Kiongozi wa kundi la kigaidi la Isis la nchini Iraq na Syria auwawa.

Kiongozi wa kundi la kigaidi la Isis la nchini Iraq na Syria auwawa.

Imeloa

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Posts
14,885
Reaction score
18,083
Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed Shia Al Sudani alitangaza siku ya Ijumaa kwamba Abdullah Miki Musleh al Rifai ambaye pia hujulikana kama Abu Khadija kiongozi wa kundi la kigaidi cha Isis cha Iraq na Syria ameuwawa.

Gaidi huyo ameuawa kwenye opereseheni iliyofanywa na vikosi vya ulinzi vya Iraq kwa ushirikiano na Marekani.

Abu Khadija alikuwa akifikiriwa kuwa moja kati ya magaidi hatari nchini Iraq na duniani kwa ujumla.

Abu Khadija alikuwa ni nguzo katika safu ya uongozi katika kikundi cha kigaidi cha Isis na hapo kabla alitajwa kama mtu ambaye angeweza kuwa kinara wa kundi hilo maarufu kama "Caliph" kutokana na nafasi yake katika kundi hilo la kigaidi. Kifo chake kinawakilisha pigo kubwa kwa opereseheni za kundi hilo la kigaidi kieneo.

ISIS leader for Syria and Iraq Abu Khadija killed: Iraq PM - The Times of India
 
Back
Top Bottom