Recta.
hapo juu umesema kwamba wito huu ni kwa waumini wake... vizuri sana, lakini tatizo ni kwamba wewe ndiye mwenye makosa kulingana na mawazo ya wawakilishi na watu wengine niliowasoma humu..kwani muda wote watu wamesisitiza kuwa waraka umetolewa sii kwa waumini wa kikatoliki peke yake isipokuwa kwa wananchi wote, na ndio maana serikali inatakiwa kuhusishwa. Hivyo kama wameutoa kwa waumini wake kulikuwa na haja gani kupata baraka za serikali kwani hii ni haki yao wenyewe unless hatua waliyotaka kuichukua ingepingana na baadhi vifungu vya katiba yetu..
Mkuu toka huko nyuma tunazoga kuhusiana na waraka kwa sababu unalenga watu wote na nachosema mimi sikatai maudhui ya waraka huu lakini tatizo ni pale tu mnapotumia vigezo na sababu za dini kukuipeleka ujumbe na kikubwa zaidi ni kuhusishwa kwa kanisa badala ya wataalam walioandika waraka huo moja kwa moja, hata kama hawa wataalam walisoma au ni wataalam toka kanisa Katoliki.
Muheshimiwa amekuonyesha kwamba huo "waraka" umelengwa kwa waumini wake kwa kuunukuhu waraka wenyewe. Wewe unaamua kuu-ignore huo waraka na kuamini watu wengine wanachokuambia. Na mimi nikikwambia waraka huo umetumwa na Vatican utaamini tu kwa sababu umenisoma hapa? Au unachagua kuamini unachotaka kukiamini?
Ushaambiwa waraka wenyewe unajieleza mlengwa wake ni nani. Mimi nadhani busara ingesema kingine chochote ni makosa. Na kwa kufuta mantiki hii, nakubaliana na wewe kwamba kutaka baraka za serikali (kama hicho kitu kweli kimefanyika) inaweza ikawa ni makosa. Lakini hata kama makosa hayo yakfanywa na aliyetunga huo waraka, haibadilishi kilichoandikwa na waraka huo, na mlengwa wa waraka huo atabaki ni yule yule.
Wewe ukiambiwa waraka unakuhusu lakini ukakuta paragraph ya kwanza inasema "waraka huu ni kwa ajili ya wezi", na wewe unajijua si mwizi, au "waraka huu ni kwa ajili ya wapagani" na wewe unajijua si mpagani, au "waraka huu ni kwa ajili ya malaika" na wewe unajijua si malaika, pengine utaendelea tu kuusoma lakini je, utaendelea tu kung'ang'ania kwamba wewe ni mlengwa kwa sababu tu kuna mtu kakwambia wewe ni mlengwa? Mimi nadhani hapo utamrudia liyekwambia na kumuuliza "mbona umeniambia kwamba mimi ni mlengwa wa huu waraka wakati wenyewe unasema tofauti" na sio kusema waraka umekosewa.
Ligi nyingine zinaweza kuwa ndeeeeefu, kumbe wote mko upande mmoja.
Again, nitasema kuhusishwa kwa kanisa ktk maswala ya siasa ambayo kila mmoja wetu ana imani yake, kisha wakatumia vigezo vya mafundisho ya kanisa ambayo mimi Mkandara na raia wengine ktk madhehebu yao tofauti na Katoliki, wataona haya sii mapendekezo bali ni shinikizo kwa serikali kufuata yalke wanayoyafikiria wao...maanake ni mafundisho ya kanisa ambalo mimi sikubaliani na mafuindisho yake!
Utanisamehe sikutaka kusema hivi ila ni ktk kujaribu kupanua mtazamo wako kwa watu wengine wasioamini kanisa katoliki hivyo nimetumia jina langu mwenyewe upate kutazama upande huu..
Kwa hiyo sasa mlengwa mwengine wa waraka huo amekuwa Serikali? Serikali inashinikizwa vipi na huu waraka? Na inashinikizwa kufanya nini? Unaweza kutaja hata kamstari kamoja ka waraka huo ambacho kinasema serikali inashurutishwa kufanya kitu?
Nakubaliana na wewe si sawa kumshurutisha mwingine kufuta imani yako. Ila nina maneno mawili matatu kwako, na lengo ni kuonyesha aina ya dishonesty ya baadhi ya arguments kwenye thread hii.
Kwanza, kwa nini ukausoma huo waraka wakati haukuhusu? Kama ulivyokwishaoneshwa, waraka unajieleza wazi mlengwa ni nani.
Pili, kama uliusoma na kuona kwamba unazidi kupingana na imani yako, kwa nini usiamue kutoufuata tu mashauri yake kama vile ambavyo hufuati mashauri ya maandiko mengine mengi yanayotolewa na watu hao hao? Yaani ukiona inakupendeza kuchagua wezi, waraka huo utakuzuia kufanya hivyo?
Mkuu wangu hata katika Kuondoa Umaskini wetu, mara nyingi IMF inatuandikia waraka wake wakitoa masharti mengi yanayohusiana na Uongozi bora.. WE as tanzania hupokea waraka ule kwa kufahamu hiki chombo kinatawaliwa na watu gani na tunaelewa fika ushirikiano wake na financial Institution ikiwa ni pamoja na World Bank.. hivyo tunapokubaliana nao tunafahamu tumekubaliana na watu gani acha kabisa ile habari ya wataalam kwani hata alipokuwepo huko mzee Mtei (mtanzania mwenzetu) hakutuwakilisha sisi ila aliwakilisha vyombo hivyo...Mtei alituwakilisha sisi akiwa waziri na raia wa Tanzania lakini anapokuwa chini ya chombo fulani na kutoa mawazo yake chini ya nembo ya IMF mkuu wangu huyu mtu hawakilishi wananchi wala nchi ila anawakilisha taasisi yake. Na Nyerere alipokataa, hakukataa kwa sababu ni ushauri wa Mtei ila alichokataa ni masharti ya IMF.. ieleweke hivyo!
Ni katika mtazamo huo, watu kama Kingunge hawezi kukubaliana na mawazo yanayotanguliwa na imani ya dini.. Utanisamehe, binafsi naposoma waraka ukisema ati wao WAMETUMWA, hali mimi siamini utume wao inanipa shida kuamini kinachowakilishwa..Lakini kama watawakilisha Wakristu na dhehebu la katoliki basi huu mjadala wala hauna sababu kuendelea. Mimi naunga mkono kabisa na naweza jiunga nao hata kama ni Muislaam au Pagani maadam nakubaliana na mawazo yao ...
Nadhani Mkandara ni kichwa. Ukweli ni kwamba mlengwa amewekwa wazi kwenye huo waraka, ni vingine vyote vinaonekana kama ni propaganda kwangu. Wewe ndio uamue kuzifuata au la.
Busara yako na ikutangulie muhishimiwa Mukandara. Kama kuna jirani yako mkatoliki anayetaka kuufuta waraka huu, mpe moyo kwa sababu atakayofanya yatakuwa kwa faida yako pia. Ukitaka kujua atafanya nini, soma huo waraka (ignore all religious stuff).
Unajua argument ya msingi inayowekwa mbele na wanaopinga huu waraka ni udini kwenye siasa. Ambayo inaweza kuwa ni valid argument.
Lakini sijasikia hata mmoja akiseme nini kwenye huo waraka ni tatizo. Ni nini kwenye huo waraka hao wakristu wanaambiwa wafanye ambacho ni kibaya, au ni uvunjaji wa sheria. Ni nii hicho wanachoambiwa hao wakristu ambacho wakikifanya nchi hii itaenda pabaya, au mafisadi ndio watazidi kustawi. Ningependa nisikie ni nini hicho kilichoko kwenye huo waraka ambacho hao wakristu wakikifanya basi watakuwa wamewafanyia ubaya waislamu na wenye imani nyingine na wasio na imani.
... lakini siwezi kuwalazimisha watu wote kuamini kwamba waraka huo unawakilisha Watanzania wote... Utanisamehe mkuu lakini mimi Mkandara siwakilishwi na kanisa wala Bakwata ktk maswala ya kisiasa.
Hoja ya uwakilishi katika context hii pengine ni hoja yenye matege.
Unamaanisha nini na waraka huo "kuwakilisha" kundi fulani la watu, au watanzania wote? Mimi sioni huo uwakilishi unaouzungumzia. Huu waraka unawaambia walengwa wake nini cha kufanya, kwishnehi. Na pengine wasipoufanya wataenda motoni (lol haya ni maneno yangu usije ukasema jamaa wanawatishia waumini wao). Hakuna swala la uwakilishi hapo. Kama wewe ni muumini wao na unaona huo waraka unakukwaza, nadhani una uhuru wa kuhama. Na kabisa kabisa sioni jinsi gani huo waraka unakuwa umetumwa kwa sisi wengine wote, sisi wenyewe ndio tunapigana propaganda na kuanza ku-act kama vile tumetumiwa wananchi wote.
Kama walichowaelekeza watu wale kufanya ni kibaya, then speak it out; sema nini walichoambiwa wafanye ni kibaya au pengine kina athari kwao au kwa jamii nzima.
...
Na hata siku moja sintaomba wala kukubali Bakwata wakae na serikali kuzungumzia mwongozo wa nchi hii kwani sii kazi yao kabisa
Msimamo mzuri!
Mukandara, kuna watu wanaoogopa kwamba karibia nusu ya wapiga kura watafundishwa kufanya kitu sahihi this time round. Na hii haitakua nzuri kwa hawa watu. Nadhani kama BAKWATA na wengine nao wangetoa nyaraka zao za aina hii, na kweli waumini hao wakazifuata, na wapagani nao wakatafuta njia ya kufanya hivyo hivyo, hii nchi inaweza kubadilika ndani ya siku kadhaa tu. Imagine 100% pa wapiga kura wanaenda kufanya kitu sahihi. It doesnt matter much kama wanaenda kufanya kitu sahihi kwa sababu wanadhani wataenda mbinguni, au wanaenda kufanya kitu sahahihi bila hata ya kujua kwamba ni kitu sahihi.