Huyu babu kapitwa na wakati. Haelewi anachozungumza, kwani wabunge wako kwa maslahi ya chama au maslahi ya Wananchi??
Sijui kwanini bado anaongea anatakiwa akapuzike ili angalau awekwe kwenye historia nzuri. Otherwise tutahitaji kupima ubongo wake ili ieleweke kama anaweza kutoa ushauri kwa Taifa muda huu.
Kingunge alipuka
na Rahel Chizoza
Tumegundua nia ya wapinzani ni kutaka kukidhoofisha chama chetu, hawawezi na sisi tumejipanga imara, si tu kwamba wakinawa hawatakula, bali pia hawatakiwi hata kunawa
MKONGWE wa siasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Kingunge Ngombale-Mwiru, amewashangaa viongozi wa chama hicho wanaoiponda serikali kwa madai ya kutetea masilahi ya taifa.
Kingunge alitoa kauli hiyo juzi baada ya kupokea maandamano yaliyoandaliwa na CCM Mkoa wa Dodoma, kwa lengo la kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete kwa hotuba aliyoitoa bungeni mwishoni mwa wiki.
Alisema kila kiongozi aliyepo ndani ya CCM, amepata umaarufu kupitia chama hicho na si kwa juhudi zake binafsi.
Wanaodhani umaarufu walionao umetokana na wao wenyewe, wanajidanganya, hebu wasimame peke yao tuwaone kama wataendelea kuwa maarufu, umaarufu huo ni kwa ajili ya chama chao na madaraka waliyonayo yametokana na chama, alisema Kingunge mbele ya waandamanaji wachache waliojitokeza.
Alisema viongozi wa CCM wanapaswa kuwa makini, vinginevyo watajikuta wakiwasaidia wapinzani katika kukivuruga chama na serikali kwa kisingizio cha kusimamia masilahi ya taifa.
Ingawa hakutaja majina ya wana CCM aliokuwa akiwazungumzia, ni dhahiri mkongwe huyo alikuwa akiwalenga baadhi ya wabunge wa CCM wa aina ya Spika wa Bunge, Samuel Sitta (Urambo Magharibi), Anne Kilango (Same Mashariki), Harrison Mwakyembe (Kyela), Aloyce Kimaro (Vunjo) na Christopher ole Sendeka (Simanjiro), ambao wamekuwa mbele kuikosoa serikali, hasa katika masuala yanayohusu masilahi ya taifa, hususan vita dhidi ya ufisadi.
Kingunge alisema hivi sasa kuna tabia iliyozuka kwa wabunge wa upinzani kuanzisha hoja na kudai si ya upinzani bali ya kitaifa, hali inayosababisha baadhi ya wabunge wa CCM kujiingiza katika kutetea hoja hizo bila kujua kwamba kwa kufanya hivyo, wanakidhoofisha chama chao.
Umezuka mtindo hivi sasa, wapinzani wanaibua hoja ili kuwakamata vizuri CCM, wanasema hoja hii ni ya kitaifa, kwa masilahi ya wananchi, hivyo viongozi wetu wa CCM nao wanajikuta wakiingia katika mijadala hiyo bila kujua kwamba wanachofanya ni kukidhoofisha chama, alisema.
Mkongwe huyo wa siasa alikwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa wapo wana CCM wanaorukia hoja za wapinzani kwamba wanazungumzia masilahi ya taifa bila kujua lengo la wapinzani ni kutaka kuwamaliza kisiasa.
Aliwataka wana CCM kuwa na umoja na kuwataka wanaounga mkono hoja za wapinzani, kuacha kufanya hivyo mara moja.
Umaarufu wa magazetini haufai, ni wa kupita tu, na inapofikia kipindi fulani, hata hayo magazeti yanakusahau, wapo wengi tuliwaona, lakini wako wapi sasa? alihoji Kingunge.
Aliwataka wanaojiingiza kwenye hoja za wapinzani na kuzizungumzia kwa nguvu, watafakari kabla ya kukurupu na wajitahidi kuweka mbele masilahi ya chama chao.
Kingunge aliwataka wana CCM kuwa makini na vyama vya upinzani, kwani si vya kuvibeza.
Wapinzani hawana hoja wala sera za kueleweka, ndiyo maana wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali za kuwarubuni wana CCM kwa kuwataka wachangie hoja zao baada ya kuzipa nguvu na kuziita hoja za kitaifa.
Tumegundua nia ya wapinzani ni kutaka kukidhoofisha chama chetu, hawawezi na sisi tumejipanga imara, si tu kwamba wakinawa hawatakula bali pia hawatakiwi hata kunawa, alisisitiza.
Kuhusu suala la Muungano ambalo limezua mjadala wa muda mrefu na kuhitimishwa na Rais Kikwete katika hotuba yake aliyoitoa bungeni, alisema walioanzisha mazungumzo hayo wana ajenda zao za siri.
Aliwashangaa pia viongozi wa CCM walioingilia kati na kuanza kuzungumzia suala la muungano bila kujua kwamba wanajimaliza wenyewe.
Wanaozungumzia muungano hivi sasa, miaka yote walikuwa wapi kama si kutaka kusababisha vurugu na kutaka kuiyumbisha serikali? alisema Kingunge.
Kingunge anatoa kauli yake, siku chache tu baada ya Spika wa Bunge kutoa matamshi muda mfupi baada ya Rais Kikwete kulihutubia Bunge, ambayo baadhi ya wana CCM wameyatafsiri kuwa yaliyokuwa yakilenga kuikosoa serikali na rais mwenyewe.
Aidha, kauli hiyo ya Kingunge inakuja wakati baadhi ya wabunge wa chama hicho tawala wakiwa mstari wa mbele kuikosoa serikali kwa namna inavyoshughulikia masuala mbalimbali, kama mikataba ya madini na ufisadi wa Richmond na EPA