Kinondoni yafunga saluni zinazotoa huduma za masaji na kujichubua ngozi kwa kuwatundikia drip

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imefanya ukaguzi wa saluni kadhaa zinazotoa huduma mbalimbali, ikiwemo huduma za ‘kusinga’, ili kubaini ikiwa zinafuata taratibu za utoaji huduma. Hadi sasa, wamefunga saluni mbili zinazotoa huduma hizo pamoja na urembo wa ngozi kwa sababu walikuwa wakifanya shughuli hizo kinyume cha sheria.

"Watanzania wanakwenda pale wanapotaka kuwa weupe mwili mzima; wanatundikiwa drip, wanatengeneza sura zao na wanataka kubadilika, si masaji kama ilivyoainishwa. Hawana kibali chochote na hawana utaalam huo." – Dkt. Peter Nsanya
Your browser is not able to display this video.
Soma:
+
Saluni za "kuchua" zashamiri Dar
+ Acheni kujichubua
+ Muonekano wa mchezaji wa Senegal Keita Baldé, baada ya kuacha kujichubua
 
Aiseeeee
 
Hizo saluni ni madanguro ya siri
 
"Watanzania wanakwenda pale wanapotaka kuwa weupe mwili mzima; wanatundikiwa drip, wanatengeneza sura zao na wanataka kubadilika, si masaji kama ilivyoainishwa. Hawana kibali chochote na hawana utaalam huo." – Dkt. Peter Nsanya
Hayo madrip yanaingiaje nchini
 
Wacha wale pesa za wajinga wanaojichubua.
Waende sehemu nyingine wakafungue ofisi wapige pesa za wajinga.
Bado wajinga wamejaa tele na pesa wanazo na kudanga wanataka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…