Bakhresa ni Mkurugenzi/CEO muda mwingi anawaza jinsi ya kuendeleza makampuni yake hawezi kuwa na muda wa kutosha kudili na figisufigisu.
Hivi unawajua vizuri watu ambao wanategemea siasa ndio maisha yao yaende wanakuwaje reaction yao pale wanapoona unataka kuwaletea upinzani?waogope sana hao watu huwa hawalali,na ndio maana kuna ule msemo unaosema"Siasa ni mchezo mchafu" huu msemo umebeba maana nzito sana.
Achilia mbali kwenye level za ubunge yaani hata kwenye level za udiwani na mwenyekiti wa mtaa watu wanatumia nguvu nyingi sana aisee usifanye mchezo.
Ngoja nikupe kisa kimoja hivi unaweza ukanielewa ninachokiongea"Kuna jamaa mmoja yeye ni kiongozi/mwenyekiti wa mtaa fulani-Sasa huyu jamaa ana tuhuma ya kuuza kiwanja cha mpira wa miguu ambayo ni kama mali ya umma yaani tangu nimezaliwa mimi kile kiwanja nimekikuta na tulikuwa tunacheza mpira tukiwa wadogo hadi hii leo mimi ni mtu mzima,sasa mwaka jana nimerudi home nikaambiwa kile kiwanja kimeuzwa kwa wawekezaji na nimekuta kweli ile sehemu kumechimbwa misingi na kuna matofali yamelazwa,sasa kutokana na hilo jambo wananchi walichukizwa sana na hicho kitendo wakawa wanatoa minong'ono kumsema vibaya yule jamaa na wakaapa kumpiga chini kwenye uchaguzi ili wapate kiongozi mwingine mzuri.
Basi ikafika siku ya uchaguzi watu wakapiga kura lakini cha ajabu yule jamaa ambaye ameuza kiwanja ameshinda uchaguzi na sasa hivi ni mwenyekiti anaendelea kama kawaida-Siasa mchezo mchafu.