Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Emmanuel Kingu, amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya nchini, hatua inayofanya huduma za tiba kuboreshwa kwa kiasi kikubwa katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani.
Kingu ameeleza kuwa ni jambo lisilo la haki kusema kwamba Watanzania milioni 60 wanaweza kwenda kutibiwa Zanzibar, akisisitiza kuwa kauli hiyo inalenga kumdhalilisha Rais Samia na kudharau juhudi kubwa zilizofanyika katika kuboresha miundombinu ya afya nchini.
Soma: Kaimu Waziri wa Afya-Saada: Hatuwezi Kuwatibu wasio Wazanzibari
Ameongeza kuwa serikali imewekeza katika ujenzi wa zahanati, vituo vya afya na hospitali pamoja na ununuzi wa mashine za kisasa za matibabu, hali inayofanya hata wagonjwa kutoka mataifa mengine kuja Tanzania Bara kupata huduma kutokana na ubora wa miundombinu iliyopo.