Kingunge na Kiapo

Kingunge na Kiapo

Chizi Fureshi

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Posts
1,718
Reaction score
461
Wote tunajua kuwa katika BMK zoezi linaloendelea ni la kila mjumbe kuapa mbele ya Mwenyekiti. Hamu yangu ni kumsikia Kingunge Ngombare Mwiru.
 
s%20%28247%29.jpg

Huyu huwa hashiki kitabu chochote cha kunishangaza mwishoni huwa anasema ee Mungu nisaidie sijui ana Mungu wake wa mungu?
 
Kingunge ni Mzee mwenye hekima sana, Mungu ampe maisha marefu.
 
Keshaapa, hakushika kitabu na wala hakusema kuwa "Ee Mwenyezi Mungu nisaidie"!

Ila anaonekana kachoka sana na kavaa viatu vikubwa kumzidi!
 
Fidel80, nimebahatika kumwona akiapa. Hakushika kitabu chochote cha Dini na hajamwomba Mungu amsaidie!
 
Last edited by a moderator:
Alikuwa mjanja tangu zamani hawa wazungu walimkoma kabisa kutuita majina ya kizungu na kiarabu sio fasheni
 
Nami nimemuona huyu mzee kweli ananishangaza maana hajashika kitabu chochote cha dini na hajamtaja hata Mwenyezi Mungu ,
 
Hajatekwa kifikra wala kiimani na hao wazungu au waarabu wenu.
 
unaweza ukawa unamuamini mungu kupitia kwa mizimu ya mababu na sio huwe mkristu au mwislamu ndio uwe na mungu kumbuka dini ni imani ila mungu ni mmoja
 
s%20%28247%29.jpg

Huyu huwa hashiki kitabu chochote cha kunishangaza mwishoni huwa anasema ee Mungu nisaidie sijui ana Mungu wake wa mungu?

Kingunge ni MKATOLIKI na ametoa sehemu ya kiwanja chake kujengwa kanisa..anaitwa HERMAN! hapo atakua anafanya siasa tu!
 
...nashawishika kuwa kunawatu wenye nyadhifa za juu sana serikalini ni wachawi,na wanaloga maendeleo ya nchi,hususan decision makers...
 
Mtikila naye sijui atapaje maana kwenye hicho kiapo ninaona sehemu inayitamka jamhuri ya muungano wa Tanzania wakati yeye anatambua Tanganyika tuu
 
Kingunge ni MKATOLIKI na ametoa sehemu ya kiwanja chake kujengwa kanisa..anaitwa HERMAN! hapo atakua anafanya siasa tu!

kingunge alikuwa Mkatoliki na ameasi. Jina lake la Ubatizo ni Cajetan. Huyo aliyetoa eneo la kujenga Kanisa alikuwa baba yake mkubwa ambaye ndie alikuwa Mkristu wa kwanza Kilwa Kipatimu, na alikuwa Katekista pia. Kaburi lake lipo pembeni mwa ngazi za Kanisa Katoliki Kilwa Kipatimu.
 
Kingunge ni MKATOLIKI na ametoa sehemu ya kiwanja chake kujengwa kanisa..anaitwa HERMAN! hapo atakua anafanya siasa tu!
Atasema, "Ee mungu wa Kinjekitile Ng'wale nisaidie!" Kumbuka huyu ni muwakilishi wa waganga wakienyeji na waabudu mizimu pale Bungeni!
 
Kwa kuwa Kingunge hana dini ndio maana hata yule mtoto wake hakumpa mafundisho mema hadi anajihusisha na Biashara ya Madawa ya Kulevya (Ref. Sakata la Aikina Masogange)
 
Kingunge alipitia masomo ya ukominist ya wakati huo wa cold war, na akaiva sana katika nadharia ya dialectical materialism ambayo mojawapo ya nguzo zake zilikuwa ni kutokuamini kuwepo kwa Mungu. Hiyo ilimsaida sana kwani tangu alipoanza kama mkuu wa mkoa wa Arusha mwishoni mwa miaka ya sitini, hakuwahi kutoka kwenye siasa za ujamaa za wakati huo. Lakini ujamaa uliponyofolewa, hakusema lolote na akabakia katika sistem akiwa undefined. Ni mwanasiasa wa kitanzania kama walivyo wenzake wanaoangalia matumbo yao. Wanasiasa sehemu nyinggi duniani huangalia matumbo yao na imani zao lakini wetu wa Tanzania huangalia matumbo tu.
 
Back
Top Bottom