POTOSHI kiongozi amepata ajali 14/01/2026 na hii ndiyo picha ya gari lililopata ajali

POTOSHI kiongozi amepata ajali 14/01/2026 na hii ndiyo picha ya gari lililopata ajali

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Wakuu nimekutana na hii Post huko Facebook ikiwa na ujumbe huu pamoja na picha.

👉
😀
😀
Sasa mbona hii ajali hamtangazi na imetokea toka jana jioni!
👉
Tuseme mpaka sisi #KigogoMedia tutangaze ndio nanyie mtatangaza?mtu kateuliwa juzi akaanza na kaul za kutisha watu sasa aendelee kutisha watu.
Msipotangaza mpaka saa 7 mchana nitakuja hadharani na taarifa yote.
1768539092631.png

Potoshi Ajali Jan 16.jpg
 
Tunachokijua
Kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, mtumiaji mmoja alichapisha taarifa Januari 15, 2026 akiambatanisha na picha ya gari lililopata ajali na kueleza kuwa ni ajali ya kiongozi mkubwa iliyotokea jioni ya Januari 14, 2026.

Uhalisia wa Taarifa hiyo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejirirdhisha kuwa hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha picha hiyo.

Picha iliyotumika pia si ya mwaka 2026 kama inavyodaiwa, kwa kutumia Google reverse image search imebainika kuwa picha hiyo ni mwaka 2023 ambapo ilichapishwa katika vyanzo mbalimbali vya taarifa.
1768544202251-png.3530392

Picha hiyo ilipochapishwa mwaka 2023 ilielezwa kuwa ni gari ya aliyekuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI, Festo Dugange ambaye alipata ajali huko Dodoma akiwa na gari hiyo ambayo alikuwa akiiendesha yeye mwenyewe.

Taarifa ya Polisi ilieleza kuwa ajali hiyo ilitokea 26/04/2023 katika barabara ya Iyumbu, wilaya na jiji la Dodoma, ambapo Naibu waziri huyo alipata majeraha kadhaa. Hivyo picha hiyo kutumika mwaka 2026 ni kupotosha uhalisia.
Back
Top Bottom