Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 651
- 433
KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU AZINDUA HUDUMA ZA AFYA ZAHANATI YA KIJIJI NDULUNGU
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Ndg. Wazo Michael Mwang'onda, tarehe 24 Julai, 2026, amekagua na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ndulungu, uliopo kijiji Ndulungu, kata ya Ndulungu, tarafa ya Ndago, na kuzindua rasmi huduma za afya katika zahanati hiyo.
Akizindua huduma hizo Ndg. Mwang'onda ametoa pongezi kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha huduma za afya nchini.
" Lengo kubwa la serikali ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora za afya" alisema
Akisoma taarifa ya mradi, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Dkt. Peter Luhenga, ameeleza kuwa mradi huo una thamani ya shilingi milioni 225, fedha kutoka Serikali Kuu.
Mradi huo unahusisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la huduma za mama na mtoto, nyumba ya watumishi, kichomea taka, shimo la plasenta, shimo la majivu, mnara wa tanki la maji na tanki lenye uwezo wa lita 5,000, pamoja na ukamilishaji wa jengo la kujifungulia.
Kukamilika kwa mradi huo kumeimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wa Kata ya Ndulungu na maeneo jirani, sambamba na kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa afya.