is the liar's most useful tool"

Haya ni maneno yaliyopata kusemwa na
Stephen King

 
Back
Top Bottom