Kiongozi wa upinzani Uganda, Kizza Besigye aanguka ghafla mahakamani, akakimbizwa hospitalini

Kiongozi wa upinzani Uganda, Kizza Besigye aanguka ghafla mahakamani, akakimbizwa hospitalini

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Dkt. Kizza Besigye, ameanguka ghafla akiwa ndani ya kizimba cha Mahakama Kuu mjini Kampala leo wakati kesi yake ya uhaini ikiendelea kusikilizwa.

Besigye alisikika akipaza sauti akiomba mahakama isimamishe mwenendo wa kesi kabla ya kuanguka, hali iliyosababisha shughuli za mahakama kusitishwa na wahudumu wa afya kumkimbilia.

Baadae Besigye alionekana akiondolewa mahakamani kwa gari la wagonjwa huku hali yake ikielezwa kuwa ya kutatanisha.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 70 amekuwa rumande tangu Novemba 2024 akikabiliwa na mashtaka ya uhaini ambayo yeye na wenzake wanayakana, huku maombi yake ya dhamana yakikataliwa mara kadhaa.

 
Back
Top Bottom