Kiongozi wa NCCR adai Mbowe alinunua bia baada ya kusikia msiba!

Kiongozi wa NCCR adai Mbowe alinunua bia baada ya kusikia msiba!

Je kuna kosa kwa Mbowe kupiga kileo wakati chacha alipofariki

  • Total voters
    20
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Alah! kumbe inasemekana na wala haijathibitishwa......

Tunawahitaji sana Nyani wenye akili kama wewe.
Kwa kuwa siku za hivi karibuni Tanzania inaonekana kupiga hatua kubwa katika tekinolojia, hasa baada ya uchawi uloiomwagwa Bungeni kuchunguzwa na Mkemia Mkuu na kutoa majibu, sitashangaa iwapo yupo mtu aliyepima kiwango cha furaha au huzuni ya Mbowe baada ya kupewa taarifa za msiba
 
Mimi kama Mtanzania huru kwenye nchi huru nahisi huu ni upandikaji wa chuki wenye maslahi binafsi kwa watu wachache wenye yao mambo!

Kevo,
Sikuwa na nia ya kuchangia katika thread hii zaidi ya kusoma na kuacha kama ilivyo. Lakini ninaomba turudishe kumbukumbu zetu nyuma hasa pale unaposema kuwa '...ni upandikizaji wa chuki...' Kama ulikuwa ni mfuatiliaji makini wa wanasiasa wa Tanzania katika kampeni za urais 2005, Mh Mbowe ndiye aliyekuwa anasema kuwa lazima apandikize chuki kwa wananchi ili waichukie serikali yao. Wacha siasa zifanye kazi za wanasiasa!
 
Mzee Mwanakijiji,

Jamii nyingi za Kiafrika hunywa pombe kwenye msiba. Ila mtu aliyembali, akionekana anaendelea kuweka kinywaji na wenzake baada ya kupata habari za msiba, hapo watu wengi wanaweza kushutuka.

Baada ya kufika kwenye msiba na kumwaga chozi la nguvu, hapo ndipo unaanza kusherehekea maisha ya marehemu na mnaweza kupata na kinywaji.

Kama mheshimiwa aliendelea kupata moja baridi, moja moto, hiyo ni dalili hakushutushwa na kifo cha marehemu.

Binafsi simlaumu Mbowe kwa hilo. Kama alimchukia Wangwe akiwa hai, kuna haja gani ya kuweka unafiki na kujifanya alikuwa kipenzi chake baada ya kufa?

Mtanzania,

Borta umesema ukweli kuhsuiana na kile ninachokifahamu.Mie nadhani ni wakati mzuri wa kurudisha heshima ya Upinzani iliyoharibiwa na watu.

Hii siyo jokes bwana,Mie nadhani kuna kitu hapa JF ambacho sikielewi.Ina maana Kama mtu ni wa CHADEMA hajadiliki???Mtueoleze and we will stop talking

Mkuki kwa Nguruwe siyo??
 
Gembe umeoza unanuka ufisadi kama hao mafisadi wenzako waliokutuma kutuchanganya hapa JF ili tusiwabade mafisadi. wewe ni mufilisi... ni sawa na yule ibilisi aliyewashawishi Adam na Eva kula tunda. Kwani kununulia pombe watu ni kosa? wewe mbona unanunuliwa na mafisadi. Kama unayaandika haya ili udhoofishe vita ya kuwakomboa Watanzania masikini wanaonyanyasika kwa matokeo ya ufisadi na ulaanike! Damu ya watanzania wanaokufa kwa ajili ya huo ufisadi unaotetea na iwe juu yako na kizazi chako. Ikulilie popote uendako. Utangetange kama yule ibilisi aliyelaaniwa!!!

Jadili hoja usijadili mtu, mwache Gembe aendelea kutoa hoja na sisi wengine kuzipinge kwa hoja vilevile. Usipoteze muda wako kwa kuandika kama ulivyoandika hapo juu. Kama unampenda sana Mh Mbowe na hutaki aongelewe hapa basi nenda ukanywe nae chai. Tunahitaji hoja.
 
Acheni unafiki wakijinga kaeni chini andikeni vitu ambavyo vitaikomboa nchi hii siyo kushikilia udaku hapa..hel of you..nyie ndo mafisadi kwa kupelekwapelekwa
Twende sasa,

Mie nadhani hivi vitu ni vya misngi sababu vitakomboa vyama vya Upinzania and Hence vitakomboa nchi yetu kw aujumla,nadhani wewe uanhisi tuna mpango wa kumuangamiza Mwenyekiti ..la hasha tuko hapa kujadili tu nini kifanyike sababu ya ugomvi wa vyama hivi vya upinzani.
unaweza ukaona Joke kama Mod alivyoamua ila joke ndizo huwa zinakuwa za kweli,kama Mwenyekiti alikiri hivi inakuwaje Joke.Ya msingi nyie mlishayaacha siku nyingi mkaanza kukimbilia kuongela watu na kuacha mambo yanayowahusu wananchi yasijadilike.Hii ni wiki ya mwisho then tutaanza kuzungumzia yanayohusu nchi kwa kuwa Rais ataanza kuyafanyia kazi kuanzia Alhamisi

Gembe

Tazama akili zako zilivyo, tazama mlivyo na muda wa ziada, Tazama mnavyojikanganya, sijui tunaelekea wapi, mmejijaza hapa kujadili upuuzi, badala ya kutoa ushauri ili kuboresha upinzani ninyi mnazidi kuubomoa.

Akili zenu ndivyo zilivyo, toeni mapendekezo nini kifanyike ili kuboresha jamani, kisha nagundua kuwa leo hamna kazi za kufanya, fuadi yangu yanisukuma niwaambie jitahidini kuwa na mikakati ya 2010 kuliko kumjadili Mtu(Mbowe) kila kukicha.

Mimi katika thread yangu ile nilimshauri Mbowe ajiweke pembeni ili hawa Mafisadi na wale wate wanaotumiwa na Mafisadi wakose Mshiko.

Sasa tazama wanavyoyabuni, tazama wanavyompaka Tope, Tazama wanavyohakikisha kuwa Demokrasia hii changa haikui.

Isaya Mwita,
Unatumia jina la nyumbani ili tukuheshimu au?huu ni upuuzi?Ushauri tulishawapa siku nyingi hamtaki kusikia,tuliawaambia msijione Bora kuliko vyama vingine mkatupuuza mkaona siye tupo kwa ajili yenu?
Nini kifanyike?hilo ndilo swali la msingi

1.Ondeeni sura ya ukabila ndani ya CHADEMA,kionekana chama ambacho kipo kwa ajili ya watanzania wote na siyo kwa ajili ya watu wa kanda ya kaskazini hasa wachagga

2.Mnyika aende akaaombe msamaha kwa viongozi wa Upinzani ,tena akiambatana na Mbowe waseme walikosea kujiona wao wapo juu ya vyama hivi vingine.

3.Mwenyekiti aome radhi kuwa alikosea sana kukataa rambi rambi ya wale watu waliompa kule SA.

4.Mwambieni Zitto akiri kuwa Marehemu chacha wangwe ameacha Pengo kubwa katika Chama Chenu.Na aseme wakati ule alipoohojiwa alikuwa katika wakti mgumu wa kughafilika alipoulizwa na watu wa Media

Hayo ni machache tu kwa leo,mkianzia hapo nitawapa mengine ya kufuata
 
Gembe

Tazama akili zako zilivyo, tazama mlivyo na muda wa ziada, Tazama mnavyojikanganya, sijui tunaelekea wapi, mmejijaza hapa kujadili upuuzi, badala ya kutoa ushauri ili kuboresha upinzani ninyi mnazidi kuubomoa.

Akili zenu ndivyo zilivyo, toeni mapendekezo nini kifanyike ili kuboresha jamani, kisha nagundua kuwa leo hamna kazi za kufanya, fuadi yangu yanisukuma niwaambie jitahidini kuwa na mikakati ya 2010 kuliko kumjadili Mtu(Mbowe) kila kukicha.

Mimi katika thread yangu ile nilimshauri Mbowe ajiweke pembeni ili hawa Mafisadi na wale wate wanaotumiwa na Mafisadi wakose Mshiko.

Sasa tazama wanavyoyabuni, tazama wanavyompaka Tope, Tazama wanavyohakikisha kuwa Demokrasia hii changa haikui.

Isayamwita,
Kama kweli unapenda demokrasia iendelee kukuwa katika nchi hii basi usiogope kusema yale ambayo unayaamini na vilevile usiogope mawazo tofauti na yale ya kwako. Kukosoa na kukosolewa ni sehemu ya misingi ya kuimarisha demokrasi.
Ni vyema pia ukaupata upande wa pili wa watu wengine jinsi wanavyomuona kiongozi wako, kumbuka hata China wanabadilika wakati wa 'utukufu' umekwisha.
 
Tatizo Watuwa CHADEMA wanajipa uwezo kwamba hawajdiliki
 
Yaani mzee uliweka hii taarifa bila kuangalia kwanza kwenye hayo magazeti? na kila taarifa ya gaezti ni ya kuiweka hapa?? Nina maswali yafuatayo kwako mkuu

1.Je ulipita muda gani tangu Mbowe kupata taarifa na kuwanunulia watu bia?
2.Je huwa ni kawaida yake kuwanunulia watu bia au ilitokea siku hiyo tu wakati amepata taarifa?
3.Ikiwa ni mara ya kwanza kuwanunulia watu bia je si tunaweza kusema alipata na mshtuko na ili kurelief stress zake akanunua bia?
4.Kuna standard gani ya mshtuko ambayo mtu akiipata kuhusu msiba tutasema ama kweli alishtuka!
5.Na je katika 'mashtuko' au vilio vyote ya misiba wanayoipata watu yote huwa ya kweli na mingine haina walakini? Kwa maana kama ulitaka Mbowe ashtuke bado tu angejifanya ameanguka na watu mkaamini(kama yeye amehusika), kwa hiyo hoja ya kushtuka haingii akilini.Watu wametofautiana kuabsorb shocks, na perception za watu zimetofautiana.Ulitaka afanye nini kaka?Nimeona watu wakiact kuwa wamezimia kumbe ndio walioua!
6.Je katika kusema hivyo no matter umepata wapi taarifa hii, je wewe mawazo yako ni nini? unataka kutoa conclusion gani? usizunguke mbuyu?
7.Je wewe ukipata msiba huwa unareact vipi tujue kuwa umeshtuka, katika misiba yote uliyowahi kusikia( here I am talking about your personal experience).?
8.Hiyo picha kwenye jina lako ni nani Mkapa au?

Waberoya
Don't let school interfere with your education
1.Je ulipita muda gani tangu Mbowe kupata taarifa na kuwanunulia watu bia?
hilo analijua Mbowe
2.Je huwa ni kawaida yake kuwanunulia watu bia au ilitokea siku hiyo tu wakati amepata taarifa?
Hilo anaweza kulijibu Mbowe
3.Ikiwa ni mara ya kwanza kuwanunulia watu bia je si tunaweza kusema alipata na mshtuko na ili kurelief stress zake akanunua bia?
wewe unasemaje?
4.Kuna standard gani ya mshtuko ambayo mtu akiipata kuhusu msiba tutasema ama kweli alishtuka!
5.Na je katika 'mashtuko' au vilio vyote ya misiba wanayoipata watu yote huwa ya kweli na mingine haina walakini? Kwa maana kama ulitaka Mbowe ashtuke bado tu angejifanya ameanguka na watu mkaamini(kama yeye amehusika), kwa hiyo hoja ya kushtuka haingii akilini.Watu wametofautiana kuabsorb shocks, na perception za watu zimetofautiana.Ulitaka afanye nini kaka?Nimeona watu wakiact kuwa wamezimia kumbe ndio walioua!
6.Je katika kusema hivyo no matter umepata wapi taarifa hii, je wewe mawazo yako ni nini? unataka kutoa conclusion gani? usizunguke mbuyu?
Mawazo yangu nilishayatoa unaweza kuyasoma hapo juu
7.Je wewe ukipata msiba huwa unareact vipi tujue kuwa umeshtuka, katika misiba yote uliyowahi kusikia( here I am talking about your personal experience).?
Mie nikipata Msiba huwa namuachia mungu anipe Faraja
8.Hiyo picha kwenye jina lako ni nani Mkapa au?
Hiyo picha ni ya mzee mkapa na ilipigwa kipindi kile cha Mbowe club kama ulikuwapo
 
Gembe toa vielelezo; sie tupo hapa Bongo yetu hakuna kitu kama hicho; wewe ni mzushi uliye majuu au unapata habari ambazo sio credible? Najua wewe ni kada tu tena mbaya unataka kujisahau; msomi mzuri ni yule aliyeelewa mazingira na ambaye ukada wake unalenga kuwaleteam maisha bora wa TZ. Mbowe hana zaidi ya kuwa SA kwa shughuli maalum; na hiyo unaihusishaje na ajali; yeye akiwa SA nani limuona; ni gazeti gani la Tanzania lilienda na Mbowe SA; ni rafiki yake yupi aliyekwenda na Mbowe Sa aliyebwia pombe za mbowe t hen akamsaliti; speculation hizi hazina kichwa wala miguu na hizi zinatutoa ktk mada ya msingi ya EPA;Ufisadi;Zanzibar na Tanganyika; maisha magumu badala ya maisha bora; mafuta kupanda na dola kuzidi kupaa; mkuu tupeni mawazo mbadala ya kuendelez anchi yetu sio soga za vijiweni; hii forum serious sana na ina watu serious kweli kwa maisha ya wa TZ
 
Kevo,
Sikuwa na nia ya kuchangia katika thread hii zaidi ya kusoma na kuacha kama ilivyo. Lakini ninaomba turudishe kumbukumbu zetu nyuma hasa pale unaposema kuwa '...ni upandikizaji wa chuki...' Kama ulikuwa ni mfuatiliaji makini wa wanasiasa wa Tanzania katika kampeni za urais 2005, Mh Mbowe ndiye aliyekuwa anasema kuwa lazima apandikize chuki kwa wananchi ili waichukie serikali yao. Wacha siasa zifanye kazi za wanasiasa!

Kwa hiyo its eye for an eye siyo?
Chuki inalipizwa kwa chuki?
Simply coz alishawahi kufanya ama kusema hivyo ndio alipiziwe?
Tuone tutafika wapi tukiendelea na mambo kama haya!
 
Gembe toa vielelezo; sie tupo hapa Bongo yetu hakuna kitu kama hicho; wewe ni mzushi uliye majuu au unapata habari ambazo sio credible?

Mie ni kada tu mtanzania ila siyo kada mPinzani
Mie siyo mzushi kama unavyofikiri kipinzani
Kwa taarifa yako aliyeyasema haya ni Mpinzani
Ndiyo Mbowe mwenyewe alikiri yalisemwa na Mpinzani

Nimekuwa Mzushi siyo,Yeah Miw Mzushi Msema Ukweli
 
Asalamu Alaykum.

Kuhusu kunywa pombe baada ya kusikia msiba kunaweza kutafsiriwa kwa namna tofauti pengine alifurahia msiba wa hasimu wake lakini pia inawezekana alikunywa pombe kama kujiliwaza baada ya kupata haabri za msiba maana kila mmoja na mambo yake juu ya kujipa faraja baada ya taarifa za kuhuzunisha.

katika akili ya kawaida na utamaduni wetu watanzania sio rahisi kwa kweli kupata taarifa za msiba hata kama mtu ni hasimu wake mkubwa aliyefariki hawezi kufurahi.

mimi siamini sana kama Freeman Mbowe ameweza kufanya hivyo kwa nia mbaya sidhani pia kama amefurahi kwa kusikia habari za msiba inawezekana alijisikia kunywa kutokana na kutaka kupunguza mawazo tu. lakini unajua tena jambo likishaanza kutiwa chumvi kila mmoja anaweza kusema lake lakini katika hilo nani anaweza kuthibitisha kama kweli alifurahi kwa kunywa pombe na inakuwaje itoshe mtu kunywa pombe ndio kufurahi?
stonetowner
 
Kwa hiyo its eye for an eye siyo?
Chuki inalipizwa kwa chuki?
Simply coz alishawahi kufanya ama kusema hivyo ndio alipiziwe?
Tuone tutafika wapi tukiendelea na mambo kama haya!

Ni vyema tukajenga tabia ya kuwasilikiza hawa viongozi wetu wanapoongea na baadae tuje tuwapime kwa matendo yao. Ni mara kadhaa Mh. Mbowe ambaye aligombea urais wa nchi alihubiria wale anaotaka kuwaongoza wawe na tabia ya chuki. Kumbuka kuwa 'wimbo mbaya habembelezewei mtoto' Kama ni chuki ambazo unaziona zikimlenga Mh. Mbowe unadhani nani alizipandikiza?
Ni wakati mwafaka sasa wa kuwakumbusha hawa viongozi wetu kuwa wawe makini kwa yale wanayoyaongea, 'watanzania siyo mabwege tena'
 
Tena huu ni wakati Mzuri kwa kuwa tuanelekea kwenye uchaguzi wa TARIME ambao utafanyika tarehe 12 october 2008.

Tuanze kuchangisha pesa za Helikopta mapema
 
Ni vyema tukajenga tabia ya kuwasilikiza hawa viongozi wetu wanapoongea na baadae tuje tuwapime kwa matendo yao. Ni mara kadhaa Mh. Mbowe ambaye aligombea urais wa nchi alihubiria wale anaotaka kuwaongoza wawe na tabia ya chuki. Kumbuka kuwa 'wimbo mbaya habembelezewei mtoto' Kama ni chuki ambazo unaziona zikimlenga Mh. Mbowe unadhani nani alizipandikiza?
Ni wakati mwafaka sasa wa kuwakumbusha hawa viongozi wetu kuwa wawe makini kwa yale wanayoyaongea, 'watanzania siyo mabwege tena'

Mkuu mimi sikubishii!Kama alisema watu anaotaka kuwaongoza wawe na chuki mimi sijawahi kusikia kitu kama hiki na wala sitapinga wala kukubaliana na wewe maana I did not know about this!
Ila hata kama alisema kwa hiyo dawa ni kumlipishia kwa kumchafulia jina?
Please!!!!!!!!!!!
 
Muhimu hapa siyo mtu kuchafuliwa jina, la hasha, ni vema tufike wakati tuwakumbushe hawa waheshimiwa kuwa wanayoyasema tunayachukua na ikibidi kuyafanyia kazi. Endapo alikuwa anaongea kama 'porojo' wakati wakuomba kura kwa wananchi basi the guy was not serious, la kama ndivyo alivyomaanisha basi hana budi kuwajibika kwa kauli zake.
Tusidhani kuwa kurekebisha mambo katika nchi hii ni kazi ya viongozi, no! sisi sote kila mmoja wetu anawajibu kukosoa pale ambapo pamekosewa. Tukifanya hivi tutakuwa tunawatendea haki hao wanaotuongoza. Tuwaambie ukweli hata kama tunawapenda kiasi gani!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom