Kingunge alipitia masomo ya ukominist ya wakati huo wa cold war, na akaiva sana katika nadharia ya dialectical materialism ambayo mojawapo ya nguzo zake zilikuwa ni kutokuamini kuwepo kwa Mungu. Hiyo ilimsaida sana kwani tangu alipoanza kama mkuu wa mkoa wa Arusha mwishoni mwa miaka ya sitini, hakuwahi kutoka kwenye siasa za ujamaa za wakati huo. Lakini ujamaa uliponyofolewa, hakusema lolote na akabakia katika sistem akiwa undefined. Ni mwanasiasa wa kitanzania kama walivyo wenzake wanaoangalia matumbo yao. Wanasiasa sehemu nyinggi duniani huangalia matumbo yao na imani zao lakini wetu wa Tanzania huangalia matumbo tu.