Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,172
Alah! kumbe inasemekana na wala haijathibitishwa......
Mimi kama Mtanzania huru kwenye nchi huru nahisi huu ni upandikaji wa chuki wenye maslahi binafsi kwa watu wachache wenye yao mambo!
Kwa hiyo utaka kusema Ndugu Mbowe alifurahia kifo cha Wangwe?
Mzee Mwanakijiji,
Jamii nyingi za Kiafrika hunywa pombe kwenye msiba. Ila mtu aliyembali, akionekana anaendelea kuweka kinywaji na wenzake baada ya kupata habari za msiba, hapo watu wengi wanaweza kushutuka.
Baada ya kufika kwenye msiba na kumwaga chozi la nguvu, hapo ndipo unaanza kusherehekea maisha ya marehemu na mnaweza kupata na kinywaji.
Kama mheshimiwa aliendelea kupata moja baridi, moja moto, hiyo ni dalili hakushutushwa na kifo cha marehemu.
Binafsi simlaumu Mbowe kwa hilo. Kama alimchukia Wangwe akiwa hai, kuna haja gani ya kuweka unafiki na kujifanya alikuwa kipenzi chake baada ya kufa?
Gembe umeoza unanuka ufisadi kama hao mafisadi wenzako waliokutuma kutuchanganya hapa JF ili tusiwabade mafisadi. wewe ni mufilisi... ni sawa na yule ibilisi aliyewashawishi Adam na Eva kula tunda. Kwani kununulia pombe watu ni kosa? wewe mbona unanunuliwa na mafisadi. Kama unayaandika haya ili udhoofishe vita ya kuwakomboa Watanzania masikini wanaonyanyasika kwa matokeo ya ufisadi na ulaanike! Damu ya watanzania wanaokufa kwa ajili ya huo ufisadi unaotetea na iwe juu yako na kizazi chako. Ikulilie popote uendako. Utangetange kama yule ibilisi aliyelaaniwa!!!
Twende sasa,Acheni unafiki wakijinga kaeni chini andikeni vitu ambavyo vitaikomboa nchi hii siyo kushikilia udaku hapa..hel of you..nyie ndo mafisadi kwa kupelekwapelekwa
Gembe
Tazama akili zako zilivyo, tazama mlivyo na muda wa ziada, Tazama mnavyojikanganya, sijui tunaelekea wapi, mmejijaza hapa kujadili upuuzi, badala ya kutoa ushauri ili kuboresha upinzani ninyi mnazidi kuubomoa.
Akili zenu ndivyo zilivyo, toeni mapendekezo nini kifanyike ili kuboresha jamani, kisha nagundua kuwa leo hamna kazi za kufanya, fuadi yangu yanisukuma niwaambie jitahidini kuwa na mikakati ya 2010 kuliko kumjadili Mtu(Mbowe) kila kukicha.
Mimi katika thread yangu ile nilimshauri Mbowe ajiweke pembeni ili hawa Mafisadi na wale wate wanaotumiwa na Mafisadi wakose Mshiko.
Sasa tazama wanavyoyabuni, tazama wanavyompaka Tope, Tazama wanavyohakikisha kuwa Demokrasia hii changa haikui.
Gembe
Tazama akili zako zilivyo, tazama mlivyo na muda wa ziada, Tazama mnavyojikanganya, sijui tunaelekea wapi, mmejijaza hapa kujadili upuuzi, badala ya kutoa ushauri ili kuboresha upinzani ninyi mnazidi kuubomoa.
Akili zenu ndivyo zilivyo, toeni mapendekezo nini kifanyike ili kuboresha jamani, kisha nagundua kuwa leo hamna kazi za kufanya, fuadi yangu yanisukuma niwaambie jitahidini kuwa na mikakati ya 2010 kuliko kumjadili Mtu(Mbowe) kila kukicha.
Mimi katika thread yangu ile nilimshauri Mbowe ajiweke pembeni ili hawa Mafisadi na wale wate wanaotumiwa na Mafisadi wakose Mshiko.
Sasa tazama wanavyoyabuni, tazama wanavyompaka Tope, Tazama wanavyohakikisha kuwa Demokrasia hii changa haikui.
Isayamwita,
Kama kweli unapenda demokrasia iendelee kukuwa katika nchi hii basi usiogope kusema yale ambayo unayaamini na vilevile usiogope mawazo tofauti na yale ya kwako. Kukosoa na kukosolewa ni sehemu ya misingi ya kuimarisha demokrasi.
Ni vyema pia ukaupata upande wa pili wa watu wengine jinsi wanavyomuona kiongozi wako, kumbuka hata China wanabadilika wakati wa 'utukufu' umekwisha.
1.Je ulipita muda gani tangu Mbowe kupata taarifa na kuwanunulia watu bia?Yaani mzee uliweka hii taarifa bila kuangalia kwanza kwenye hayo magazeti? na kila taarifa ya gaezti ni ya kuiweka hapa?? Nina maswali yafuatayo kwako mkuu
1.Je ulipita muda gani tangu Mbowe kupata taarifa na kuwanunulia watu bia?
2.Je huwa ni kawaida yake kuwanunulia watu bia au ilitokea siku hiyo tu wakati amepata taarifa?
3.Ikiwa ni mara ya kwanza kuwanunulia watu bia je si tunaweza kusema alipata na mshtuko na ili kurelief stress zake akanunua bia?
4.Kuna standard gani ya mshtuko ambayo mtu akiipata kuhusu msiba tutasema ama kweli alishtuka!
5.Na je katika 'mashtuko' au vilio vyote ya misiba wanayoipata watu yote huwa ya kweli na mingine haina walakini? Kwa maana kama ulitaka Mbowe ashtuke bado tu angejifanya ameanguka na watu mkaamini(kama yeye amehusika), kwa hiyo hoja ya kushtuka haingii akilini.Watu wametofautiana kuabsorb shocks, na perception za watu zimetofautiana.Ulitaka afanye nini kaka?Nimeona watu wakiact kuwa wamezimia kumbe ndio walioua!
6.Je katika kusema hivyo no matter umepata wapi taarifa hii, je wewe mawazo yako ni nini? unataka kutoa conclusion gani? usizunguke mbuyu?
7.Je wewe ukipata msiba huwa unareact vipi tujue kuwa umeshtuka, katika misiba yote uliyowahi kusikia( here I am talking about your personal experience).?
8.Hiyo picha kwenye jina lako ni nani Mkapa au?
Waberoya
Don't let school interfere with your education
Kevo,
Sikuwa na nia ya kuchangia katika thread hii zaidi ya kusoma na kuacha kama ilivyo. Lakini ninaomba turudishe kumbukumbu zetu nyuma hasa pale unaposema kuwa '...ni upandikizaji wa chuki...' Kama ulikuwa ni mfuatiliaji makini wa wanasiasa wa Tanzania katika kampeni za urais 2005, Mh Mbowe ndiye aliyekuwa anasema kuwa lazima apandikize chuki kwa wananchi ili waichukie serikali yao. Wacha siasa zifanye kazi za wanasiasa!
Gembe toa vielelezo; sie tupo hapa Bongo yetu hakuna kitu kama hicho; wewe ni mzushi uliye majuu au unapata habari ambazo sio credible?
Kwa hiyo its eye for an eye siyo?
Chuki inalipizwa kwa chuki?
Simply coz alishawahi kufanya ama kusema hivyo ndio alipiziwe?
Tuone tutafika wapi tukiendelea na mambo kama haya!
Tena huu ni wakati Mzuri kwa kuwa tuanelekea kwenye uchaguzi wa TARIME ambao utafanyika tarehe 12 october 2008.Ni vyema tukajenga tabia ya kuwasilikiza hawa viongozi wetu wanapoongea na baadae tuje tuwapime kwa matendo yao. Ni mara kadhaa Mh. Mbowe ambaye aligombea urais wa nchi alihubiria wale anaotaka kuwaongoza wawe na tabia ya chuki. Kumbuka kuwa 'wimbo mbaya habembelezewei mtoto' Kama ni chuki ambazo unaziona zikimlenga Mh. Mbowe unadhani nani alizipandikiza?
Ni wakati mwafaka sasa wa kuwakumbusha hawa viongozi wetu kuwa wawe makini kwa yale wanayoyaongea, 'watanzania siyo mabwege tena'
Ni vyema tukajenga tabia ya kuwasilikiza hawa viongozi wetu wanapoongea na baadae tuje tuwapime kwa matendo yao. Ni mara kadhaa Mh. Mbowe ambaye aligombea urais wa nchi alihubiria wale anaotaka kuwaongoza wawe na tabia ya chuki. Kumbuka kuwa 'wimbo mbaya habembelezewei mtoto' Kama ni chuki ambazo unaziona zikimlenga Mh. Mbowe unadhani nani alizipandikiza?
Ni wakati mwafaka sasa wa kuwakumbusha hawa viongozi wetu kuwa wawe makini kwa yale wanayoyaongea, 'watanzania siyo mabwege tena'
Mkuu mimi sikubishii!Kama alisema watu anaotaka kuwaongoza wawe na chuki mimi sijawahi kusikia kitu kama hiki na wala sitapinga wala kukubaliana na wewe maana I did not know about this!
Ila hata kama alisema kwa hiyo dawa ni kumlipishia kwa kumchafulia jina?
Please!!!!!!!!!!!