wazanaki
JF-Expert Member
- Mar 20, 2020
- 1,092
- 808
Wakuu Leo naomba tupate elimu kidogo kwenye mada inayohusu nidhamu ya uongozi na wajibu.
Kwenye nchi zetu za Kiafrika viongozi huwa wanajisahau sana wanapofika kwenye nafasi za uongozi kutokana ulimbukeni wa madaraka na mali na kusahau jukumu la uongozi.
Kiongozi wa taifa inatakiwa afanye majukumu yake kama anavofanya refa katika mchezo wa mpira. Unapokua na taifa unakua umechukua dhamana ya watu zaidi ya milioni unatakiwa uwe makini sana.
Jukumu kubwa la kiongozi yoyote duniani ni kusimamia haki za wananchi na kuhakikisha analinda malighafi za wananchi. Hii ndo kazi kuu kubwa ya msingi. "Haki"
Ni kama refa uwanjani. Refa hatakiwi kupendelea upande mmoja tu. Pia refa hatakiwi kucheza mpira. Lakini kwa baadhi ya viongozi wengi wa afrika wanacheza mpira na kupendelea upande wao mmoja. Refa akisimamia mechi vizuri na kwa haki. Mechi inakua na ubora.
Hata siku moja tusije kufikiria raisi yuko pale kushika nyundo na jembe kufanya kazi. Maendeleo yanaletwa na wananchi wenyewe. Barabara zote na madaraja, usafiri, kilimo vinafanywa na wananchi. Ila utasikia mtu anasema raisi kafanya.
Wananchi siku zote wataendelea na shughuli zao za kila siku hata kama raisi hayupo. Ila raisi anasifiwa zaidi kwa kusimamia haki na mipango ya maendeleo iishe kwa wakati.
Shughuli yake ya usimamizi wa haki isipotoshwe na utendaji wa kazi wa wananchi wenyewe. Kila kitu kinafanywa na wananchi.
Wananchi wanachohitaji kwa kiongozi ni usimamizi wa haki na mali zao (madini, rasilimali watu, mbuga...nk) kwa kutumia katiba na katiba italindwa na jeshi la wananchi. Na jeshi la wananchi litalindwa na katiba.