Upepo wa siasa za mtaani ulichangamama katikati ya jiji wakati wananchi walipoamua kufanya "uchaguzi wa mtaani" kwa njia ya ucheshi na mzaha. Boxi la kadibodi na vikapu viwili vya plastiki kimoja kikiwa kimeandikwa jina la Sifuna na kingine Ruto vilikuwa ndivyo sanduku za kura za siku hiyo.
Shughuli ilianza pale maafisa wa "IEBC ya mtaani" walipoketi tayari kuhesabu kura zilizopigwa kwa vipande vya makaratasi ya kadibodi.
Vigelegele na kelele za mashabiki zilijaa hewani kila kura ilipotolewa kikapuni. Mchezo huo ulipata msisimko wa kipekee pale kura za Ruto zilipokuwa zikihesabiwa mwanzo kwa sauti kuu, lakini mambo yalibadilika ghafla wakati wa kuhesabu kura za Sifuna.
Mstari wa kura za Sifuna ulionekana kuwa mrefu usio na mwisho! Yule afisa aliyekuwa akihesabu kura hizo al sabaikiliza kila kura kwa sauti na kasi ya ajabu, akizidisha idadi huku umati ukimshangilia kwa vicheko na makofi. Mvutano na uchangamfu uliongezeka kwa kila tarakimu iliyosomwa, hadi ikamfanya muhesabu kura kuchoka kabisa na kuomba maji ya kunywa katikati ya shughuli hiyo, jambo lililozua kicheko kikubwa zaidi miongoni mwa waliohudhuria.
Uchaguzi huo wa mtaani haukuwa tu wa kutafuta mshindi, bali ulikuwa uonyesho wa jinsi Wakenya wanavyoweza kuchukulia masuala mazito ya kisiasa kwa njia ya furaha, ushirikiano na vicheko. Nawe unaona mbinu hii ya mtaani ya kuelezea maoni ya umma inaleta taswira gani kuhusu siasa za sasa?
Source: SsTv