Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Ugonjwa wa Malaria kwa wanawake wanajawazito huleta athari kubwa za kudumaza ukuaji wa mtoto tumboni au kuufanya ujauzito husika uharibike.
Ili kuondoa athari hizi, Serikali kupitia Wizara ya Afya imeweka utaratibu wa wanawake wote kupata dozi tatu za dawa ya SP (sulphadoxine+pyrimethamine ) kuanzia wiki ya 14 ya ujauzito.
Dawa hizi hutumika kama kinga ya kuzuia vimelea vya Malaria visizaliane kwenye kondo la uzazi, sehemu inayo muunganisha mama na mtoto.
Madhara mengine ya ugonjwa huu ni kupatwa na tatizo la upungufu mkubwa wa damu, kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo au njiti pamoja na kuingilia mfumo wa utengenezwaji wa viungo vya mtoto hivyo kumfanya azaliwe akiwa na mapungufu ya kudumu.
Kwa kuwa kinga ya ugonjwa wa Malaria hupungua sana kwa wanawake wajawazito, ni muhimu kujilinda kwa kutumia dawa hizi ili dhumuni la kupunguza vifo vya mama na mtoto litimie.
Chanzo: Wizara ya Afya ( STG NELIT 2021)