Kiongozi HAMAS apongeza msimamo uliooneshwa na Russia na China katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Kiongozi HAMAS apongeza msimamo uliooneshwa na Russia na China katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
6,846
Reaction score
10,288
Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amepongeza msimamo ulioonyeshwa na Russia na China katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na hatua hayo ya kulipigia kura ya turufu azimio lililopendekezwa na Marekani la kuuunga mkono utawala vamizi wa Kizayuni unaokalia ardhi kwa mabavu.

Kwa mujibu wa IRNA, Ismail Haniyah ameeleza katika taarifa maalumu aliyotoa, akizipongeza na kuzishukuru pia nchi zote wanachama na zisizo wanachama wa Baraza la Usalama ambazo zimetaka kusitishwa mara moja mashambulizi na jinai dhidi ya watu wa Gaza.

Aidha, Haniyah ameitaka Jamii ya Kimataifa iulazimishe utawala wa Kizayuni uheshimu haki za binadamu na kutekeleza sheria na maazimio ya kimataifa na ya kibinadamu kwa ajili ya haki za wananchi wa Palestina hususan watu wa Gaza.

Russia na China zimelipigia kura ya veto azimio lililopendekezwa na Marekani kuhusiana na Gaza katika Baraza la Usalama, ambalo lilikuwa linaupendelea utawala wa Kizayuni.
 
Back
Top Bottom