Kiongozi mwema Sayyid Khalifa bin Haroub 1879 - 1960

Kiongozi mwema Sayyid Khalifa bin Haroub 1879 - 1960

Utangulizi

Wapenzi wasomaji nimekuta ujumbe huu katika group moja katika Whatsapp na nimeupenda. Nimeona niuweke hapa kwa faida yetu sote. Ndani ya ujumbe huu kuna mengi ya kuzingatia na pia kushukuru kuwa leo tunaweza tukawakumbuka masultani waliotawala Zanzibar kwa kheri na kisha tukawaombe dua kwa Allah.

RcrMs6-xDoCSi7-rY-b99xCk9QYVJ5nnkLwsiaXy3FYLUR49ZuIHHvmCcYOhAuCzL4DTDMfKs3O4r3Y1kM97OUXtvYy_W73KPIoH9sLKxER8FIRLnbOzZfjihpS3ezKVUVIVzK1QFQMrFeDurbH7FvIu1nP0LYFuFy0ulPm4megyg4MRu9DeAczxnGvuudxeXfM7DLKhWPnWUg37Ucw9oj6OahEZjIw4GT0w5G_cKlgU-lEKf9x2sEcP73SJeqOdEt9S1TxdV89bPnit88cyttXbfvVEnh7M6zj8LKwLcjHTO1TKymrxXvsmU06O3bWPBo53Sk2cxpj7aQ8jtwkss68Yd3ZyQvlBpRdnOD5YPGtwOANnCZWym7jKUYcOZjnxaiE20f3c16AMJ-qiSc128KmRLmcoXDm35lxfbL0tfOYvCAViDw4vh_2XTM8UAylRyWIieyFMc018zFAY5Q87nOMu6_KGCKsSSWhX1zhkju6GPR-bchQ_J6rVCWfgnC-B37RMEqaplEHxyYF8osjIv_hdtyNrjy4PCUhTKmHjq-vs-3YZbdyxHgWY4VlnPVjEKLJzKY4U-QMhfskfM-NHmGbq_nrbt3qCq9MyZI2HdLsyrRNq0Q=w1231-h692-no

Maziko ya Sultan Sayyid Khalifa bin Haroub

Haya ni mazishi ya Mfalme wa Zanzibar Sayyid Khalifa bin Haroub Albusaidy aliyefariki 1960 alitawala muda wa miaka 49 ilibakia mwaka mmoja tu afanyiwe Diamond Jubilee.

Alikuwa Mfalme mpole mwenye huruma akiwapenda sana wananchi wake akiwatembelea kwa miguu na akiwahi kuwaamkia kabla yeye hajaamkiwa akipita pahala watu wote husimama kwa kumlahiki kwa furaha kubwa wakati anasalimiana nao.

Alipokuwa Uingereza aliulizwa, "Je nchini kwako kuna siasa za vyama vingi vinavyoshindana si huenda wale wakagombana wasiwafikiane?

Akajibu, "Habana hawa ni ndugu hawagombani wanazungumza tu maendeleo ya nchi yao watawafikiana."

Alikuwa hapendi ugomvi wala mivutano, alipenda kuona watu wake wanaishi kwa raha.

Siku za Maulidi ya Mtume SAW watu wa Maulidi ya Home na dhikri wa mashamba wakifika Forodhani Sultan Palace wakimsomea maulidi na dhikri na yeye akiwapikia biriani nzuri sana na sharbati ikisha akishuka na marashi akitia marashi kwa mkono wake kisha akiwatunza pesa na Ahli dhikri na Ahlul Maulidi wakifurahi kwa taadhima na heshima hiyo kubwa wanayopewa na Sayyid Sultan.

Allah amuweke peponi pamoja na Mtume wetu Muhammad SAW na Allah atupe baraka zake na madad yake na Allah aijalie Zanzibar iwe nchi ya amani upendo huruma na mshikamano baina ya wananchi wake na viongozi wao Amin Amin.
Mzee MS naomba nikuulize kitu nisicho kijua hivi hawa watu wanaoitwa wakoloni waliotawala hizi nchi za kiafrika ikiwemo hii znz waliruhusu siasa za vya vingi ktk nchi walizo zitwala kwa wakati wanatawala?
Nakama waliruhusu ni nchi zipi hizo?
Na kama waliruhusu mfumo wa vyama vingi kama ingetokea chama fulani kushinda amcho kingekuwa chama cha wanaotawaliwa je ingekuwa ndio mwisho wa wakoloni kuitawala nchi hiyo?
 
Wazungu wa America waliwauwa na kuwafanya watumwa waafrika 180 million. Vipi na wazungu wanawapenda waafrika?[emoji15]
Sikusema chochote kuhusu mzungu infact ndiyo watu ninaowachukia to thé max
 
Kwa kweli binadamu yoyote yule anayemdhalilisha, kubaka, kumnajisi, kumuuwa na kumtumikisha binadamu mwenzake kwa macho yangu hafai hata kidogo kuheshimiwa wala kuenziwa, sawa historia iwepo kuwa yalifanyika haya, ila kuanza kumuenzi kama alikuwa mpenda haki wakati minyororo, damu yao waliochanganya na mashimo ya kuwahifadhi wenzake wenzake yapo na yanaonekana?! Hapo hapana, awe mzungu, mwarabu, mweusi au wanjano, mbona histioria za waarabu na wazungu zipo makumbusho?! Kuna haja ya kweli kuwasifia hawa wakoloni wawe wa kizungu au kiarabu kweli?! Bado tuna safari ndefu kwa kweli, tumesamehe ila hatujasahau...
 
Seyyid Khalifa ndie aliepiga marufuku biashara ya utumwa
Ni yeye ndio alioijenga himaya ya Zanzibar kiuchumi na kidiplomasia
Alianzisha uhusiano na USA , Germany , Uk
Ni yeye ndio alitilia mkazo zao la karafuu na nazi....
Ni wakati wake ndio bandari ya zanzibar ilikua free trade na kituo kikubwa cha meli zote zipitazo bahari ya hindi
Ni wakati wake ambapo Elimu ilipewa upendeleo na kufanywa ni kitu muhimu kwa Wazanzibari...walishindana kosoma na kujielimisha. Mashule makubwa ya kisasa yalijengwa ikiwamo shule za King George IV sasa lumumba,
Tumekuja Shool
Bint Matuta school, sasa Benbella
Haille salalsie school
dajarani school
Vikokotoni school
Mkunazini school
Sunni madrassa
Forodhani school
Vikokotoni school
Hamamni school
Kajificheni school
Zanzibar tech school sasa Karume
Kwa Upande wa Pemba
Utaani school former wete boys
Mitiulaya school former wete girls
Jadida school
madungu school
Ngambwa school
Chake chake tech school sasa fidel castro..
Pia ni wakati wake alihakikisha wanafunzi wa Zanzibar wanapata nafasi za kutosha kwenda Makerere University ambayo ndio only University kwa East Afrika...Kina Aboud Jumbe, Ali Hassan Mwinyi wote walifaidika...Seyyid Khalifa aliitembelea Makerere na kuchangia katika ujenzi wa maabara na msikiti mkubwa uliopo hapo.
Upande wa afya ndio ilijengwz hii hospital kubwa ya Mnazi mmoja, wasamaria wema waliijenga hii baada ya ushauri wa Seyyid Kahalifa
Pia alijenga hospital kubwa ya kina mama ya mwembeladu
Hspital ya wete pemba na chake chake
Aloyafanya Kiongozi huyu ni makubwa na ameacha legacy kubwa ambayo hakuna mpaka sasa ambaye amekuja kuyavunja..
Upande wa elimu tulichofanya ni kubadilisha majina ya shule na afys pia.
Kuanzia 64 mpaka 1972 hakuna mwanafunzi alokwenda Makerere wala UDSM...Miaka 8 bila ya kusomesha raia wako ni sawa na kuliua taifa kabisa kabisa...
Upande wa siasa kama alivo eleza sheikh Mohamed Said ni wakati wake mfumo wa vyama vingi ulianzishwa....ni wakati wake katiba ya zanzibar ilijadiliwa na kukubaliwa na vyama vyote....
Huwezi kuitaja Zanzibar bila Seyyid Khalifa....
 
Kweli kabisa, its absolutely nonsense, si kweli kwamba alikuwa mwema, sababu bado alikuwa na watumwa wa kuwatumikisha na kuwafanya chochote atakacho, yeye na wenzake, pia si kweli yeye ndiye aliyepiga vita biashara ya utumwa, yeye aliendeleza upigaji vita biashara ya utumwa, na kama isingekuwa mahasimu wenzao wa kizungu, sidhani kama waarabu wangeacha, anaelezwa kujenga miundo mbini hasa Zanzibar ni Sheikh Barghash bin Said Al-Busaid, huyu Sheikh Khalifa I bin Said Al-Busaid, anaelezwa kuendeleza ya mwenzake nyuma. Sasa wema unaousema kaufanya baada ya kuja kwenye nchi ya watu na kuwatawala bila idhini yao sijuwi na sielewi ni wema wa aina gani?! Unashangaza kabisa, ni kama leo tuseme tuliwakaribisha wajerumani na waingereza eti waje kututawala na tuwashukuru kwa wema wao?! Ni upuuzi na ujinga usio kifani! Kumbuka utawala wa kizungu na kisultani waliondolewa kwa nguvu na sio vinginevyo, wakatili kabisa...
 
Kwani kuna wazanzibari walofanywa watumwa.....wewe uliwahi kusikia mtumwa wa kitumbatu ? Au wa donge au makunduchi au wa pemba ?
Yey hakua mgeni alizaliwa hapona kukulia hapo ni kwao....hakua mkoloni....mkoloni alikua muingereza...yeye alikua kwao....
Alitenda mengi mazuri.
Hakuua mzanizbari hata mmoja
Wala hakufunga raia zake
Ria wote walikua sawa...alikua mwema kweli.....alipandisha zanzibar mpaka ikawa himaya , Empire...ilikua nchi , ikiheshimika dunia nzima
Ni zanzibar ilotoa wanazuoni wakubwa chini yake.... alipo ondoka dunaini misingi yake ni Zanzibar kuwa Mwanachama wa UN na commonwealth....nchi huru kabisa.....
Wakaja walokuja wavamizi wakaweka vibaraka wao , waka iuza nchi ...ikawa mkoa....
Huwezi kumlinganisha kabisa mzalendo huyu aloipenda nchi yake na watu wake na wauza nchi kwa vyeo...
 
Wote hao WAARABU, WAZUNGU, wahindi, wachina etc kwa ujumla wao watu weupe siyo wazuri kwetu waafrica.
Walitumia udhaifu kiuchumi na kielimu wa mababu na mabibi zetu kutudhalilisha na kisha kutuaminisha vya kwao na kusema vya kwetu ni vya kikafiri na sisi kwa unyonge wetu tumekuwa WATUMWA.

Hakuna mtawala yeyote mweupe alimfikira mwafrika kama naye anastahili. Mbaya zaidi wenzetu waliopokea madaraka kutoka kwao nao badala ya kuwatumikia waafrika wenzao nao wanawawazia hao weupe kwa kuwapa raslimali zetu bure kwa mikataba inayoinyonga nchi
 
Kwani kuna wazanzibari walofanywa watumwa.....wewe uliwahi kusikia mtumwa wa kitumbatu ? Au wa donge au makunduchi au wa pemba ?
Yey hakua mgeni alizaliwa hapona kukulia hapo ni kwao....hakua mkoloni....mkoloni alikua muingereza...yeye alikua kwao....
Alitenda mengi mazuri.
Hakuua mzanizbari hata mmoja
Wala hakufunga raia zake
Ria wote walikua sawa...alikua mwema kweli.....alipandisha zanzibar mpaka ikawa himaya , Empire...ilikua nchi , ikiheshimika dunia nzima
Ni zanzibar ilotoa wanazuoni wakubwa chini yake.... alipo ondoka dunaini misingi yake ni Zanzibar kuwa Mwanachama wa UN na commonwealth....nchi huru kabisa.....
Wakaja walokuja wavamizi wakaweka vibaraka wao , waka iuza nchi ...ikawa mkoa....
Huwezi kumlinganisha kabisa mzalendo huyu aloipenda nchi yake na watu wake na wauza nchi kwa vyeo...
Ndo maana mnafeli sana mitihani ya NECTA. Haya mambo hayaki hasira !!!
 
Sahim1,
Swali linaeleweka vizuri likiulizwa kwa kuzingatia mipaka yaani,
"demarcation. "

Swali lako limekuwa, "general," inakuwa shida sana kulipa jibu
la kueleweka.

Hii mada inahusu historia ya Zanzibar na utawala wa Sayyid

Khalifa
.
Hebu liulize upya ukizingatia hayo niloyokugusia.
 
Kaka Mohamed Said , hivi kabla ya hao Waarabu na Masultan wao, Zanzibar haikuwa Dola ya watu weusi wanaojitawala?, hao Waarabu walipofika Zanzibara hawakukuta watu hapo? Kulikuwa hakuna uongozi?, wewe ni bingwa wa kupigania Historia "zilizofichwa" iweje Historia ya Zanzibar ianzie kwenye utawala wa Kiarabu?
 
Sikusema chochote kuhusu mzungu infact ndiyo watu ninaowachukia to thé max
Ze Farmer,
Chuki katika ni katika maradhi mbaya sana ya nafsi.

Chuki hudhoofisha ubongo kwa kasi ya ajabu sana
na huathiri maungo.

Kubwa na baya sana ni kuwa chuki huua fikra nzuri
na kukijaza kifua na joto la ghadhabu.

Mwenye ghadhabu hasemi ila la shari.
 
Ze Farmer,
Chuki katika ni katika maradhi mbaya sana ya nafsi.

Chuki hudhoofisha ubongo kwa kasi ya ajabu sana na huathiri maungo.

Kubwa na baya sana ni kuwa chuki huua fikra nzuri na kukijaza kifua na joto la ghadhabu.

Mwenye ghadhabu hasemi ila la shari.

Hivi chuki ulionayo kwa binadamu wasio waislamu huioni?Tena ndio mbaya sana...

Chuki za wenzako unaziona vizuri,zako huzioni,wewe ni perfect kabisaa....nicheke mie [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kaka Mohamed Said , hivi kabla ya hao Waarabu na Masultan wao, Zanzibar haikuwa Dola ya watu weusi wanaojitawala?, hao Waarabu walipofika Zanzibara hawakukuta watu hapo? Kulikuwa hakuna uongozi?, wewe ni bingwa wa kupigania Historia "zilizofichwa" iweje Historia ya Zanzibar ianzie kwenye utawala wa Kiarabu?

Mohamed Said jibu hili...tena kwa ufasaha kabisa,usifiche kitu wala usimung'unye kitu..
 
Kwa kweli binadamu yoyote yule anayemdhalilisha, kubaka, kumnajisi, kumuuwa na kumtumikisha binadamu mwenzake kwa macho yangu hafai hata kidogo kuheshimiwa wala kuenziwa, sawa historia iwepo kuwa yalifanyika haya, ila kuanza kumuenzi kama alikuwa mpenda haki wakati minyororo, damu yao waliochanganya na mashimo ya kuwahifadhi wenzake wenzake yapo na yanaonekana?! Hapo hapana, awe mzungu, mwarabu, mweusi au wanjano, mbona histioria za waarabu na wazungu zipo makumbusho?! Kuna haja ya kweli kuwasifia hawa wakoloni wawe wa kizungu au kiarabu kweli?! Bado tuna safari ndefu kwa kweli, tumesamehe ila hatujasahau...
Jebs2002,
Ikiwa hayo usemayo unakusudia Zanzibar ukipenda tunaweza tukafanya
mnakasha kwa faida ya wote.

Zanzibar hakuna Sultani aliyepatapo kuua wala kuweka jela ya mateso.
Mauaji na jela za mateso zilikuja baada ya mapinduzi mwaka wa 1964.

Kuhusu suala la ukoloni katika Zanzibar ni muhimu ukaijua historia ya
Uingereza katika visiwa hivyo na uhusiano uliokuwapo kati ya sultani na
Muingereza.

Isome historia ya Zanzibar utaujua ukweli.
 
Ndo maana mnafeli sana mitihani ya NECTA. Haya mambo hayaki hasira !!!
Maringeni,
Haya ya kufeli mitihani na jibu ulilopewa lina uhusiano gani?
Ikiwa unadhani upo uhusiano itapendeza kutufafanulia.

Wala hapakuwa na hasira katika jibu alokupa nduguyo.

Lakini ikiwa unataka kujua kiwango cha elimu ya Zanzibar
kabla ya mapinduzi jibu ni kuwa kilikuwa kiwango cha juu
sana.

Elimu iliporomoka baada ya mapinduzi.
Ukipenda tunaweza tukajadili hili pia.
 
Sahim1,
Swali linaeleweka vizuri likiulizwa kwa kuzingatia mipaka yaani, "demarcation. "

Swali lako limekuwa, "general," inakuwa shida kulipa jibu la kueleweka.

Hii mada inahusu historia ya Zanzibar na utawala wa Sayyid Khalifa.

Hebu liulize upya ukizingatia hayo niloyokugusia.
Wakati wa utawala wa sayyid khalifa je kulikuwa na vyama vingapi vya siasa?
 
Hivi chuki ulionayo kwa binadamu wasio waislamu huioni?Tena ndio mbaya sana...

Chuki za wenzako unaziona vizuri,zako huzioni,wewe ni perfect kabisaa....nicheke mie [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Lebron,
Lete ushahidi kuwa nina chuki na wasio Waislam ili nijitetee.
 
Wakati wa utawala wa sayyid khalifa je kulikuwa na vyama vingapi vya siasa?
Sahim1,
Utafanyaje mjadala ikiwa hata somo lenyewe hulijui?

Sayyid Khalifa katawala kutoka 1911 - 1960.
Hujui siasa za vyama vilianza lini Zanzibar?

Kasome kwanza historia ya Zanzibar ndipo urejee hapa kwenye mjadala.
 
Back
Top Bottom