Kiongozi wa Waasi Syria Ahutubia Ulimwengu, Atuma Ujumbe Mahsusi kwa Iran, Atumia CNN, Na Siyo TV za Nchi za Kiarabu

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,362
Reaction score
48,879
Kiongozi mkuu wa Waasi, bwana Abu Jolani ametoa hotuba ambayo imetafsiriwa ililenga zaidi kuuambia Ulimwengu ni nini anakusudia kwa Taifa la Syria. Ameitolea hotuba yake ndani ya msikiti mkuu wa kale zaidi, msikiti wa Ummayad.

Aliichagua CNN kuirusha hotuba yake live, wachunguzi wa mambo wakidai kuwa aliulenga Ulimwengu, hasa nchi ya Iran, Marekani na Israel.

Kwa Iran, ujumbe wake upo wazi na umenyoka, kuwa Iran itambue kuwa Syria haitatumika tena kama nchi ya kuendeleza matakwa yake ya kuyajenga makundi ya kigaidi kama Hezbollah.

. “This new triumph, my brothers, marks a new chapter in the history of the region, a history fraught with dangers (that left) Syria as a playground for Iranian ambitions, spreading sectarianism, stirring corruption,” he said.

Lakini kwa upande mwingine alitaka kupeleka ujumbe kwa Marekani ambayo ilikuwa imetenga zawadi ya Dola 10 milioni kwa yeyote atakayesaidia kupatikana kwa yeye Abu Jolani alipokuwa mpiganaji wa Al Qaeda. Ni dhahiri anataka Marekani na Israel imwondoe kwenye orodha ya magaidi wanaotafutwa, kwa vile yeye ni mtu mstaarabu atakayeiongoza Syria kuelekea kwenye ustaarabu.

“Syria is being purified,” he said, referring to the country’s regional reputation as a narco-state, saying Assad’s Syria had “become the world’s leading source of Captagon,”.

Hotuba yake ilifuatiliwa na Rais Biden, ambaye baadaye ameeleza kuwa hotuba hiyo ni nzuri, lakini itabudi kusubiria matendo.

Speaking a few hours later, Biden said he had heard Jolani “saying the right things,” but insisted the rebel leader be judged by his actions.

Siku kadhaa zilizopita, Jolani akihojiwa na CNN alisema kuwa aliamua kujitenga na makundi ya wapiganaji wa Al Qaeda, kwa sababu hakuafiki kabisa matendo yao ya ukatili.

Tumwombee Abu Jolani na wenzake watakaounda Serikali, waipeleke Syria kwenye mwanga na amani. Syria ipo kwenye nafasi nzuri ya kukomesha makundi ya kigaidi ya Iran, kwani Iran haiwezi kuwafikishia silaha makundi ya kigaidi kama Hezbollah nchini Lebanon, bila ya kupitia nchini Syria.
 
Good ameshasamehewa tayari
 
Achape kazi ashirikiane na Marekani pamoja na Israel hakuna shida atapata
Mmarekani hana rafiki hasa ukiwa na malighafi never,either Mossad or CIA watafanya kazi yake very soon,ingawa nguvu ya kumtoa Assad wao ndio wamempatia ila hii haijaisha bado trust me,ametumia cnn kwakua walikua nyuma yake wkt anapigana
 
Aruhusu tu ndoa za jinsia mbili atakublika na Marekani bil shida yoyote
 
Back
Top Bottom