MAUBIG
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 1,039
- 855
Habari wadau,
Hii imetokea leo kwenye basi la kampuni maarufu hapa Dodoma. Ilikuwa kama ifuatavyo:-
Mnamo majira ya asubuhi Leo nilipanda basi kwa lengo kwenda Dodoma mjini nikitokea moja ya wilaya za Dodoma. Jirani na nilipokaa kulikuwa na mzungu amekaa ila tatizo siti haikuwa yake. Baadaye kidogo mwenye siti yake akawasili, tabu ndipo ilipoanzia.
Jamaa akaanza kulalamika kwa Konda kwamba siti yake imekaliwa, Konda kucheki anakutana na mzungu, akagwaya kidogo, ikabidi amwambie yule abiria amwambie mzungu apishe, abiria akagoma na kumwambia konda yeye ndio amwambie kwani ndio kazi yake, basi ikawa ni kusukumiana mpira kati ya konda na mwenye siti. Mwishoni kabisa abiria akaona isiwe tabu, akamuongelesha mzungu na bila shida akasimama zake mzungu wa watu.
Lakini cha ajabu kuna mswahili mwenzetu naye alikaa siti ya mtu, makonda wakamkomalia na maneno makali mpaka jamaa akasimama. Nikaja gundua kumbe kwa mzungu walikuwa kama wamemwagiwa Maji lakini kwa mbongo mwenzao kisa lugha gongana
Taabu tupu