Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,524
- 13,682
Katika kipindi cha "Je tutafika" cha channel ten, Kingunge ameonyesha masikitiko yake kwa kitendo cha JK kuridhia kuanzishwa kwa mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya kwa sababu CCM haikuwa imejiandaa kwa mabadiliko ya katiba! Kingunge amedai kuwa CCM iliandaa sera za masafa marefu za 2000 - 2010 na 2010 - 2020 ambazo hakuna hata moja ilikuwa na mpango wa kuandika katiba mpya!
Aidha Kingunge ameishangaa Tume kupendekeza serikali tatu katika katiba mpya kwa kuwa haikuwa sehemu ya hadidu za rejea walizopewa Tume ya Warioba!
Kingunge amesema kitendo cha JK kuridhia kuanzishwa kwa mchakato wa kuandika katiba mpya ni surprise kwa CCM kwa kuwa haikuwahi kujadiliwa katika kikao cho chote cha CCM!
Naye Vuai Naibu katibu mkuu wa CCM (Zanzibar) aliyeshiriki katika kipindi hicho amesema kuanzishwa kwa serikali tatu ni pigo kwa Wazanzibari kwa kuwa kwa kiwango kikubwa Wazanzibari wamekuwa wanategemea Tanzania Bara kwa elimu, uchumi na shughuli za kijamii!! Amesema katika muundo wa sasa wa muungano Wazanzibari wamekuwa huru kufanya shughuli zao Tanzania bara bila bugudha zo zote!
Aidha Vuai amelaani slogan ya CUF huko Zanzibar inayosema "Tunataka nchi yetu"
Kingunge na Vuai wote wanadhani kitendo cha Warioba kupendekeza serikali tatu ni kuvunja muungano!
Tutafakari upya hoja zetu za serikali tatu au nne zinazopendekezwa wa Wapemba!!