JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mahakama ya Wilaya ya Iringa, imemhukumu kinyozi, Batista Ngwale (27) kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumtia hatiani kwa kumpa mimba mwanafunzi mwenye umri wa miaka 18.
Binti huyo alikuwa akisoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kibena iliyopo Iringa Vijijini.
Binti aliiambia Mahakama kuwa alianza uhusiano na Batista, Mei 2021, alipopata ujauzito mtuhumiwa akamwambia atoe lakini binti huyo hakufanya hivyo.
Mashahidi 6 waliohusika katika kesi hiyo akiwemo Daktari wa Kituo cha Afya cha Ifunda.
Video: Azam TV