Kinga kwa viongozi baada ya kustaafu haitawasaidia kabisa viongozi hao endapo upinzani utachukua nchi

Kinga kwa viongozi baada ya kustaafu haitawasaidia kabisa viongozi hao endapo upinzani utachukua nchi

M-mbabe

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2009
Posts
13,203
Reaction score
23,027
Huu ndiyo ukweli wenyewe.

Wapinzani wakichukua nchi watatumia fimbo ile ile ambayo sisi CCM tumekuwa tukiitumia dhidi ya tusiowapenda, wakiwemo wa vyama vya upinzani.

Na tusijidanganye kuwa CCM tutakaa madarakani milele. Dalili zilizopo zinaonyesha tutaondolewa madarakani muda si mrefu.

Kitakachotokea upinzani ukiingia ikulu ni hiki:

Bila kujali ni kinyume cha katiba au la, kwa nyakati tofauti (say kwa interval ya miezi sita sita) serekali chini ya upinzani itawasweka Segerea viongozi wastaafu kwa mashitaka yasiyodhaminika kwa staili ile ile inayotumika sasa. Wanaweza kukaa selo hata kwa miaka 15 kwa kisingizio cha kutokamilika kwa upelelezi. Yatakuwa ni majuto makubwa sana kwao na kwa wanaowategemea.

Nitoe wito kwa watu wenye ushawishi ndani ya chama chetu CCM waendelee kuwashauri sana viongozi walio madarakani sasa kuzingatia kutenda haki kwa wote ili wasiwape kisingizio wahasimu wao kuja kulipa visasi huko mbeleni.

What goes around comes around!
 
Mkuu mi nadhani kinga itaendelea kuwepo hadi pale mabadiliko ya Katiba yakifanyika.
 
MKUU MI NADHANI KINGA ITAENDELEA KUWEPO HADI PALE MABADILIKO YA KATIBA YAKIFANYIKA.
Ni kweli kinga itakuwepo lakini bado wataswekwa rumande "wakisubiri upelelezi ukamilike".

Na "upelelezi ukikamilika" baada ya miaka 15 itajulikana kumbe wana kinga, wataachiliwa huru!
 
Kwa hiyo waache wabadili sheria za kuwalinda lakini wakae wakijua kuwa kuna mwamba anawasubiri huko mbeleni.
 
Back
Top Bottom