SI KWELI Kinyonga wakati wa uzazi wake hupasuka tumbo na kufariki

SI KWELI Kinyonga wakati wa uzazi wake hupasuka tumbo na kufariki

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Hivi ni kweli kwamba kinyonga akiwa anazaa hupanda juu ya mti na kujirusha chini hali inayopelekea tumbo lake kupasuka na kufariki?

1726213177018.png
 
Tunachokijua
Kinyonga kwa jina la kisayansi wanajulikana kama Chamaeleonidae wapo kwenye kundi la viumbe hai wanaotambaa chini. Kinyonga anakadiriwa kuishi kati ya miezi minne hadi miaka tisa kulingana na aina husika ya kinyonga huku akikadiriwa kuwa na urefu wa kuanzia nchi 0.85 hadi kufikia futi 2.2.

Kuna aina takribani 200 za vinyonga huku aina 76 zikipatikana kwenye visiwa vya madagascar tu. Miongoni mwa sifa za Kinyonga ni uwezo wake wa kubadili rangi.

1726212717164-png.3094759

Kumekuwepo na hoja inayodai kuwa kinyonga jike akizaa hupasuka na kufariki. Hoja hiyo inafafanua kuwa kinyonga anapotaka kuzaa hupanda juu ya mti na kujirusha chini kisha tumbo hupasuka na mtoto kutoka na kisha yeye aliyezaa hufariki hapo hapo. Hoja hii iliyoletwa na Mdau wa JamiiCheck imewahi kuchapishwa na baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii (tazama hapa na hapa)

Ukweli upoje?
JamiiCheck imepitia machapisho na tafiti mbalimbali na kubaini taarifa hizo si za kweli mfano chapisho liliochapishwa na National Geographic kwenye website yao wameeleza kuwa vinyonga wana aina mbili za kuzaliana kulingana na aina husika ya kinyonga.

Ambapo aina nyingi za vinyonga huzaliana kwa njia ya mayai ambapo kinyonga jike hutaga mayai na kuyafukia ardhini, idadi ya mayai hutegemeana pia na aina husika ya kinyonga na baada ya muda mayai hayo hujitotoa.

Lakini pia Shirika la uhifadhi la San Diego Zoo Wild Alliance animals and plants kupitia chapisho lao lililowekwa kwenye tovuti yao wameeleza aina chache za vinyonga zilizobaki mfano kinyonga aina ya Jackson huzaliana kwa njia isiyo ya mayai na badala yake kinyonga jike huzaa watoto walio hai moja kwa moja kama inavyoonekana kwenye video iliyochapishwa kwenye youtube chanel ya BBC earth.

1726212826065-png.3094761

Picha: Kinyonga aina ya Jackson
Back
Top Bottom