Kinywaji gani chenye kilevi kinamfaa mwenye kisukari?

Kinywaji gani chenye kilevi kinamfaa mwenye kisukari?

bigmash

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
416
Reaction score
421
Wadau,
Najua humu kuna wajuzi. Mimi ni mnywaji sana wa hivi vinywaji vyenye vilevi (alcohol), lakini leo nilienda kupima sukari na Bp, sukari yangu imeonekana ipo juu na inakaribia kufikia kiwango cha kuitwa mgonjwa wa kisukari, Bp pia ipo juu zaidi. Moja ya maelekezo niliyopewa na doctor ni kupunguza unywaji wa pombe na ikiwezekana niache kabisa, pamoja na mazoezi na ulaji mlo kamili na kupunguza kula. Sasa swali langu ni kinywaji gani naweza tumia ili isiharibu usawa wa sukari yangu?
 
Serengeti brother, ndio kinywaji kinachoshauriwa kwa wenye kisukari!!
 
Serengeti brother, ndio kinywaji kinachoshauriwa kwa wenye kisukari!!
Nashukuru Sana, lakini sina uhakika Sana Kama Serengeti haina sukari japo nilishasikia hili.
 
Kisukukari na presha ni magonjwa yanayoongoza kutuua wanaume. Kitakachofuatia hapo ni heart attack au stroke.

Ningekuwa wewe ningezingatia ushauri wa daktari na kupumzika pombe kwanza mpaka mambo yatakapotengamaa. Sukari na calories za kwenye pombe hazina manufaa yo yote katika mwili wako. Afadhali upate sukari kutoka katika vyakula utakavyokuwa unakula.

Ingia google uangalie diabetic foods na uzingatie kwa makini. Mkuu ukiwa full diabetic na blood pressure juu ni matatizo makubwa na likely hata nguvu za kiume utazisikia kwenye mabango ya waganga wa kienyeji tu. Please usifanyie suala hili utani. Kila la heri!!!
 
Piga Freixnet mkuu...sukari full kushuka mpaka 0 rt
 
Kuna coke zero, kwa alcohol labda wine kiasi. Lakini beer na soda zingine zote si rafiki kwako
 
Maji ndicho kinywaji pekee kinachomfaa mgonjwa wa sukari. viwaji vungine bora ukaachana navyo vitapunga muda wako wa kuishi.
 
Back
Top Bottom