Kiongozi wa mbio za mwenge 2022 anaupiga mwingi

ESCORT 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Posts
1,412
Reaction score
3,043
Kwenye kukagua miradi yuko makini sana, anathibitisha yeye mwenyewe yaani kama VAR katika mpira.

Tuliona akikagua ubora wa barabara, na sasa tunaona akikagua miundombinu mbalimbali akiwa mkoani Mtwara.

Kwa hakika, huyu jamaa waliomfanyia vetting walichagua kiongozi bora natamani haya makeke yake angekuwa anayafanya awamu ile ya 5 naamini angefika mbali sana.

Kongole kwake...



 
Akakague zile temporary office za full suit mabati moja ya milioni Saba na nyingine ya milioni Mia.
Lkn pia akakague zile pikipiki za milioni 11.
Kwanini hawakaguagi reli SGR DAR Moro .
Tuliambiwa itafanyiwa majaribio April mwaka huu. Leo ni tarehe 17 sioni dalili na mvua zimeanza
 
Hivi huyo mtu ana mamlaka juu ya RC, au?
Halafu yeye anaripoti kwa nani?
Na, ana taaluma gani?
 
Aende bandarini akakague..hakika atajionea maajabu ya nchi.

#MaendeleoHayanaChama
 
A
Akifika kilimanjaro kule wilaya ya Hai, akakague barabara zolizojengwa na Tarura huko vijijini ajionee fedha zinavyoibiwa hovyo
 
Anapotumia sululu siyo kwamba anakagua Ubora, anachofanya ni mbadala ya Drilling ili kuweza kujua thickness kujua unene wa Mchanga, Kokoto, Zege, Lami nk. So tusibeze kila kitu jamani yeye ndio njia aliyooona inafaaa kugagua layers za hiyo barabara. Labda mkuu twambie njia gani angeweza kutumia ikawa na Ufanisi zaidi?
 
Njia zipo za aina tofauti tofauti, hiyo drilling sio njia ya kutest bituminous Road quality. Labda angetumia mojawapo kati ya hizi

1. Crack index
2. International Roughness Index
3. Friction Testing, au
4. Falling Weight Deflectometer Test
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…