rodgers123
Senior Member
- Jul 12, 2015
- 180
- 152
Ndugu zangu ICC inaendelea kuwawajibisha wale wote wanaoshiriki
mauaji, unyanyasaji na adha zingine za ukiukaji wa haki za binadamu.
-------------------------------------------------
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imemhukumu Ali Muhammad Ali Abd-Al-Rahman (Ali Kushayb) kifungo cha miaka 20 jela kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu uliotekelezwa Darfur mnamo 2003–2004.
Kushayb, mmoja wa viongozi wa Janjaweed, alihukumiwa kwa kuamuru na kushiriki mauaji, ubakaji, na mashambulizi dhidi ya makabila yasiyo ya Kiarabu. Ni mtu wa kwanza kufikishwa ICC kwa uhalifu wa Darfur.
Kesi yake imekuja wakati Darfur ikikumbwa tena na ukatili katika vita vya sasa kati ya jeshi la Sudan na RSF, kundi lililotokana na Janjaweed.
Licha ya hukumu hii, ICC bado inasubiri kukamatwa kwa watuhumiwa wengine, akiwemo rais wa zamani Omar al-Bashir, anayekabiliwa na tuhuma za mauaji ya kimbari.
1)Je miaka 20 aliyopewa jamaa wa Sudan ni adhabu ndogo sana ukilinganisha na uhai wa binadamu..?
2)Je nani atawajibishwa kwa yaliyoendelea Tanzania ?
3)Je ni aliye halalisha watu wauliwe ?
Toa maoni yako.