Tom Mabe amewatia hofu na kiwewe huku akiwachekesha maelfu kwa Kinyago chake mithili ya Kishetani au Msukule kinachoruka angani.
Hukirusha kimwanasesere chenye sura ya mfu kwenye bustani zenye watu ambapo watu wakiwapo watoto hutimka ovyo wanapokiona. Utadhani ni flamu ya Dracula vile. Kinaendeshwa kwa umeme kama helikopta huku akitumia remote control kukirusha, kutua na kuvinjari maeneo ya watu wanaostarehe.