kinywaji chetu pendwa grandmalt kimeingiliwa na viwanda bubu ? kwanini za elf 2 zipo ofauti na za 2.500

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760


Bei ya Grand malt iliyozoeleka ni elf 2 na mia tano lakini sikuhizi kuna maduka unapata kwa elf 2

Nilianza kununua za elf 2, Sijajua kama koo na ulimi wangu vina matatizo lakini nahisi kuna vitu vimepungua kuanzia ladha, ubaridi, gesi, jinsi inavyopita kwenye koo, n.k.

Nimeanzisha uzi huu kwasababu leo nimerejaribu kununua ya 2,500 nimeinywa na kuridhika
 
Watakuwa washaanza kufyatua feki yao kama kwenye pombe za bei kubwa
 
View attachment 3144491

Bei ya Grand malt iliyozoeleka ni elf 2 na mia tano lakini sikuhizi kuna maduka unapata kwa elf 2

Nilianza kununua za elf 2, Sijajua kama koo na ulimi wangu vina matatizo lakini nahisi kuba vitu vimepungua
Kiwanda changu cha Nongwa enterprises and liquor store tunafyatua hizo. Tuko hapahapa kimara temboni
 
Nilidhani ni mimi mwenyewe kumbe na wengine wameona. moja ina ladha ya sukari zaidi nyingine kama ina uchungu kwa mbali....na hii ilianza kuna miezi kadhaa hapo nyuma zilipotea kabisa alafu zilipoanza kuja ndyo zikawa tofauti
 
Soon tutarudi kwenye togwa tu
 
Nafikiri kwa sasa turudi kwenye minazi na ulanzi ndo asili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…