Kiongozi wa waismailia Aga Khan katika Tanganyika ya kikoloni

Kiongozi wa waismailia Aga Khan katika Tanganyika ya kikoloni

Bhachu,
Mie nakusihi tujadili hii mada ya Ismailia huko unakokwenda si mada yetu.

La unataka tujadili hilo bora ufungue uzi mpya.
 
Kituko,
Madrasa ni shule.
Darsa ni darasa na darasa ni shule.

Hivi wewe shule hadi pawe na kuta, milango na madirisha?

Sisi kwetu maalim anaweza kusomesha bila ya jengo na
ilm yote hii iliyopo Afrika ya Mashariki imesomeshwa kwa
mtindo huo.

Haya ndio maneno yako
"Sababu ya kujenga shule hii ni kuwa wazee wetu na wao walitaka wawe na mahali pa kuwasomesha watoto wao kuepuka vijana wao kubatizwa katika shule ambazo serikali ya kikoloni iliziweka mikononi kwa kanisa"
Na ndipo hoja iliposimamia, so kabla ya hapo palikuwa hakuna elimu ya dunia, Fizikia, Kemia, Hisabati (acha kuhesabu), Swali ni kwa nini kwa miaka yote hiyo Waarabu hawakujenga shule za masomo hayo, zaidi ya masomo ya dini?
Kama kujua kuhesabu, kila Kabila linajua kuhesabu na kila Kabila lina aina zake za kuhesabu, iweje Wazungu walipokuja kufundisha kuhesabu liwe tatizo kwa waislamu?, vipi kuhusu makabila yaliyoamka na kujikuta hayajui tena kuhesabu?
 
Kituko,
Jibu nishakupa.

Ukitaka nikupe jibu utakaloridhia hili haliwezekani.

La unauliza mchango wa Uislam katika elimu fungua uzi nitakuja kukupa darsa.
 
Yeah kujua kama muhamad alikao katoto ka miaka Tisa na kuahidiwa bikra 70 na mito ya pombe peponi

Wanamajlis,
Huyo hapo chini ndiye Chief Kimweri wa Vuga:

XBnaxSqMnu82y8Q0gcMnrwlthbdArzmDvFv72slbyhl5l3u4FiDoSutRdMJIT7xpBrd2U16FQyLIfEo4QZMm1dhPrRZoipnOp6ufls3BtG3pD8FinjRgZZnZqma5sH_tthM7-bbduTg9fprPs7452Ix9x3OPObx3waGRO09WXyMGAM1IPLuAeZ4k-5Y1X3QWByTtS9epjVP1v4Gw3zsRZTFs-ac-pp6qvF3WzDtpt9XJ7bnfWy3ilWp6KVMTQnpV8o9S0ayP4_D_vwTmfbYfT3DHZvlKoUYJlBPP5-7xG3JxiTN0uy1USqmYAfXcA1fEKayehnGO2kgpojgAzYB-NXwtuRSZ4yHytY4U7v34mCnki1JPvtuwOCJCX_tUmMxZb6UuaxMnxFlA6hBAP02B4lhXrp7SVksJIvrVuxVdiTcNt6V95nhRbABIxlHQXt010ZTkVR50oaEbwg-A0B20WQCvM4flafsL_PM0ris7z7mRUe550VY8gCKjZvagMwATfFm3mg95AfX4oM47C4C8NelwNrwpF_ByDxYknlKFcGhpt4sYR0RjL6jSX44aoUPgNNX6SJ64tjZV3ZHnjkIrbEvaAumnBkiH_WO2aUT3xTc=w355-h627-no

Ingiza akili mwako kuwa Krapf katika akili yake alivyotoka kwao Ujerumani
anajua anakuja Tanganyika atawakuta watu wanaishi katika miti sasa anafika
Vuga anamkuta Chief Kimweri kavaa kazu na joho na kapiga kilemba yuko
katika barza lake anahukumu huku akisoma na kuandika kwa hati za Kiarabu.
 
''...zitasomesha Qur’an pamoja na masomo mengine.''

Kipaumbele cha waislam ilikuwa Ilm akhera halafu kwa mbali elimu dunia. Vijana wengi wa kiislam walikosa elimu dunia tokea zamani na ndio maana hili jambo limewatesa kwa muda mrefu na kuanza kushambulia wakristo kuwa wanawanyonya huku wakisahau wakristu wao waliwekeza katika elimu yenye manufaa zaidi.
Hawakuwekeza bali mfumo uliwababa
 
Hawakuwekeza bali mfumo uliwababa
Mimi si muhenga ila huwa napenda kujua na kudadisi mambo. Ningependa kujua mfumo gani uliwabana kama waliweza kujenga skuli na kuwekeza katika Elimu ya kiarabu na kuacha elimu dunia ambayo ingewapa ujuzi mbalimbali.
 
Kodi za waislam zilikusanywa na mkoloni na wakapewa wamisionari waendeshe shule Tanganyika, Mkoloni akaweka sharti la kumbatiza kila mwanafunzi na kumpa jina la kikoloni kitu ambacho waislamu wengi wenye akili wakalikataa hilo sharti la kipuuzi.
 
Chachu Ombara,
Naam Qur'an kwetu sisi ndicho bora zaidi
lakini wazee wetu hawakupuuza
elimu ya sekula na ndiyo maana umeona wakajenga shule.

Baada ya uhuru 1961, mwaka wa 1962 Waislam walifanya mkutano wa
kwanza, Muslim Congress na wakaweka azimio la kujenga shule na chuo
kikuu.

Hii ni historia ya pekee katika historia ya Waislam wa Tanganyika na kwa
urefu kabisa nimeeleza yaliyotokea kati ya serikali na uongozi wa Waislam
chini ya East African Muslim Welfare Society (EAMWS) ilipodhihirika kuwa
kwa mipango hiyo Waislam watajinasua katika mtego wa elimu uliokuwa
umetegwa na wakoloni wakishirikiana na wamishionari.

Hiki ni kisa maalum kipo katika kitabu cha Abdul Sykes.

Asante kwa majibu mazuri ila ningependa kueleweshwa juu ya sentensi nilizo bold.

Naam Qur'an kwetu sisi ndicho bora zaidi - Sijawahi kusoma Qur'an kutokana na lugha iliyotumika na inayotumiwa kufundishwa, huwa naamini hakuna Waislam bila kiarabu. Najiaminisha kwamba kwenye Qur'an hakuna elimu zaidi ya imani na dini hivyo kuipa kipaumbele kabla ya elimu dunia ilikuwa ni kuwanyima fursa nyingine za ajira zinazohitaji ujuzi katika sekta fulani.

Waislam watajinasua katika mtego wa elimu uliokuwa umetegwa na wakoloni wakishirikiana na wamishionari - Ningependa kujua ni mtego gani waislam walitegwa na wakoloni na wamishionari? Au ndio suala la kubatizwa katika ukristu.
 
Kodi za waislam zilikusanywa na mkoloni na wakapewa wamisionari waendeshe shule Tanganyika, Mkoloni akaweka sharti la kumbatiza kila mwanafunzi na kumpa jina la kikoloni kitu ambacho waislamu wengi wenye akili wakalikataa hilo sharti la kipuuzi.

Kabla ya mkoloni kuja alikuwepo mwarabu, yeye kodi alifanyia nini? Kuna waislam wengi wamesoma shule za wamisionari ila hawakubadilishwa dini wala kubatizwa, hizo sababu naona hazina mashiko.
 
Kabla ya mkoloni kuja alikuwepo mwarabu, yeye kodi alifanyia nini? Kuna waislam wengi wamesoma shule za wamisionari ila hawakubadilishwa dini wala kubatizwa, hizo sababu naona hazina mashiko.
Mwarabu hajaitawala Tanganyika hata siku moja. Angeiitawala maendeleo yangekuwa juu sana. Huwezi kufananusha maendeleo ya waarabu na haya ya Afrika ingawa unasema hawakusoma kikoloni.
 
Mimi si muhenga ila huwa napenda kujua na kudadisi mambo. Ningependa kujua mfumo gani uliwabana kama waliweza kujenga skuli na kuwekeza katika Elimu ya kiarabu na kuacha elimu dunia ambayo ingewapa ujuzi mbalimbali.
Chachu Ombara,
Wakati wa ukoloni elimu ilikuwa katika mikono ya serikali na wamishionari na
shule za mishionari zikipewa fungu na serikali kuziendesha kupitia Grant in Aid.

(Grant-in-aid - Wikipedia
Grant-in-aid - Wikipedia
A grant-in-aid is money coming from central government for a specific project. This kind of funding is usually used when the government and parliament have decided that the recipient should be publicly funded but operate with reasonable independence from the state).

Hii ilikuwa kutoka miaka ya 1920 katikati.

Waislam walipoanza na wao kujenga shule zao katika miaka ya 1940 na wao
wakaomba wapewe fungu ili waziendeshe kwa ufanisi kama wamishionari.

Serikali ya kikoloni ikakataa kuwaingiza katika Grant in Aid.
Sasa ningependa kukueleza kuwa hapakuwa na Elimu ya Kiarabu.

Kilichokuwapo ni elimu ya dini ya Kiislam ambayo hii hadi leo iko katika uhimili
madhubuti wa Waislam wenyewe.

Hizi ni madras ambazo wala si lazima maalim awe na jengo anaweza hata kwenye
kibaraza au upenu wa nyumba akasomesha na wanafunzi wakahitimu.

Katika miaka ya 1970 wakati wa Nguvu Kazi ya Edward Sokoine walimu wa madras
waliorodheshwa kama watu wasio na kazi.

Nataka nikufahamishe kuwa mimi nilimwandikia barua Waziri Mkuu Edward Soloine
na kumfahamisha kuwa hilo ni kosa hatutafunga madras zetu kwa hiyo Nguvu Ngazi.

Nakumbuka katika barua yangu nilimtaja Rashid Kawawa na kuomba asaidie kuileza
historia za madras katika Tanganyika.

Barua yangu ilijibiwa na Ofisi ya TANU Lumumba wakiniomba nifike ofisini kwao ili
wanieleweshe.

Jibu nililowarejeshea lilikuwa wa kuelimishwa si mimi bali ni Waislam ndiyo waelezwe
tatizo liko wapi.

Sikupata jibu lakini madras zikaendelea hadi hii leo na hakuna mwalimu yeyote wa
madras alikamatwa katika operesheni ya Nguvu Kazi.
 
Kabla ya mkoloni kuja alikuwepo mwarabu, yeye kodi alifanyia nini? Kuna waislam wengi wamesoma shule za wamisionari ila hawakubadilishwa dini wala kubatizwa, hizo sababu naona hazina mashiko.
Chachu Ombara,
Usipuuze hili la Waislam kubadilishwa dini.
Lilikuwapo na ipo mifano mingi sana.

Lakini ukitaka wewe uweze kujua saikolojia ya Muislam katika suala
la Mungu ni lazima ukae chini usome na kuzingatia.

Vinginevyo wewe utaona si jambo kubwa na utashangzwa kwa nini
mzazi amzuie mwanae kusoma shule ya misheni.

Hiki ni kitu muhimu sana kwako kujifunza.

Soma hapo chini niliyokutananayo wakati nafanya utafiti wa kitabu
cha Abdul Sykes:

''Ili kuepuka mgongano na Waislam wamishonari walikuwa wamejenga kanisa kubwa sana juu ya kilele cha mlima maili chache toka Mikindani sehemu moja ikijulikana kama Mchuchu. Karibu na kanisa walikuwa wamejenga shule ambayo Alfred Omari alikuwa akifundisha. Baba yake Alfred alikuwa Mmakua Muislam lakini mwanae alibatizwa kwa ajili ya kupata elimu. Inasemekana Mwafrika wa kwanza kusoma shule ya misheni kule kusini alikuwa Charles Suleiman. Huyu alikuwa kijana wa Kiislamu aliyebatizwa na wamishonari. Alikuja kuwa Mwafrika wa kwanza kufuzu ualimu katika miaka ya mwishoni ya 1800.''
 
Bhachu,
Mie nakusihi tujadili hii mada ya Ismailia huko unakokwenda si mada yetu.

La unataka tujadili hilo bora ufungue uzi mpya.
NAAM MOHAMED SAID..... HIVI KWA NINI WAMISHONARI WALIWAFANYIA ROHO MBAYA WAISLAM KTK ELIMI ILHALI WAO ZAMA ZA ULAYA KTK UJINGA WAKIELIMISHWA NA WAISLAM BILA UBAGUZI???

KWA NINI?
 
NAAM MOHAMED SAID..... HIVI KWA NINI WAMISHONARI WALIWAFANYIA ROHO MBAYA WAISLAM KTK ELIMI ILHALI WAO ZAMA ZA ULAYA KTK UJINGA WAKIELIMISHWA NA WAISLAM BILA UBAGUZI???

KWA NINI?
Katununu,
WalikuWa na hofu kubwa na Uislam
 
Katununu,
WalikuWa na hofu kubwa na Uislam
KWA HIYO NAWEZA KUWA SAWA NIKIDHANI KUWA MPAKA TUNAPATA UHURU MKAKATI WA UKRISTO KATIKA AFRIKA ILIKUWA SIO CO EXISTENCE NA UISLAM BALI ELIMINATION(KWA KUSHIRIKIANA NA AKINA NYERERE) , YAANI KUUTOKOMEZA UISLAM SI TU AFRIKA MASHARIKI BALI DUNIA NZIMA????
 
Tanga Schule.jpg
Sio kweli,shule ya kwanza ya secondary,Tanganyika ilijengwa Tanga,na mpaka le ipo katikati ya jiji la Tanga,inaitwa Old Tanga Secondary School,ni shule ambayo ina maendeleo mazuri kabisa,na ni shule ambayo mpaka leo iko katika hali yake ya ujenzi wa kihistoria.Na vile vile shule ya kwanza ya secondary kujengwa baada ya Uhuru,ni Tanga School,shule hii ipo mpaka leo.Shule hizi ndio za kwanza,na ziko katika mji uliokuwa na waislamu wengi.
Hizi shule ,kuna mchango mkubwa wa wazee wa kiislamu,wakiwemo waarabu na waafrika.
Mjenzi wa shule ya Tanga ilikuwa serikali ya kikoloni ya Kijerumani mnamo mwaka 1892. Sababu haikuwa mahitaji ya wenyeji wa Tanga lakini mahitaji ya serikali ya koloni kupata wazalendo walioandaliwa kufanya kazi ya mafundi, makarani na walimu kwenye shule (chache) za vijijini. Shule hii ilianzishwa na serikali ya Wajerumani kwa sababu kwa upande moja walikuwa wakati mwingine na mashaka kuhusu shule za wamisionari na kwa upande mwingine katika miaka ya kwanza ya koloni walitegemea zaidi watumishi kutoka pwani kwa kujenga utumishi wa serikali yao na hapa waliona ya kwamba Waislamu wa Pwani waliogopa kupeleka watoto katika shule za misioni (na sehemu ya shule hizi ilipokeas watoto wa Wakristo pekee). Kutegemea watu wa pwani ilikuwa pia sababu ya kwamba Wajerumani waliamua kufanya Kiswahili kuwa lugha rasmi katika koloni yao ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (DOA).
Hapa picha ya shule ya Tanga mnamo mwaka 1910
 
View attachment 712040

Kipala,
Ahsante sana kwa historia hii.
 
Back
Top Bottom