Kingunge amechanganyikiwa?

Hakuna haja ya kumshangaa mzee Kingunge katika hili, watu wangejua Pesa anayopewa na kina RA awatetee, wangegundua kuwa anafanya hivyo under influence.

Mzee K pole, ila ukome kuwatetea mafisadi na unyamaze kimya
 
Babylon, nakubaliana nawe sana. Lakini sasa tutajuaje athari za warakahuo kama mzee wetu hataki kusema utatuleteaje matatizo? Kama wewe unayajua tafadhali naomba utuambie ili nasi tuelewe. Naomba muibadilishe mitizamo yetu kwa hoja, badala ya hisia.

Kuna msemo mmoja wa wazungu unaosema "Guilty Afraids". Je tuanze kuubandika msemo huo kwa mzee Kingunge?
 
Tatizo moja ninaloliona kuhusu waraka huu wa kanisa katoliki na jinsi watu wanavyoujadili ni kwamba; watu wanaangalia nani kauandika badala ya nini kimeandikwa . Consequently, what is being discussed is not what has been written[issues-Hoja] but the authors.[the Roman Cathoric Church]. Dini zote nadhani zitakubaliana na hicho kilichoandikwa kuwa wananchi wanapaswa kuchagua viongozi waadilifu irrespective of their religious beliefs kwenye uchaguzi ujao; na kuna very high correlation kati ya viongozi waadilifu na hali ya maisha ya waumini wao,kwahiyo wakichagua viongozi mafisadi mzigo utawaangukia wao kuwahudumia waumini wao hali inapowawia kuwa ngumu!! Dini zote basi ikiwemo ya wakatoloki wana kila sababu ya kuwaelimisha waumini wau wachague viongozi bora na makini. Mafisadi ndani ya CCM kama wakina Kingunge hawawezi kupenda waraka huu kwa sababu ushindi wao katika chaguzi unategemea sana ujinga wa wadanganyika ambao waraka unasahihisha!
 
Kama tunataka kuheshimu KATIBA ya nchi yetu ni vizuri sasa Serikali iache kupeleka HOJA ya mahakama ya KADHI na suala la Tanzania kujiunga na OIC kujadiliwa bungeni. Kumbuka kuwa hoja hizo zilipelekwa bungeni na Serikali. Hoja zote hizo ni za kidini, je Katiba haitambuliki hapa?

Waraka wa Katoliki haukuomba baraka wala msaada wa Bunge wala Serikali. Wao kama chombo kimoja wapo ktk nchi yetu cha kuelimisha jamii, waliona ni busara kutoa mwongozo kwa wananchi juu ya kumpata kiongozi bora. Nina imani kubwa sana, kwa kuzingatia maandiko ya vitabu vya dini zetu, madhehebu mengine yakitoa waraka wao, utakuwa na mtizamo unaofanana na huo wa Katoliki.
 
Kama kuna hoja hakuna tatizo. Watu wananmwuliza aonyeshe hayo mambo yanayohatarisha amani. Jibu lake ni kuwa waraka utawagawa watanzania. Kwa mtu wa namna hii kuna haja gani ya kumsikiliza? No resesearch no right to speak inafanya kazi hapa.

Unakataa uzee usitumike kujadili pumba zake ambazo wewe unaita maoni wakati huohuo wewe mwenyewe unasema uzee wao usitumike hapa uko upande upi? Kilichowazi lazima kutafuta chanzo cha mtu kutoa pumba kama za huyu mzee. Moja wapo ni kuishiwa uwezo wa ufikiri ukihusishwa na umri kumtupa mkono. Kubwa zaidi ni UFISADI ambao ndio umemsukuma kutamka haya
 
Bulesi, Thank you very much for your understanding in this regard. Tunahitaji kujadili kwa mtizamo chanya na sio hasi. Tukijikita ktk mtizamo hasi, basi tutajikuta tunajadili viatu vya Askofu Kilaini ni vizuri sana, miwani yake ni ya bei mbaya, Jjoho lake ni zito, na kadhalika...

Sidhani kama huko ndiko tunakotaka kwenda, unless nimedandia bus nisilojua liendako.
 
MC, sitashangaa nikisikia kuwa mzee wetu kishatumbukia ktk dini ya ufisadi, maana hatoi kauli za kukemea ufisadi pale anapohitajika kufanya hivyo, bali hukaa kimya kana kwamba hakuna jambo zito zinaloendelea, badala yake, wakijitokeza watu kuupinga ufisadi, yeye ndiyo anajitokeza na kuwakemea, sasa anataka tuamini nini kutokana na vitendo vyake hivyo?
 
mmh huyu mbunge sijui wa chama gani?maana sijamuelewa kabisa yuko upande gani
 
Kingunge, Kingunge, Kingunge, Mwana wa Kilwa

Salamu

Ama baada ya salamu mimi ni mzima hofu na mashaka ni kwako wewe ulie mbali na upeo wa macho yangu

Dhumuni la waraka huu ni Upumbaf wako unaoouonyesha katika siku za karibuni kupitia Bunge letu tukufu na vyombo mbalimbali vya habari.

Nabii Issa kati ya mafundisho yake maarufu ni pamoja ya lile la “ MTI UTATAMBULIKA KUTOKANA NA MATUNDA YAKE”

Kama ulivyojieleza karibuni kuhusu historia yako, ni kweli hakuna awezaye kuielezea sio kwa sababu ni ngumu ama ndefu, HAIPO.

Miaka yote zaidi ya Arobaini katika siasa za Tanzania hakuna hata sehemu moja ambayo unaweza kukuta nyayo za kingunge Ngombare Mwiru, hakuna matunda ambayo watanzania leo hii wanajivunia Wakiyala kwa sifa na heshima ya Kingunge ,hakuna. Watanzania hawajui matunda uzaayo Kingunge, hawafahamu wewe ni mti wa namna gani, MNAFKI?

Ulipopigania uhuru wa nchi hii ingawa ni ngumu kuthibitisha si kwa ajili yako na wenzio wachache, Ilikuwa ni kwa faida ya wengi kwa hiyo kama ni kweli wakoloni walikutukana kwa hilo basi walikuwa sahihi kwani walijua kuwa u mnafki na leo hii watanzania wanashuhudia ukweli wa wakati ule UNAFKI.

Nikuulize swali moja wewe, nini tofauti ya Waraka na Ilani? Kama ungeweza tofautisha haya mawili usingetukanwa kama unavyodai wala kulaaniwa bali ungesifiwa na kushukuriwa kama watanzania wengine walio na upeo wa kujua tofauti ya haya mawili, kitu kingine Nikiita kuku ,kuku hilo sio tusi bali ni jina la kweli bali nikiita mbuzi kondoo hilo ni tusi kwa mbuzi, wewe kuitwa mpumbavu, Fisadi sio matusi hizo ni sifa zako na unaendelea siku hadi siku kuzionyesha machoni pa watanzania, NYAMAZA PUMBAF WEWE.

Umoja wa kitaifa , unajua nini wewe kuhusu hili? Mwalimu kati ya mafundisho yake makubwa kwa taifa hili alituelezea sifa za maendeleo, alisema ili tuendelee tunahitaji,1.………..,2.…………,3.……………,4.………….

Kingunge unaweza kujazia humo .....enh...enh...unasema,....enh... siku nyingi? umeshasahau? Katika hilo la nne ndio limekuwa tatizo kwa watanzania kwa kipindi chote tokea uhuru na kubwa wakati huu, kwa kiongozi wa jamii ya watanzania katika ngazi yoyote ile atakuwa amelisemea hili katika namna tofauti lakini kwa lengo moja, kuwaonyesha watanzania ufahamu wake wa matatizo yanayowakabili. Kitendo cha wewe kupinga waraka wa Wataaluma wa Kikatoliki na sio Maaskofu kama unavyodai inaonyesha wazi kuwa hujui matatizo yanayowakabili watanzania,UFISADI iwe kwa ufahamu wako haba ama kuchagua kupigana kwa kuwa wewe nawe ni mmoja wao.
Rostam anaimba" mimi ni mmoja wao katika mafisadi ,je wewe Kingunge............."

Wanaigawa nchi? Nani hao, wanaokutuma ama wanaowaumbua

Babu sikiliza, wanaokutumia wanakosea haki ya umri wako sababu haviendani, Kubwa zima aibu................ wamejaribu kujitetea wenyewe wamekwama sasa wameamua watumie ma-agent wao ukiwa mmoja wao, kwa gharama gani Kingunge unauza utu wako? ............. gharama gani Kingunge.

Mwishoni namshukuru mjumbe wako wa nyumba kumi aliyekusomea waraka wangu huu mimi niko mkoani mara bado nakunywa maji yenye sumu toka kwenye mgodi wa dhahabu.

Wasalimie wengine wote huko .

Ndimi Mjukuu wako
 
Nimekuelewa vema, hata hivyo wale wanao lilia wembe wakiamini haukati si wapewe?
 
Kama kuna kitu kinachoweza kutishia amani ya nchi yetu sio waraka huu wa wataalam wa kikatoliki bali ni watu kama Mzee Kingunge Ngombale Mwilu ambao wanatumia nafasi zao katika chama kuwahadaa wananchi badala ya kuwa chimbuko la hekima kama watu tunavyotarajia kutoka kwa wazee kama yeyee. Huyu mzee, kama wanaCCM wataendelea kumsikiliza atawafikisha pabaya kwani maneno na mwenendo wake wa hivi karibuni unaashiria kuligawa Taifa letu; mfano mzuri ni hivi karibuni pale bungeni alipotumia CCM kukataa kubadilisha budget ya wizara ya miundombinu; kwakukata kubadilisha budget ile maana yake ni kwamba mgawanyo wa resources utaendelea kupendelea maeneo wanayotoka mawaziri na viongozi wa nchi na kwakufanya hivyo kutatokea uhasama wa wananchi wa maeneo mbali mbali ya nchi. Kingunge akumbuke kuwa uneven distribution of the National Resources ndio chanzo cha machafuko na uvunjifu wa amani katika nchi zinazoendelea na kamwe elimu kwa wananchi haivunji amani bali inaleta maelewano baina ya watu..
 
Mimi nadhani waraka wa Kaholiki ungeweza/unaweza kuwa na manufaa sana kwa vyama vya siasa na kwa Taifa zima badala ya kudhani vinginevyo.

Pamoja na nia njema ya waraka huo, ingefaa zaidi kuangalia maeneo yanayoweza kuboreshwa ili waraka huo au mwingine wowote uwe mzuri zaidi. Kwa mtazamo wangu, sioni tatizo kama taasisi nyingine zote (za kidini na za kiraia) zingetoa mapendekezo yao kama ambavyo CPT walivyofanya kwa kutoa waraka wao. Naamini pia kuwa ni haki ya kila mpenda maendeleo kushiriki kupendekeza namna bora ya kuimarisha uongozi wa nchi yetu, kuboresha ustaarabu wa watu wetu na pia kuweka misingi bora ya kiuchumi, ulinzi, elimu, na ustawi wa jamii kwa jumla n.k.

Nashindwa kuelewa nini hasa kinachowakera viongozi wetu hasa wanapopata ushauri kupitia waraka kama huu, bila gharama yoyote. Naamini pia kuwa, ilani zote za vyama vya siasa zitakazoanza kutolewa muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010, hazitapingana kimaudhui na waraka huu. Sasa nini hasa kinachowakera?
 
Sioni mahali popote ambapo waraka huo wa Katholiki unashabikia kwa namna yoyote uwakilishi wa kidhehebu. Waraka huo haujasema kiongozi bora ni lazima awe mkristu, au ni lazima aamini lolote linaloaminiwa na wakristu, wala anaeshiriki katika mambo yanayoshirikisha ukristu.

Waraka uko kamili na hauna ahadi za kampeni kwa wagombea wowote kama wataamua kuufuata, hauna hata nia ya kulazimisha ufuatwe. Unabaki kuwa ni mapendekezo na matamanio ya waliyouandaa kuhusiana na aina ya uongozi wanaodhani unafaa kwa Taifa letu.


Sioni mahali popote katika kauli wala mapendekezo ya waraka uliotolewa na Katholiki unaotaka au kukusudia kuingilia serikali katika kupata viongozi wake. Nadhani iko wazi kuwa waraka huo unatamani serikali itakayosaidia kuwafanya wananchi waweze kufuata maadili mema na si vinginevyo.

Kwa mtazamo wangu hakuna taasisi zozote ambazo hazina siasa ndani yake. Hata Taasisi za dini zina siasa zake, nazo ndizo zinazofuatwa na viongozi na waumini wao. Siasa ni utaratibu ambao unahusisha watu kila wanapobidi kushirikiana kwa umoja wao.

Serikali haiwezi kushinikiza kuwa dini zisiwe na kauli yoyote kama inaona mambo yanakwenda mrama katika uongozi wa serikali hizo. Ni vigumu kwa kuwa, waumini wao ndio hao hao wanaoshiriki katika serikali na ndio wanaokuwa affected na siasa za vyama na serikali inayokuwa madarakani. Inawezekana dini ikaachana na siasa za vyama na serikali endapo tu, wanachama wa vyama na wanaohusika na serikali watakuwa ni tofauti na wale wanaoamini katika dini hizo.
 
mimi nahsi mzee kingunge amesema kweli. kwani amesema ndani ya waraka huo uansema " kanisa litahakikisha linaweka watu wake na kuwadhibiti" sasa jee kanisa litapofanikiwa kuweka watu wake na kuwadhibiti . itakuwa kwa manufaa ya nani?
Mkuu, sidhani kuwa hayo yamesemwa kwenye waraka huo. Labda utusaidie kujua ni kwenye kurasa zipi maneno hayo yaliandikwa.
 

Mkuu Wild hapa sina cha kuongeza. Hayo ni maswali ambayo Kingunge alitakiwa kujiuliza siku nyingi lakini naona ni kama hata kujiuliza sasa hivi hawezi. Kuna mengi ambayo yana connection na dini yanatokea kila leo lakini alikaa kimya, lakini hili la kuwashambulia mafisadi linakuwa nongwa. Sasa sijui mzee wetu lengo lake hasa ni nini, na uju be wake hasa ni nini.
 
Mimi nadhani tatizo sio waraka. Tatizo ni:

1. Uvivu wa kusoma kwa watanzania wengi ambao wanaambiwa badala ya wao wenyewe kusoma na kutafakari yaliyomo.

2. Michango ya mawazo toka taasisi mbalimbali ni muhimu. Tatizo ni kutokuwa na mfumo rasmi wa kupokea michango hiyo.

3. Baadhi ya wanasiasa bado wako kwenye zama za kuwaona wananchi kama ni watu wa kupiga kura tu na kusubiri miaka mitano mingine. Siasa za sasa ni shirikishi, ambapo wapiga kura wangependa kuona wale waliowachagua wanafanya yale wanayotarajiwa kufanya.

Katika hili, naamini kanisa na Kingunge wana mambo yanayotakiwa kurekebishwa.

Badala ya kuita ILANI (Hii ni kwa vyama vinavyotaka dola) wangeita orodha ya vipaumbele. Nadhani wangepunguza mzozo na wanasiasa.

Kingunge anatakiwa kuelewa kwamba siasa za sasa ni shirikishi. Sio zile alizosoma Lumumba miak hiyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…