Kingu: Kusema Watanzania milioni 60 kutibiwa Zanzibar ni kumdhalilisha Rais Samia na kudharau juhudi zake

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Emmanuel Kingu, amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya nchini, hatua inayofanya huduma za tiba kuboreshwa kwa kiasi kikubwa katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani.

Kingu ameeleza kuwa ni jambo lisilo la haki kusema kwamba Watanzania milioni 60 wanaweza kwenda kutibiwa Zanzibar, akisisitiza kuwa kauli hiyo inalenga kumdhalilisha Rais Samia na kudharau juhudi kubwa zilizofanyika katika kuboresha miundombinu ya afya nchini.

Soma: Kaimu Waziri wa Afya-Saada: Hatuwezi Kuwatibu wasio Wazanzibari

Ameongeza kuwa serikali imewekeza katika ujenzi wa zahanati, vituo vya afya na hospitali pamoja na ununuzi wa mashine za kisasa za matibabu, hali inayofanya hata wagonjwa kutoka mataifa mengine kuja Tanzania Bara kupata huduma kutokana na ubora wa miundombinu iliyopo.

Your browser is not able to display this video.
 
Stupid, lazima kutaja Rais! Haya majitu sijui yakoje vichwani....yanatafuta teuzi as if yataingia kaburini na teuzi
 
Huyo waziri wa ZNZ ni mpumbavu sana. Alikuwaga naibu waziri wa fedha, alikuwa wa ovyo mno, hakujua hata alilokuwa akiongea. Nimeshangaa watu kwenda kutibiwa Zanzibar, labda wawafuate waganga wa kienyeji. Tanganyika tuna huduma za kibingwa, sijawahi kusikia mtu anaenda kutibiwa Zanzibar akitokea Tanganyika, wao ndiyo wanakuja Tanganyika. Huyo mama ana shida ya akili, kwa vile alivyo alivyo ni lazima ana matatizo ya mtindio wa akili.
 
Mh.Kingu yuko sahihi 100%,

Dr Samia Suluhu Hassan amewekeza vya kutosha kuhudumia waTanzania wote bara na visiwani na mpaka hata wagonjwa kutoka nje ya nchi 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Alishakuwa Waziri Kamili wa Fedha wa Jamhuri ..kazingua
 
Huyo msukuma ni mbogamboga tu kama maccm wengine tu hana mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…