Kinyozi, mchomeleaji, bodaboda, mama ntilie,n.k. hulaza wastan elfu 10 kwa siku, mhitimu unaeogopa kuchekwa endelea kukaa nyumbani

Kinyozi, mchomeleaji, bodaboda, mama ntilie,n.k. hulaza wastan elfu 10 kwa siku, mhitimu unaeogopa kuchekwa endelea kukaa nyumbani

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
30 paaap !!

"Nina vyeti nitapata ajira", "siwezi fanya kazi nje ya taaluma niliyosomea", n.k. ni jinamizi litalokulalia uchelewe kuanza life lako.

Ajira hizo unazoziota zipo chache sana na connection zimerudi kwa kasi, awamu iliyopita ajira zilisimamiwa na idara ya utumishi angalau kulikuwa na fairness, awamu ya sasa maboss wa taasisi na vitengo wanaweza kujisimamia, hapo wenye kipaumbele ni watoto, watoto wa shangazi, ndugu wa mke, n.k. wewe na gpa yako ya 3.5+ utabaki kushangaa wenzako wenye 2.x wanapenya.

Umemaliza chuo hakuna haja ya kusubiria graduation, itafika na kama huna mishe utarudi nyumbani, anza kupiga mishe zako iwe ni kunyoa, boda, umama ntilie, ususi, kushona, n.k. on average angalau uwe una uwezo wa kujitegemea kuanzia kula, kujivisha, kukodi chumba, n.k.

unapiga mishe zako huku unaendelea kucheza bahati nasibu (kubeti) kuajiriwa, hata ukikosa ajira unaendelea na mishe zako na inaweza kufikia kipindi umepanua biashara zako kiasi kwamba hutamani tena ajira, ni bora kuzidi aliekosa ajira anaanza kujitafuta akiwa kwenye 30s from scratch.

Tatizo linalofanya wahitimu wengi wasifanye kazi hizi ni stereotype ya jamii huziona ni za watu waliofeli shule, wahitimu wanaogopa kuhisi watachekwa na watu wa mitaa waliyokulia, Tiba ya hii hofu ni kuhama sehemu uliyokulia, kama umesoma chuo mkoa mwengine baki huko huko, hii inakupa ujasiri wa kujichanganya na kufanya kazi zako kwa uhuru.

Mfano Dar utakuta vijana wengi wadogo wanakuja kusoma na wakimaliza chuo wanabaki na kuanza kujitafuta, wengi wananyanyuka kiuchumi tofauti na wenzao wazawa wa Dar huwakuti kwenye hizo shughuli, wana ile hofu ya "watanionaje watu tunaojuana kwa muda mrefu hapa Dar ?"

we live once, Try to make a series of wise choices that can increase your probability to have a better life.
 
Hizo mbona ni kazi nzuri!
Tena zikifanywa na mtu mwenye elimu na anayeipenda, kama ni mama ntilie anakua na mgahawa wa kishua

kuna mama ntilie wanafanya mauzo ya milioni 3 kila siku.

ukitoa jumapili ambapo wanapumzika, kwa mwezi wanafanya mauzo ya zaidi ya milioni 60.

tembelea kariakoo utazame tu mauzo ya mama ntilie mtaa wa manyema na mitaa mingineyo

mama ntilie wanakuja kazini na gari kabisa.
 
30 paaap !!

"Nina vyeti nitapata ajira", "siwezi fanya kazi nje ya taaluma niliyosomea", n.k. ni jinamizi litalokulalia uchelewe kuanza life lako.

Ajira hizo unazoziota zipo chache sana, mbaya zaidi ni kwamba connection zimerudi kwa kasi ya 5g, awamu iliyopita ajira nyingi zilisimamiwa na idara ya utumishi, awamu ya sasa maboss wa taasisi na vitengo wanaweza kusimamia zoezi, hapo wenye kipaumbele ni watoto wake, watoto wa shangazi, ndugu wa mke, n.k. utabaki na gpa yako ya 3.5+ nyumbani wakati wenzako wenye 2.x wanapenya.
hivi ushawai kufanya biashara au unafanya biashara za maneno kama wale heka moja ya matikiti ni milioni 5
 
Hujasoma, kama umesoma, ulifeli somo la fikira tunduizi.

Si jambo rahisi mtu aliyesomea udaktari wa binadamu kuacha kutafuta kazi inayomhusu ili awe mama n'tilie.

Ingelikuwa ni kutafuta pesa tu, wasingehangaika huko mashuleni miaka nenda, miaka rudi.

Ninyi watu mliofeli hudhani shida zote za watu huhusisha na kutatuliwa na FEDHA tu. Ndiyo maana mlifeli sababu hamkuweza kufikiri nje ya box!

Hopeless!
 
Shida sio kufanya hizo kazi ila shida ni kwamba wengi wanaofanya hivyo ulivyovitaja ni wale ambao walituacha shule na usikute tuliwabeza iwe moja kwa moja au sio moja kwa moja pia jamii ilitupatia ufalme na kutuona sisi ndio wamaana na tulio na akilli ila hao wengine walishaonekana malooser tayari.

Sasa jaribu kuvaa viatu vya kijana wa namna hiyo ambae mtaa ulimpa ufalme na akaonekana yeye ni mwenye akili na kuonesha ikiwa na matarajio makubwa sana Kwake then arudi na degree yake akaanze kushinda salon moja na kijana ambae alionekana looser baada ya kufeli.

Tafakari hapo kwa uzuri sana then nadhani utapata picha kwamba hawa vijana sio kwamba hawatamani kufanya kazi za namna hiyo ila shida ni kwamba wanahofia jamii ambayo iliwaamini na kuwa na matarajio makubwa juu yao then Kesho iwakute kwenye kazi zile zile ambazo zinafanywa na wale ambao walionekana hawana akili.

Hiki kitu kinawaumiza sana vijana kwenye akili hadi moyo ila wanakua hawana jinsi.

But ili kuwasaidia hawa vijana ni kuwashauri tu kwamba wakishamaliza vyuo wasirudi kwenye maeneo ambayo wamekulia bali watoke na waende wakatafute maisha kwenye mikoa mingine huko hakuna anaewajua kwahiyo watakua na uwezo wakujichanganya na kufanya kazi za aina yoyote ili watafute mitaji ya kuanzisha vya kwao.

Na hii inaonekana kwenye baadhi ya mikoa ambayo nimepata kukaa kwa mfano...

Ukienda Dodoma utakutana na vijana wengi wa bodaboda ni degree holders wale wengi kiasili sio wa mkoa ule ila wameamua kubakia pale waendeleze gurudumu la maisha pia nimeona hata Iringa maeneo ya mkwawa pale bodaboda wengi ni degree holders so wapo ambao wanatoka kwenye comfort zone zao na kujitafutia kilocal katika maeneo ambayo hawajulikani sana ingawa hata maeneo hayo pia wakishajulikana kwamba wako na degree halafu wanafanya hivyo bado wanawashangaa na kuwafanya vijana hawa wakose kujiamini.

Daslam ndio utakuta vijana wengi wanatoka mikoani kuja kusoma na wakimaliza chuo wanaongoza kujitafuta kilocal na wanaongoza kufanya vizuri na wengi wananyanyuka kiuchumi ila hawa ambao ni wazawa wa Dar huwakuti kwenye hizo shughuli kwa maana bado mentality yao iko kwenye watanionaje washkaji niliomaliza nao na kadhalika.
 
Hujasoma, kama umesoma, ulifeli somo la fikira tunduizi.

Si jambo rahisi mtu aliyesomea udaktari wa binadamu kuacha kutafuta kazi inayomhusu ili awe mama n'tilie.

Ingelikuwa ni kutafuta pesa tu, wasingehangaika huko mashuleni miaka nenda, miaka rudi.

Ninyi watu mliofeli hudhani shida zote za watu huhusisha na kutatuliwa na FEDHA tu. Ndiyo maana mlifeli sababu hamkuweza kufikiri nje ya box!

Hopeless!
Wewe umesoma lakini hujaelimika, unaweza kujibu 100 -5 = 95 lakini huwezi kufikiria wahitimu 100 waliosomea udaktari wakiitwa kujaza nafasi 5, ni 95 watakosa
 
Ndio hawa hawa mama ntilie wanaoumizwa na mikopo umiza ya kitaa na vicoba ? Unaongelea kuuza tu haujaongelea chakula kubaki au kuzunguka na kutukanana na watu waliokula kwa kukopa na hawataki kulipa...

Tuache hizi brah brah brah na tuwabane hawa watumishi wetu tunaowalipa waje na sera za kueleweka za watu kupata ujira wa kuweza ku sustain maisha yao mwezi baada ya mwezi na sio kuishi kwa kukopa leo ili ulipe madeni ya mwezi juzi...
 
You need to tell degree holder /graduates to be job oriented and not money oriented.

Unapozungumzia 10k kwa siku

Nikwambie kuna watu wanalaza zaidi ya 10k uliyoandika hapo juu kupitia boda boda.

Watu sio kwamba wanadharau kuendesha boda au kuwa mama ntilie

Itapendeza ikiwa kila MTU atafanya kitu anachopenda na anachokimudu vzr.

Don't be fooled with politics being a bodaboda rider is not a job
 
Back
Top Bottom