Kiongozi shupavu haogopi ushindani, kuwajibika na kukubali ukosoaji

PLOII

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2013
Posts
1,126
Reaction score
849

Niende kwenye Mada Kwa ufupi Sana,

Nimewaza mengi lakini kubwa huenda Wazee wetu walioasisi hili Taifa letu (Tanganyika) hakuwa JASIRI kama ambavyo tunawasoma kwenye historia.

Kiongozi shupavu haogopi ushindani, kuwajibika na kukubali ukosoaji mfano tangu tupate UHURU wa Nchi yetu wakosoaji wengi walipitia nyakati ngumu akina Christopher Tumbo wakapewa vyeo nje ya Nchi (Uingereza) Lengo kunyamazisha Upinzani(iwapo baadae aliachana na hiyo nafasi na kurudi nyumbani kuendeleza MAPAMBANO) na wengine akina Bi. Titi wakafungwa Kwa kosa la uhaini pia wengine wakawekwa kizuizini (Detention) kama Tuntameke Sanga (Msomi huyu) hiyo ndio historia ya watangulizi wetu.
(
Kulingana na Uchanga wetu hasa tukiwa Moja ya Nchi iliyojitoa kusaidia na kuleta ukombozi kulikuwa na maana ya kuwa na uongozi wa namna hii plus Siasa ya Vita baridi (COLD WAR POLITICS) lakini ni lazima tukubali kuwa Changamoto za siasa za vita baridi hazijaisha Kwa hiyo umakini katika kusimamia Itikadi ya Nchi yetu ni muhimu maana Karne hii ni rahisi kupewa kiongozi mweusi mwenye Roho ya kizungu)

Watangulizi wetu waliandaa Katiba ya Leo ambayo kwetu inaonekana inaminya Demokrasia pia walianzisha mfumo wa uongozi ambao hadi Leo tunae Mama yetu kipenzi Samia na huo mfumo haujabadilika bali wamebadilika watu Kwa maana kuna vijana wamezaliwa kwenye uso wa Nchi yetu (Tanganyika) natumia neno Tanganyika Kwa sababu watu wa upande wa visiwani Wana tabia tofauti kabisa na ni waungwana Madhira Yao yote ni influence ya Tanganyika (refer General election 2015).

Hadithi zote za kiutawala na uongozi zinawekwa kuwa Siri, kuwa ni Jambo la Usalama wa Taifa na hapa ndio kiini macho kinaanzia. Shujaa pekee ni Yule atakayekuja akafungua yaliyomo huko ndani maana yale ya historia wengi tunayajua.

Humphrey Polepole hakuja na Jambo jipya bado ana tabia zile zile za kale kuficha ficha mambo tunayohitaji kujua, Kijana kaja na historia yake ambayo sio hitaji la wengi wetu mfano Mimi binafsi ningependa kama angesema Kwa uwazi hao "WAHUNI" waliotaka kuchakachua uchaguzi wa 2015 na mchakato wa Katiba 2014. Huyu kijana nilitegemea aseme Nani anaongoza na kutoa maelekezo katika Nchi yetu maana anasema
"
kama nyumba haina mwenyewe"
Anasema kuna kikundi kina nguvu na anawajua wahusika basi wataje ndio mambo tunataka lakini kaishia kusema historia na kutumia codes of which most of us we are very aware of it.

Humphrey cannot be compared with Nape na Mkapa na wengine Kwa sababu Rais wetu huyu 1995-2005 aliwahi kusema kupitia kitabu chake "
CCM tulichukuwa pesa za Serikali Kwa ajili ya kampeni ya wagombea wetu" hii statement ina uzito wake pia kijana wetu Nape akasema "tutashinda hata Kwa goli la
mkono 2015"

akamshauri Byabato Kule Bukoba akae Kwa kutulia maana yeye ni mzoefu kweli na atampa mbinu ya ushindi "issue sio kupiga Kura ila anayesimamia Kura kuhesabiwa na matokeo kutangazwa......."
Kuna DC akasema wazi kuwa 2020 Madiwani hawakufanya kampeni bali walipitishwa na yeye alishiriki ipasavyo...." nilifanya Kazi kubwa na naenda hadi porini kufanya Kazi......."

Kwangu naweza kusema hawa ndio waliongea kishujaa sio Balozi wetu Polepole anatoa simulizi nani asiyejua alihusika kwenye ulanguzi wa viongozi wa vyama pinzani ( refer case ya Mashinji) akiwa kama mkurugenzi wa mafunzo na Itikadi alibeba 30M kumlipia fine aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA (hapa namaanisha kama ameamua kuokoka toa vyote vilivyo vya shetani sio kubaki na hirizi na vyungu ukisema unaacha Kwa ajili ya kusikilizia). Kasahau 2020 Fomu ya URAIS ilikuwa Moja though anajitetea kuwa Prime Minister & Vice president hawatakiwi kuwa President wa Nchi ....... ......

Vice president ni President na haongozi kwenye term ya V yupo ya Vi kama Watangulizi wake katika awamu zao wali- enjoy the so- called Fomu Moja why not Samia, hapa nongwa ya nini na ifahamike kila zama na namna yake na kila kiongozi anapata uongozi Kwa style yake refer case ya GERALD FORD alikuwa US House of Representative lakini 1973 Spiro Theodore Agnew stepped down na Ford akawa Vice na August 1974 Nixon Richard akaondoka kwa kashifa ya "Watergate Scandal" na Ford akawa Rais wa USA. Huu ni mfano tu kuwa kila mtu anakuwa kiongozi Kwa namna tofauti Mungu anavyo mwezesha.

Kwangu Nape na Mkapa ndio mashujaa wa kusema ukweli uliofichwa Humphrey Polepole bado hajaleta Jambo Jipya yupo kwenye kutafuta legality sio legitimacy kama ambavyo alimsaidia Rais wa awamu ya TANO kutimiza the- so called LEGITIMACY Leo kijana hataki hiyo Kwa Rais Samia.

NB: Nazani Kwa kizazi cha Leo wanamhitaji mtu atakayesema ukweli mchungu ambao utapelekea mageuzi kwenye maisha ya watu wa kizazi hiki, kizazi hiki kinahitaji MITAJI, AJIRA, AFYA BORA, MAZINGIRA MAZURI YA BIASHARA, UWEKAZAJI WENYE TIJA na MIKOPO hasa Kwa watoto wetu (HESLB). Kama kuna mtu analeta narratives za Maisha yake is out of focus.

Shukran Sana ndugu zangu Naomba niishie hapa.
​
 
Uko sahihi but Kwa Upande wangu as long as aliyo yaongea pole pole Yamesababisha conflict ktk chama Chao Mimi napata Raha tu maana ma-ccm siyapendi kinoma

Na kama ilivyo desturi Tuna paswa kumuombea adui njaa
 
Vice president ni President na haongozi kwenye term ya V yupo ya Vi kama Watangulizi wake katika awamu zao wali- enjoy the so- called Fomu Moja why not Samia, hapa nongwa ya nini na ifahamike kila zama na namna yake na kila kiongozi anapata uongozi Kwa style yake
Kwanza nakupongeza sana mkuu kwa bandiko zuri na lilojaa hoja

Mbali na hayo na kulaumu kina HP kwa nini hawasemi ukweli na kwa nini waogope kuweka mambo wazi

Hata wewe, bado upo upande ule ule unaoulaumu, kwa sababu, unaposema Samia ni kiongozi wa awamu ya sita na siyo ya tano, Je, tulifanya uchaguzi lini baada ya JPM kufariki?

Huoni kwamba mbinu hizi unazozitetea ndizo zinazowatesa CCM leo?
 
Kwa miaka yote CCM imestawi na kustawi kwa mgongo wa wajinga na ujinga ambapo ukosoaji ilionekana kama ni dhambi ya kuua mtu.

Huu uamsho na uelewa ni kitu kipya kwa ccm.
 
Watangulizi wake katika awamu zao wali- enjoy the so- called Fomu Moja why not Samia,..
Je, utaratibu wa hiyo "fomu moja" umefuatwa?

Kwamba mtu amechukua na kujaza fomu, akatafuta wadhamini kwa mujibu wa taratibu, akarejesha, vikao vikamjadili na kumpitisha kama ilivyokuwa kwa hao watangulizi?

Mkivunja taratibu na kutofuata kanuni na Katiba, mnatengeneza precedence ya kukiuka zaidi Kanuni na Katiba huko mbeleni
 
Uko sahihi but Kwa Upande wangu as long as aliyo yaongea pole pole Yamesababisha conflict ktk chama Chao Mimi napata Raha tu maana ma-ccm siyapendi kinoma

Na kama ilivyo desturi Tuna paswa kumuombea adui njaa
Na wakati mwngine ikifikia hatua njaa ukaona haitoshi kumuadhibu , unamuombea adui Kifo ! Adui tulio nao kwa sasa kama Taifa, njaa haiwezi kuwaumiza maana wameisha iba na kuweka akiba ya kutosha kwenye matumbo yao hivyo hawawezi kuathiriwa na njaa, ila ni kuwaombea Kifo ndicho hawana ujanja nacho. Maana hata wakienda India bado hawataweza kukishinda ! Mungu atusaidie katika kuaharakisha kuondoka kwao hapa !
 
Kwanza nakupongeza sana mkuu kwa bandiko zuri na lilojaa hoja

Mbali na hayo na kulaumu kina HP kwa nini hawasemi ukweli na kwa nini waogope kuweka mambo wazi

Hata wewe, bado upo upande ule ule unaoulaumu, kwa sababu, unaposema Samia ni kiongozi wa awamu ya sita na siyo ya tano, Je, tulifanya uchaguzi lini baada ya JPM kufariki?

Huoni kwamba mbinu hizi unazozitetea ndizo zinazowatesa CCM leo?
Rais Samia alipita Kwa Wananchi akiwa na Magufuli bahati mbaya 2021 Magufuli akatutoka. Rais Samia ameongoza Kwa takribani miaka minne (4) ambayo ni awamu kamili Kwa maana hataruhusiwa kugombea Kwa vipindi viwili (Katiba yetu 1977). Kama ilivyo ndani ya CCM huwa tunakuwa na Legitimacy na sio Legality (H.Polele), Rais Samia anaamini pia kwenye Legitimacy kumalizia awamu yake ya pili bila kujali URAIS wake umepatikanaje ( refer bandiko hili case ya GERALD FORD, US PRESIDENT). Tatizo lipo ndani ya CCM yenyewe walipoamua kuua Legality na kukumbatia Legitimacy.
 
Je, utaratibu wa hiyo "fomu moja" umefuatwa?

Kwamba mtu amechukua na kujaza fomu, akatafuta wadhamini kwa mujibu wa taratibu, akarejesha, vikao vikamjadili na kumpitisha kama ilivyokuwa kwa hao watangulizi?

Mkivunja taratibu na kutofuata kanuni na Katiba, mnatengeneza precedence ya kukiuka zaidi Kanuni na Katiba huko mbeleni
Is a matter of legitimacy and not legality (H.polepole).
Utaratibu wa CCM baada ya miaka 5 inatakiwa kuwa na ushindani huru na wazi lakini watu waka- formalize principles to favour on their own side, Rais Samia nae anapita walipopita wenzake bila kujali kanuni za Chama zinataka nini.
 
Na wakati mwngine ikifikia hatua njaa ukaona haitoshi kumuadhibu , unamuombea adui Kifo ! Adui tulio nao kwa sasa kama Taifa, njaa haiwezi kuwaumiza maana wameisha iba na kuweka akiba ya kutosha kwenye matumbo yao hivyo hawawezi kuathiriwa na njaa, ila ni kuwaombea Kifo ndicho hawana ujanja nacho. Maana hata wakienda India bado hawataweza kukishinda ! Mungu atusaidie katika kuaharakisha kuondoka kwao hapa !
Kwa nini isiwe mbele zaidi kwa kuwasababishia vifo na si kuwaombea vifo?
 
Niende kwenye Mada Kwa ufupi Sana,

Nimewaza mengi lakini kubwa huenda Wazee wetu walioasisi hili Taifa letu (Tanganyika) hakuwa JASIRI kama ambavyo tunawasoma kwenye historia.

Kiongozi shupavu haogopi ushindani, kuwajibika na kukubali ukosoaji mfano tangu tupate UHURU wa Nchi yetu wakosoaji wengi walipitia nyakati ngumu akina Christopher Tumbo wakapewa vyeo nje ya Nchi (Uingereza) Lengo kunyamazisha Upinzani(iwapo baadae aliachana na hiyo nafasi na kurudi nyumbani kuendeleza MAPAMBANO) na wengine akina Bi. Titi wakafungwa Kwa kosa la uhaini pia wengine wakawekwa kizuizini (Detention) kama Tuntameke Sanga (Msomi huyu) hiyo ndio historia ya watangulizi wetu.
(
Kulingana na Uchanga wetu hasa tukiwa Moja ya Nchi iliyojitoa kusaidia na kuleta ukombozi kulikuwa na maana ya kuwa na uongozi wa namna hii plus Siasa ya Vita baridi (COLD WAR POLITICS) lakini ni lazima tukubali kuwa Changamoto za siasa za vita baridi hazijaisha Kwa hiyo umakini katika kusimamia Itikadi ya Nchi yetu ni muhimu maana Karne hii ni rahisi kupewa kiongozi mweusi mwenye Roho ya kizungu)

Watangulizi wetu waliandaa Katiba ya Leo ambayo kwetu inaonekana inaminya Demokrasia pia walianzisha mfumo wa uongozi ambao hadi Leo tunae Mama yetu kipenzi Samia na huo mfumo haujabadilika bali wamebadilika watu Kwa maana kuna vijana wamezaliwa kwenye uso wa Nchi yetu (Tanganyika) natumia neno Tanganyika Kwa sababu watu wa upande wa visiwani Wana tabia tofauti kabisa na ni waungwana Madhira Yao yote ni influence ya Tanganyika (refer General election 2015).

Hadithi zote za kiutawala na uongozi zinawekwa kuwa Siri, kuwa ni Jambo la Usalama wa Taifa na hapa ndio kiini macho kinaanzia. Shujaa pekee ni Yule atakayekuja akafungua yaliyomo huko ndani maana yale ya historia wengi tunayajua.

Humphrey Polepole hakuja na Jambo jipya bado ana tabia zile zile za kale kuficha ficha mambo tunayohitaji kujua, Kijana kaja na historia yake ambayo sio hitaji la wengi wetu mfano Mimi binafsi ningependa kama angesema Kwa uwazi hao "WAHUNI" waliotaka kuchakachua uchaguzi wa 2015 na mchakato wa Katiba 2014. Huyu kijana nilitegemea aseme Nani anaongoza na kutoa maelekezo katika Nchi yetu maana anasema
"
kama nyumba haina mwenyewe"
Anasema kuna kikundi kina nguvu na anawajua wahusika basi wataje ndio mambo tunataka lakini kaishia kusema historia na kutumia codes of which most of us we are very aware of it.

Humphrey cannot be compared with Nape na Mkapa na wengine Kwa sababu Rais wetu huyu 1995-2005 aliwahi kusema kupitia kitabu chake "
CCM tulichukuwa pesa za Serikali Kwa ajili ya kampeni ya wagombea wetu" hii statement ina uzito wake pia kijana wetu Nape akasema "tutashinda hata Kwa goli la
mkono 2015"

akamshauri Byabato Kule Bukoba akae Kwa kutulia maana yeye ni mzoefu kweli na atampa mbinu ya ushindi "issue sio kupiga Kura ila anayesimamia Kura kuhesabiwa na matokeo kutangazwa......."
Kuna DC akasema wazi kuwa 2020 Madiwani hawakufanya kampeni bali walipitishwa na yeye alishiriki ipasavyo...." nilifanya Kazi kubwa na naenda hadi porini kufanya Kazi......."

Kwangu naweza kusema hawa ndio waliongea kishujaa sio Balozi wetu Polepole anatoa simulizi nani asiyejua alihusika kwenye ulanguzi wa viongozi wa vyama pinzani ( refer case ya Mashinji) akiwa kama mkurugenzi wa mafunzo na Itikadi alibeba 30M kumlipia fine aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA (hapa namaanisha kama ameamua kuokoka toa vyote vilivyo vya shetani sio kubaki na hirizi na vyungu ukisema unaacha Kwa ajili ya kusikilizia). Kasahau 2020 Fomu ya URAIS ilikuwa Moja though anajitetea kuwa Prime Minister & Vice president hawatakiwi kuwa President wa Nchi ....... ......

Vice president ni President na haongozi kwenye term ya V yupo ya Vi kama Watangulizi wake katika awamu zao wali- enjoy the so- called Fomu Moja why not Samia, hapa nongwa ya nini na ifahamike kila zama na namna yake na kila kiongozi anapata uongozi Kwa style yake refer case ya GERALD FORD alikuwa US House of Representative lakini 1973 Spiro Theodore Agnew stepped down na Ford akawa Vice na August 1974 Nixon Richard akaondoka kwa kashifa ya "Watergate Scandal" na Ford akawa Rais wa USA. Huu ni mfano tu kuwa kila mtu anakuwa kiongozi Kwa namna tofauti Mungu anavyo mwezesha.

Kwangu Nape na Mkapa ndio mashujaa wa kusema ukweli uliofichwa Humphrey Polepole bado hajaleta Jambo Jipya yupo kwenye kutafuta legality sio legitimacy kama ambavyo alimsaidia Rais wa awamu ya TANO kutimiza the- so called LEGITIMACY Leo kijana hataki hiyo Kwa Rais Samia.

NB: Nazani Kwa kizazi cha Leo wanamhitaji mtu atakayesema ukweli mchungu ambao utapelekea mageuzi kwenye maisha ya watu wa kizazi hiki, kizazi hiki kinahitaji MITAJI, AJIRA, AFYA BORA, MAZINGIRA MAZURI YA BIASHARA, UWEKAZAJI WENYE TIJA na MIKOPO hasa Kwa watoto wetu (HESLB). Kama kuna mtu analeta narratives za Maisha yake is out of focus.

Shukran Sana ndugu zangu Naomba niishie hapa.
​
Kwa bongo ni kinyume chake... Kosoa uone 🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom