Kingereza ni mtihani jamani

MAUBIG

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
1,039
Reaction score
855
Habari wadau,

Hii imetokea leo kwenye basi la kampuni maarufu hapa Dodoma. Ilikuwa kama ifuatavyo:-

Mnamo majira ya asubuhi Leo nilipanda basi kwa lengo kwenda Dodoma mjini nikitokea moja ya wilaya za Dodoma. Jirani na nilipokaa kulikuwa na mzungu amekaa ila tatizo siti haikuwa yake. Baadaye kidogo mwenye siti yake akawasili, tabu ndipo ilipoanzia.

Jamaa akaanza kulalamika kwa Konda kwamba siti yake imekaliwa, Konda kucheki anakutana na mzungu, akagwaya kidogo, ikabidi amwambie yule abiria amwambie mzungu apishe, abiria akagoma na kumwambia konda yeye ndio amwambie kwani ndio kazi yake, basi ikawa ni kusukumiana mpira kati ya konda na mwenye siti. Mwishoni kabisa abiria akaona isiwe tabu, akamuongelesha mzungu na bila shida akasimama zake mzungu wa watu.

Lakini cha ajabu kuna mswahili mwenzetu naye alikaa siti ya mtu, makonda wakamkomalia na maneno makali mpaka jamaa akasimama. Nikaja gundua kumbe kwa mzungu walikuwa kama wamemwagiwa Maji lakini kwa mbongo mwenzao kisa lugha gongana

Taabu tupu
 
Si ungewasaidiaa kuongea kiingereza na mzungu! !!!!!
 
Kingereza siyo lugha yetu.huhitaji kushangaa. Je hujawahi kumsikia balozi wa japan, china au urusi hapa tz. Vipi kingereza chao? Kwa hiyo usijisike vibata mtu asipozungumza kiingereza vizuri. Haina tofauti na mhindi au mwingine yeyote anayekosea kuzungumza kiswahili.
 
konda hana tatizo kwa kuwa na kwa wale wasiojua kuongea vizuri wasilaumiwe kwa kuwa siyo lugha yao.
 

Nakubalina na wewe, lakini haya sio aina ya majibu ya kuzoea, Kiingereza kinafundishwa kuanzia darasa la tatu kwa shule za kanumba, na ndio lugha ya kufundishia kuanzia form one mpaka chuo kikuu, sasa kwa nini tushindwe kukiongea?
 
Acheni kujiweka nyuma nyuma nyie hakuna lugha rahisi duniani kama kiingereza!
 
Sio kila mzungu anaongea kiingereza wengine spaniol kifaransa kijerumani ki russia n.k acheni ushamba
 
Hapa una maanisha Kiingereza sio mashariki?

Wakuu,nilishawahi kukutana na hao "waropa" mahali fulani kwenye usafiri,na ingawa ninako kaki-ropa ka-ugoko,kila walipoongea kiingereza mi nkijibu kiswahili.Weee...acha kabisa!Kiswahili walichojibu,kaaazi kweli kweli,yaani vituko!Lugha yeyote ni ngumu kama huna weledi wake.Tujiamini jamani!
 

Bo ng'wa Queen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…