Elections 2015 King of De Docta Ignorantia: Hatuwezi kumpa FISI ulinzi wa BUCHA

Bavicha mna hoja nyepesi sana, hamnazo kabisa! Kila la kheri tarehe 25.10.2015, ila JPM ndo Rais wa JMT.
 
Ngoja nikusaidie maana naona unahangaika na kutokwa povu katika jambo usilolijua...sikua na tatizo na Slaa wala Zitto, bali nilikuwa na tatizo na aina ya uongozi dhaifu ndani ya CHADEMA, nikaliweka bayana kwenye vikao kuwa umefika wakati Mwenyekiti atupishe, maana CHADEMA ilipofikia ilihitaji renewed vision na mission...na yeye aliendelea kuwa Muhafidhina akiifanya CHADEMA ni yake na familia yake..nililipinga hilo na sio jingine.

Ila kwenye kuzungumzia unafiki ukawalinganisha CHENGE na LOWASSA kisha ukasema CCM na UKAWA ni sawa kwa kuwa sehemu zote mbili kuna WEZI...ni irrelevant comparison..Who is CHENGE kwenye CCM...zaidi ya kuwa mgombea UBUNGE ana lipi jingine ambalo amefungamana na CCM kwalo, hana effect and easy to deal with..ila LOWASSA ndio kila kitu UKAWA, ndio Kauli mbiu, ndio Kiongozi Mkuu, ndio Mgombea Urais., ndio anayedictate nini kisemwe na nini kisisemwe (refer to list of shame)

Lowassa ndio kila kitu kwenye UKAWA...hana mfano wake.
 
Ule msemo wa chukua chako mapema unaanza kuwa kweli sasa. Wajiandae kukaa pembeni hawa ccm, siku zao zinahesabika. Hatuhitaji uongo mwingine toka kwao.
 
hahahaaaaaa... Kumbe copy paste ni syndrome

Nilijua ni ya John Pombe Ngoyai pekee yake mzee wa kuiga kila kitu

mabadilikooooo.... magufuli
Magufuliiiii.... mabadiliko!!

Teh Teh Teh Teh Teh

#hapaahaditu
UFISADI ni ajenda endelevu haiwezi kuondoshwa kwa kufuta list of shame..LOWASSA ni MWIZI na hakuna mabadiliko ndani ya LOWASSA bali kuna Ufisadi uliotopea..

#HapaKaziTu.
 
UFISADI ni ajenda endelevu haiwezi kuondoshwa kwa kufuta list of shame..LOWASSA ni MWIZI na hakuna mabadiliko ndani ya LOWASSA bali kuna Ufisadi uliotopea..

#HapaKaziTu.

Unaandika lakini?? Haya

Nyumba za serikali ziliuzwa shilingi ngapi??
Na ile hasara ya kituo cha mafuta mwanza je??
Vepee kuhusu ile meli feki ya kwenda bagamoyo ukilinganisha na Kilimanjaro 5 ya Azam??
Umecheki average cost ya kujenga one kilometer ya barabara na kujua tunapigwa kifisadi matrilioni mangapi??

Bado unaandika lakini??
Hebu andika na hii... Vipi ESCROW, Meremeta, DOWANS, Meno ya Tembo, Twiga na Safari za nje zisizo na kichwa wala miguu??

Haya naomba jumla sasa

#HapaAhadiTu
 
mimi nikiri kuwa siyo mwanasiasa. Nawaombeni msaada kwa nia njema. Hivi uzuri waccm ulianzia wapi na liisha lini? Ni watu gani waliohusika kuifanya nzuri na ni nani aliyeiharibu? Watanzania au mtanzania anataka mabadiliko ya namna gani na ni nini wajibu wa kila mtanzania kwenye haya mabadiliko.
 
unatetea maslai tuu ...mengine yote ni mbembwe tuu kujionyesha nawe umesoma.(wasomi wetu wa copy and paste)
 
Juliana Shonza huna jipya a chanana na upinzani ulikushinda pandikizi wewe. Lowassa tutamchagua kwa kishindo. Mtaomba pooo.
 
Last edited by a moderator:
Peleka katika magazeti yanayopokea makala,maana hii ni story ndefu kusoma
 

Juliana Shonza kama nimekuelewa vizuri, kwa kuangalia picha kubwa una maana kuwa CCM ni Fisi ambaye hawezi kulinda bucha, kwa kuwa tayari tuna ushahidi mwingi wa nyama aliyokula. Sidhani kama kuna anayeweza kubisha hilo. Na tukiangalia picha ndogo unasema Lowassa naye ni fisi ambaye hastahili kupewa ulinzi wa bucha.

Kwa maana hiyo unataka kutuambia tufuate chama cha Zitto Kabwe. Maana ACT si wezi, na mgombea wake si mwizi.

Lakini ni kweli electorate iko tayari kwa ACT na mgombea wake?
 
Chama kinaweza kuwa na sera nzuri sana lakini kama hakina mshika bendera ambaye nyota yake ingang'aa , yaani kipenzi cha watu wengi, hakiwezi kupata ushindi. Ni watu wachache sana watakaotambua kwamba kipo. Hivyo ACT mwaka huu hawapati.
Ccm walidhani wameteua kipenzi cha watu lakini bahati mbaya nyota yake imekuja kufunikwa na ya lowassa. Hapo hamna jinsi tena mshindi ni lowassa tu, hata kama hawataki.

Kila wanavyomchafua lowassa wanamuongezea wanaompenda na wanajichafua wenyewe. Wanataka lowassa aonekane mchafu ili wao waonekane wasafi. Haiingii akilini kwamba wanamshtaki mwizi kwenye kampeni wakati dola wanalo. Watu wamestuka, wagundua mabaya wanayomsemea lowassa ndio mabaya wayafanyayo .

Tatito la nchi hii ccm, hiyo habari ya wizi na ufisadi chanzo ni nini kama siyo ccm?. Wezi ni ccm na mafisadi ni ccm, adui wa maendeleo ni ccm.

Ccm ijiandae kukaa pembeni, kwenye mioyo ya watz mgombea wao amefunikwa vibaya, kununua wasanii haitawasaidia bora wagawe dawa bure mahospitalini.
Na wale wezi na mafisadi wa ccm wajiandae kukamatwa maana nina hakika serikali ya ukawa haitakuwa legelege kama serikali ya ccm.
 
Siku ile nimekufuma umepanda bajaj mnazi mmoja ulikuwa unatoka kuchukuwa buku 7 lumumba? Muambie kinana akununulie japo starlet maana kujibaraguza kote anashindwa kukuona?
 
Wanawafuata watu vijijini kwa malori kuwapeleka kwenye mikutano yao, mtu akipanda kwenye lori anapewa buku tano. Nani abaki? Lakini wakirudi nyumbani jioni wanasema kura ukawa.
 
Juliana Shonza
Ahadi za JK baadhi zinarudiwa kuahidiwa na Magufuli....

Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora .... MAGUFULI KAAHIDI TENA, KWA NINI JK HAKUTEKELEZA HATUJUI NA HAISEMWI....


Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera.... KIMYAAAAA .... KWA NINI JK HAKUTEKELEZA HATUJUI NA HAISEMWI....
Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini ..... KIMYAAAAA....... KWA NINI JK HAKUTEKELEZA HATUJUI NA HAISEMWI....

Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini..... KIMYAA........ KWA NINI JK HAKUTEKELEZA HATUJUI NA HAISEMWI....

Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera...... KIMYAAAA......... KWA NINI JK HAKUTEKELEZA HATUJUI NA HAISEMWI....

Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera............ MAGUFULI KAAHIDI TENA, KWA NINI JK HAKUTEKELEZA HATUJUI NA HAISEMWI....


"The trust of the innocent is the liar's most useful tool"

Haya ni maneno yaliyopata kusemwa na
Stephen King

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…