Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Namwambia rafiki yangu mpita njia kwamba zama zimebadilika, malaika anaetawala sasa ni malaika wa kheri. Watu wanaenda wapendako na wanalala wanapotaka wao. Enzi za kumiliki vikosi na magenge ya wahuni zimepita, hazipo tena.
Nakwambia wewe rafiki yangu mpita njia kwamba, zama za kutishia watu bastola ama kumiminia watu risasi zimesahaulika, kwa sasa tunaendelea kuuguza na kuganga vidonda vya walioumizwa.
Nikupe taarifa tu kwamba, mpaka sasa bado kuna watu wanavilema vya maisha, na wengine hatujui waliko. Familia zao mpaka hazielewi kama waliuwawa au walifukiwa wakiwa hai, au ama walitupwa baharini.
Karibu sana mjini, mji unasisimka kwa hofu, sio furaha tena. Usione wanakenua meno ukajua wanafuraha, hapana, wana maumivu makali sana. Sijajua wale walioporwa ardhi na minyukano iliyokuwa inasimamiwa na kinjekitile ngwale enzi za mkwawa?
Tafadhali ukishika mic kwa mara ya kwanza omba msamaha, wala usione aibu. Uungwana ni vitendo, hata mbingu zitakuelewa sana! Rip all innocent.