Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Eehe yamekuwa haya.....!
kila baya likitokea ni upinzani tu
hivi wananchi kwani hatuna akili? au kwani tumeridhika?
 
Kuna habari nimezisikia kuhusu Dr Ulimboka kwenye sakata lake zinasikitisha.

Kila mtu niliyekutana naye leo anaongea Dr Ulimboka, na wako wanaume wametoa machozi.
 
....niko kwenye kifo cha horace kolimba....taarifa ya uchunguzi wa kitaalam iliyofanywa na wataalam, waliochaguliwa na familia ya marehemu haikusema lolote juu ya sumu...!
 
Haya ni mawazo ya wana CCM ili kujivua na uovu waliomtendendea Dr. Ulimboka
 
Ana habari gani huyo?

Habari awe nayo Ritz; ni kitu gani kama si UBUNIFU wa tangu leo asubuhi kumtafutia Dr Ulimboka 'Mbaya Mpya Mwenye Uwezo wa Kuteka Kijeshi' ili mhusika halisi aliyefanya mambo bila kutafakari apate kubaki salama.

Too late na narudia kwamba ni TOO LATE for any cover-up in this instance. DNA info zote zilishachukuliwa saa nyiiiiingi ajabu.

Na satelite pictures and voice signals za ndani y wiki mbili hadi leo are SO DAMNING if not overwelming!!! Ehe, hebu endelea kutuletea theories nyinginezo za kule CCM Barabara ya Lumumnba hapa tukasome.

ritz mwaga habari
 
Vichipkizi VGA TISS Bwana...Viko kizamaaaani? Utafikiri vimezaliwa Aldeia Msumbiji?
 

KOva alimsafisha eti yule askari alitumwa kwenda kumlinda Dr Ulli pale muhimbili... too late...
 

...hilo la kuuawa kwa wazanzibar kabla ya muafaka ulioleta serikali ya umoja wa kitaifa ....tuseme bila ya kutafuna maneno...ni matokeo ya "kujifanya wanajua kumbe wanaungua na jua"....mzee mwenye hekima na mwenye kuzijua siasa za zanzibar, nje ndani, aliwaambia mapema...mwaka 1995, mara tu baada ya uchaguzi, kuwa ili pawepo na amani na utulivu wa kisiasa ktk zanzibar, basi na iundwe serikali ya mseto...wakajifanya ati mafundi....!
 
Huyo hana habari zozote ni uzushi tuu ...si hao hao hana lolote wanahangaika sasa kutunga story zao ili kujaribu kupoteza ukweli !! kmnn zao .......mmeumbuka na sasa ndiyo kila kitu mwaaa.... !! Safari hii lazima mdondoke airport kwa mawazo...!
 
Tumuombee apone huyu kijana. it is so sad kwa kweli TZ inatisha!
 
Kwa mtazamo wangu binafsi huyo mama hata kama anaumafia wake hawezi kuwa na ujasiri wa kupanga mauaji kwa njia ya jinsi hiyo.
Naungana na wachangiaji wengine kwamba mipango ya kumpoteza DR. itakuwa ni mipango kutoka juu zaidi. Nina mashaka sana kwamba Mr Pinda anahusika moja kwa moja katika hili.
Mtazamo binafsi "HUENDA" Amiri Jeshi mkuu amebariki tendo hili na vijana waliotumwa kufanya kazi hiyo Roho zao zimekuwa za kibinadamu zaidi kwani hawakupenda kumtoa roho DR badala yake wameamua kumnyanyasa na kumwacha akiwa hai ili kuwaumbua wahusika wakuu wa jambo hilo.
Subira yavuta heri na siku ya kufa nyani mti yote huteleza..TUTAPATA MAJIBU..!!

 
Naomba tulejee wiki ambayo watanzania walikuwa wanajadili matokeo ya uchaguzi wa arumeru je nini kilitokea.

Tulipatwa na habari za msiba wa marehemu kanumba

Sasa tuko tunajadili mgomo wa madaktari na implication zake kwa maisha yetu,guess what we end up with,another beautiful headline.

SIASA NI MCHEZO MCHAFU
 

I am sorry to say your argument is baseless,based on hearsay. And this line of thinking is totally misguided

Kama serikali kuangushwa inajuangusha yenyewe kwa madudu inayofanywa. Je unamfahamu nani mwenye kampuni ya Kagoda? Nani walifaidi kwenye michongo kama Meremeta,Radar,Ndege ya Rais, Deep Green? Kwa nini watu wanaendelea kuiba rasilimali fedha wapo na hawachukuliwi hatua? Je mwalimu anayedai 2,000,000/= akaandikiwa hundi ya laki mbili(200,000), huku serikali ikilipa 2,000,000/= na 1,800,000/=(inakwenda tumbo street) aliyetayarisha bado yupo hapo vipi?

Kiongozi kashiriki kwenye rushwa ya radar pesa imeonekana kule Jersey Islands na anaendelea kupeta hapo vipi? Je matumizi mabovu ya rasilimali fedha yanayoendelea ndani ya serikali yamesababisha na hao wanaofanya mgomo au maandamano? Mambo yanayofanywa na serikali ni machafu sana na hayana uzalendo na mchanganyiko wa hayo yote ndio yanayozaa haya tuonayo sasa. Haya hayakutokea kwa bahati mbaya. Kwa nini? Kwa sababu zama zimebadilika,watu wanaelewa zaidi sasa kuliko miaka ya nyuma.Watu wanajiuliza,kwa nini yeye akiumwa akatibiwe Appolo India,lakini mimi ugonjwa uleule nitibiwe Mwananyamala? Kwa nini rasilimali za nchi zinagawanywa au wanagawana wachache tu,ila sisi tukidai haki yetu tunaambia serikali haina fedha? Kwa nini yeye anaweza kumpeleka mwanae shule kule Canada,Uingereza nk lakini mimi uwezo ni kumpeleka shule ya kata? Maswali yapo mengi na haya ndio yanayoleta kizaazaa chote hiki.

Serikali inachoweza kufanaya ni kutengeneza utaratibu wa kuwageuza watu wenye kujiuliza maswali haya wawe na fikra kama za zamani kwa kutengeneza teknologia itakayorudisha muda nyuma. Au serikali ijirudi iseme wizi,ubadhirifu,u-mungu mtu, kiburi cha viongozi,ubabaishaji, naizesheni sasa basi. Je lipi kati ya haya mawili ni rahisi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…