Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kingu awashukia wanamchonganisha Rais na Bunge, asema hakuna Mbunge anaweza kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Rais
Akichangia Bungeni leo Aprili 08, 2026, Mbunge wa Ikingu Magharibi, Elibariki Kingu amewaonya wale wanaojaribu kuleta mgogoro kati yao na Rais.
“Hakuna Mbunge hata mmoja wa kuthubutu kuwaza mambo kinyume na Rais wetu tuliyemchagua na kumpigania. Kuna watu kazi yao kutunga majungu na kupitia hayo majungu wanataka wapate fedha ili kusudi ionekane eti Bunge lina mgogoro na Rais,” anaeleza Elibariki Kingu Mbunge wa Ikungi Magharibi.
“Wale wanaopeleka majungu kwamba kuna wabunge eti wanataka kupiga sijui kura ya kutokuwa na imani.. hakuna Mbunge hata mmoja wa chama Cha Mapinduzi atahangaika kupoteza muda kazi yetu itakuwa kumlinda Rais,” aliongeza Kingu.