Kinywaji cha Mo Extra ni energy drink au siyo?

Kinywaji cha Mo Extra ni energy drink au siyo?

Mo extra Ni kiburudisho sio energy drink ...


Chunguza kwenye Chupa hapo ukiona hata neno lililoandikwa energy,nakupa 200k ....
Angalia kwenye ingredients, utakutana na maneno caffeine na Sugar, Hayo maneno ndo Neno "Enegy" unalosema halipo, wanacheza na akili za wajinga na wanafanikiwa.
 
Energy drink ina sifa kuu ya kuleta nguvu na uchangamfu haraka kutokana na viungo vyake kama caffeine na sukari. Viungo hivi viwili ndiyo Msingi mkuu wa Kinywaji chochote cha Energy Drink.

Sasa twende kwenye Mo Extra ambayo kimsingi watu wanaiita kuwa ni Soft Drink. Pia katika chapa yake Imepewa jina hilo.
Ili kupata majibu ya swali hili tunatakiwa kutizama Viungo vinavyotumika kupata Ladha kamili ya kinywaji hiki, ambapo Sugar pamoja na Caffeine Vimeandikwa wazi kuwa vimewekwa.

Hiyo kwa uelewa wangu nitaiita Mo Extra ni Energy Drink kwa sababu ina Caffeine na Sugar.
Nimeambatanisha na picha View attachment 2936981
 
Back
Top Bottom